kwa habari za michezo

fahamu ya liyojiri,ratiba na matokeo

kwa miziki

taarifa za miziki,nyimbo mpya na mengineo

dunia yetu leo

fahamu ya tokeayo duniani.

Showing posts with label MUSIC. Show all posts
Showing posts with label MUSIC. Show all posts

NIFANYE NA MIMI KAKA DICK -01

Author

 CHOMBEZO LA KUSISIMUA: NIFANYE NA MIMI KAKA DICK

IMEANDIKWA NA: JUMA HIZA

SIMU: 0712988278

_______________


SEHEMU YA 01.


Nakumbuka nilikutana naye Game, Mlimani City. Alionekana kuwa msichana mrembo, kuanzia sura pamoja na umbo lake matata. Kwa mara ya kwanza nilipomtazama nilijikuta nikitamani kuwa naye kimapenzi, sijui hata hisia hizo zilitokea wapi?

Akili yangu ikanituma nimfuate na kumueleza kile nilichokuwa nakitamani kwa wakati huo lakini moyo wangu ulisita. Ulinyong’onyea kutokana na aibu iliyonikumba ghafla!

Alionekana kuwa bize akifanya shopping lakini hilo halikunitisha hata kidogo, nilichokifanya ni kuanza kuzihesabu hatua zangu kuelekea pale alipokuwepo huku kimoyomoyo nikijisemea ‘liwalo na liwe’.

“Mambo,” nilimsalimia huku usoni nikilitengeneza tabasamu pana.

“Safi,” alinijibu huku akionekana kuwa bize na shopping yake.

“Unaonekana kuwa bize sana vipi naweza kukusaidia?”

“Hapana ahsante, nashukuru.”

“Ahsante maana yake nini?”

“Yaani namaanisha nashukuru, ahsante kwa msaada wako.”

“Okay! Vipi naweza kukuuliza jina lako?” nilimuuliza huku nikijifanya kama ninayetafuta kitu fulani hivi kwa kuzuga.

“Kwani kuna ulazima wa kulifahamu jina langu kaka?” alinijibu kwa kuniuliza swali lililonifanya nimuone kuwa msichana wa matawi ya juu sana. Alikuwa hapendi mambo kujuana juana sana, kwa kifupi naweza kusema alikuwa ni msichana fulani hivi wa gharama.

“Sio lazima kulifahamu lakini kama hutojali ningependa kulifahamu?”

“Wewe kaka vipi, hivi utafahamu wangapi wanaoingia supermarket hii au wewe ni mwizi nini?” 

“Ndiyo mimi ni mwizi, nataka kuliiba jina lako. Kwani kuna ubaya?” nilimjibu kwa kutania na kumfanya atokwe na kicheko cha bila kukitegemea.

“Wewe kaka umetumwa nini?”

“Ndiyo nimetumwa na moyo wangu nikuulize kuwa unaitwa nani?”

“Sitaki.”

Mpaka kufikia hapo nilikuwa nimeshafahamu kuwa alikuwa ni msichana wa aina gani, alikuwa ni miongoni mwa wale wasichana ambao wanapenda kubembelezwa, yaani wao kila kitu ni kubembelezwa tu. Nililifahamu hilo na sikutaka kulifanyia kazi, niliendelea kumsumbua mpaka pale uvumilivu ulipomshinda.

“Haya naitwa Evadia,” alijitambulisha huku akionekana kuchoshwa na usumbufu wangu.

“Nafurahi kukufahamu,” nilimwambia kisha nikampa mkono lakini hakuupokea, aliupuuzia. Hilo halikwa tatizo kabisa, niliendelea na usumbufu wangu kama kawaida.

“Naitwa Dickson lakini wengi wanapenda kuniita  Dick mapenzi,” nilijitambulisha kisha nikaanza kuondoka eneo lile kimitego, kuna kitu nilichokuwa nikikitegemea kwa wakati huo.

