Karibu nyumbani Miss

Author

Mrembo aliyevikwa taji la Miss Tanzania nambari mbili, Lilian Kamazima anatarajiwa kuwasili leo mjini Arusha na kupokewa kwa shangwe akiwa na taji lake.

Taarifa iliyotolewa na mkurugenzi wa Kampuni ya Mwandago Entertainment Ltd, Faustine Mwandago iliyosimamia ushindi wake ngazi ya kanda ilisema kuwa mrembo huyo atawasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kia) saa 6:00 mchana.
Mwandago alisema kuwa mrembo huyo atapokelewa na wenyeji wake, wakiwamo wazazi wake na kisha kupanda gari la wazi ili kuwapa fursa wakazi wa Arusha kumshuhudia.
Alisema kuwa mara baada ya kuwasili Arusha atapelekwa moja kwa moja nyumbani kwao, Sakina ili kushiriki hafla aliyoandaliwa na wazazi wake pamoja na ndugu, jamaa na marafiki.
Wakazi wa Arusha wametakiwa kujitokeza kwa wingi kumpokea mrembo huyo kwa lengo la kumpa moyo na kulikaribisha taji hilo mara baada ya ukame wa muda mrefu wa kupata taji la Miss Tanzania.

0 comments:

Post a Comment