Sikumbuki ni nini kilitokea lakini nilishangazwa sana na mshangao uliomkumba Evadia mara baada ya kumtajia jina langu. Alinitazama mara mbilimbili kisha akawa kama mtu ambaye haamini kile alichokuwa akikishuhudia kwa macho yake.

Alilirudia kuliita jina langu halafu akanitazama usoni, safari hii ule ubize aliokuwa nao ulimuisha, akanitazama tena huku akiwa haamini kabisa kukutana na mimi mahali pale.

Labda nikuambie kitu ndugu msomaji, nilikuwa na jina kubwa sana mitandaoni, hakukuwa na mtu ambaye alikuwa ni mtumiaji wa mtandao wa Istagram na Facebook halafu akawa halifahamu jina langu. Wengi walikuwa wakinifahamu kutokana na hadithi zangu aina ya chombezo nilizokuwa nikiziandika katika mitandao hiyo, nilikuwa nikiongoza kuwa na wafuatiliaji wengi (Followers).

“Dick,” aliniita kwa mshango.

“Naam,” nilimuitikia halafu nikamgeukia, akazidi kunishangaa tu.

“Ni wewe kweli?” aliniuliza.

“Yeah! ndiyo mimi,” nilimjibu huku nikimrudia, safari hii nilijifanya kubadilika kidogo, sikutaka anielewe nilikuwa ni mtu wa aina gani.

“Kwani unanifahamu?” nilimuuliza.

“Ndiyo nafuatilia sana simulizi zako mitandaoni yaani kila siku nilikuwa natamani siku moja nikuone maana sio kwa simulizi zile za mapenzi unazotunga,” aliniambia kisha akaja na kunikumbatia.

“Siamini,” aliniambia wakati huo nilikuwa nimekumbatiana naye.

“Huamini nini?” nilimuuliza.

“Yaani kukutana na wewe kwangu ni bahati kubwa sana.”

“Usijali,” nilimwambia kisha nikajitoa katika kumbato lake.

Evadia hakutaka kuamini kama alikutana na mtu kama mimi ambaye nilikuwa nikisifika sana, wasichana wengi walitamani kuniona lakini lilikuwa ni jambo gumu, hii ilitokana na ubize niliyokuwa nao, nilishindwa kukutana nao kwa wakati.

Niliishia kuzungumza na wasichana hao kwenye simu huku wengine niliishia kuchati nao tu. Kila msichana alikuwa akionekana kunipenda na hilo ndilo lilikuwa kosa kubwa walilolifanya na wote ambao walijilengesha mtegoni sikuweza kuwaacha salama, nilihakikisha nafanya nao mapenzi.

Alichoamua kukifanya Evadia kwa wakati huo ni kuitoa simu yake aina ya I phone 6 yenye  gharama ya zaidi ya shilingi milioni moja kisha akaniomba kupiga selfie na mimi, sikuwa na sababu ya kumkatalia, nilikubali na picha zikaanza kupigwa mahali hapo.

Nilichokuwa nikikiwaza kwa wakati huo ni jinsi gani ningeweza kumpata msichana huyo ambaye alikuwa amenivutia kupita kawaida.

“Unajisikiaje?” nilimuuliza huku nikimtazama, alionekana kuwa mwenye furaha sana.

“Nimefurahi sana Dick yaani sikutegemea kama kuna siku ningekuona,” alinijibu.

“Unaweza kunipa namba yako ya simu?” nilimuliza lakini kabla ya kunijibu nikashangaa akiingiza mkono katika pochi yake ndogo kisha akatoa ‘business card’ halafu akanipa.

“Utanitafuta,” aliniambia.

“Muda gani nikutafute?” nilimuuliza.

“Muda wowote kuwa huru Dick,” aliniambia.

“Ahsante sana,” nilimjibu.

Sikutaka kupoteza muda, nilimuaga kisha nikataka kuondoka mahali hapo.

 “Kwani unaenda wapi?” aliniuliza.

“Kuna sehemu nataka kwenda,” nilimjibu.

“Kwahiyo umeghairi kufanya shopping?”

“Hapana nitafanya nikirudi,” nilimjibu kisha nikaanza kuondoka eneo hilo.

Evadia alizidi kunitazama, nililifahamu hilo pale nilipogeuka na kumuangalia, alikuwa akinitazama muda wote. Nilichukua maamuzi ya kuondoka lakini akilini nilikuwa nikiwaza ni njia gani ningeitumia ya  kumpata.

Niliamini kupitia kipaji changu cha kuandika simulizi na machombezo ndicho ambacho kingeweza kunirahisihia kazi yangu hiyo na kuwa nyepesi kabisa.

“Msichana mrembo kama wewe lazima nikumiliki tu,” nilijiambia kisha nikatabasamu.

Nilipotoka nje ya supermarket hiyo eneo la kuegeshea magari, macho yangu yaliendelea kushuhudia wasichana wengi warembo waliyokuwa wakiingia na kutoka ndani ya jengo hilo la Mlimani City.

Macho yangu yalitua kwa msichana mmoja ambaye alikuwa akilielekea gari aina ya Land cruser prado lenye rangi nyeusi. Alikuwa na sura ya mvuto, kiuno kichoingia ndani kama mdudu nyigu. Alitamanisha kupita kawaida.

Nilipomtazama nilikumbwa na mshangao wa ajabu, niliendelea kumtazama mpaka pale alipogundua nilikuwa nikimtazama.

“Wewe kaka vipi?” sauti yake nyororo ndiyo iliyonigutua kutoka katika bumbuwazi zito lililonikumba muda huo.

“Vipi kuhusu nini?” nilimuuliza.

“Mbona unanitumbulia mimacho yako muda wote?” 

“Kwani kuna ubaya nikikutazama?” 

“Hakuna ubaya lakini umezidi kha!” aliniambia kisha akaubetua mdomo wake, alizidi kuonekana kuwa mrembo mno.

“Yaani siamini hata kidogo,” nilimwambia huku macho yangu yakiendelea kutalii vyema kifuani mwake, alikuwa na chuchu zilizosimama dede.

“Huamini nini?” aliniuliza.

“Hivi kumbe Tanzania bado kuna wasichana warembo?” nilimuuliza swali la kizushi lililomfanya anishangae.

“Kwani umesikia hawapo?”

“Nina miaka kama kumi hivi sijawahi kumuona msichana mrembo kama wewe, wote naishia kuwasoma katika simulizi,” nilimuambia maneno yaliyomfanya atokwe na tabasamu lililotengeneza vishimo vidogo mashavuni mwake.

“Halafu kumbe unajua kuficha siri?” nilimuuliza huku nikijifanya kama nimeshtuka kwa kuona kitu ambacho sikukitegemea kwa wakati huo.

“Siri gani tena?” aliniuliza.

“Nimesimama na wewe muda wote huo kwanini hujaniambia kuwa una dimpoz?” nilimuuliza swali lililomfanya acheke.

“Mbona unanicheka sasa?”

“Hapana sikucheki.”

“Ila?”

“Umenifurahisha tu.”

“Halafu hujaniambia kitu?”

“Kitu gani?”

“Jina lako?”

“Oooh! Sorry naitwa Precious.”

“Precious ndiyo jina lako?”

“Ndiyo Precious Kamba.”

“Aliyekupa jina wala hakukosea yaani limefit mahali pake kabisa.”

“Kwanini?”

“Jina zuri halafu na wewe mwenyewe pia ni mzuri.”

“Ahsante na wewe unaitwa nani?”

“Mimi naitwa Akili za wote.”

“Ndiyo jina lako?”

“Ndiyo.”

“Unaishi wapi?”

“Tandale kwa tumbo.”

“Tandale?”

“Ndiyo kwani vipi?”

“Hamna!”

“Sawa haina noma.”

“Haya kwahiyo unaingia au unatoka.”

“Nipo katikati.”

“Niambie bana ili kama ni lift nikupe kama hutojali maana naelekea Magomeni napitia Tandale.”

“Dah! nashukuru Precious umeiokoa nauli yangu ya ngama maani sisi wengine kuja supermarket mpaka pawe na sababu maalum,” nilimwambia Precious kisha akacheka.

Tulipanda kwenye gari na safari ikaanza, barabarani hakukuwa kuna kitu kingine nilichokiwaza zaidi ya mapenzi, yaani kwa muda mfupi niliyomuona msichana huyo nilitamani kuwa naye kimapenzi na siku hiyo hiyo pia nilipanga kumlaghai mpaka akubali nimpeleke nyumbani kwangu japokuwa alionekana kuwa mwenye haraka mno.

_________________


HUU NI MWANZO TU. 


Wewe unayesoma kimyakimya hau-Like, ku-Share wala kuComment chochote ndiye unaweza kunifanya niache kuipost simulizi hii hapa niendelee kwenye WhatsApp tu. Nipe ushirikiano nijue uwepo wako humu. FANANI BILA HADHIRA haina maana.😎


Unajua nini kilitokea?

Hebu bashiri, niambie unahisi nini kitatokea?


SHARE KWA MARAFIKI ZAKO ILI TUZIDI KUSONGA MBELE.

UTATA WASANII KUMUAGA RAIS

Author
HAFLA inayotajwa kuandaliwa na “Umoja wa Wasanii Tanzania” ya kumuaga Rais Jakaya Kikwete anayestaafu baada ya uchaguzi wa Okotoba mwaka huu, imezua mjadala mkubwa nchini. Mjadala wenyewe unatokana na kile ambacho wengi wa wasanii wanasema kwamba hawajapata kujua kwamba kuna umoja wa wasanii Tanzania.
Mingi ya mijadala inayoendelea kwenye kota mbalimbali za jiiji la Dar es Salaam pamoja na mitandao ya kijamii yanajadili kwamba kama ni umoja wa wasanii kumuaga Rais kikwete, imekuaje ukumbi umejaa makada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) akiwepo mgombea Urais wa chama hicho katika uchaguzi mkuu huo, John Magufuli.
Hoja kuu hapa ni, Je, umoja huo wa wasanii umeundwa ndani ya mfumo wa CCM? au wasanii waliokuwa mbele katika hafla hiyo walitumika tu kujenga picha kwamba umma wa wasanii Tanzania unamsapoti Magufuli?
Ukweli ni kwamba, katika miongoni mwa wasanii wenye majina makubwa katika tasnia ya filamu na muziki, ukiwemo wa bongo fleva, taarabu, muziki wa injili na dansi, wapo wengi siyo tu ni viongozi katika vyama vya upinzani, pia ni wagombea nafasi za ubunge kupitia vyama hivyo vya upinzani.
Baadhi wa wasanii ambao ni wagombea ni Seleman Msindi ‘Afande Sele’ na Joseph Haule ‘Prof. Jay’. Wasanii waliokuwa meza kuu katika hafla hiyo sambamba na Kikwete ni Jacob Steven ‘JB’ na Nikii wa Pili.
Yafuatavyo ni maswali yanayouliwa katika mijadala iliyopo katika mitandao ya kijamii:-
  1. Umoja huo umeanzishwa lini na viongozi wao kina nani?
  2. Wasanii wanatambua kua kuna umoja wa wasanii tena usiokua na jina rasmi?
  3. Kama wasanii wameungana ili kumuaga rais wa nchi, kwanini kulikuwa na lundo la viongozi wa chama kimoja cha siasa?
  4. Magufuli kupewa nafasi ya kipekee, alienda kama mgombea wa chama, kama waziri au kama mpiga ngoma mtarajiwa wa Twanga?
  5. Nani aligharamia gharama za sherehe?
  6. Wasanii walizipataje hizo pesa za sherehe wakati wenzao wakiumwa hadi waandae matamasha ya kuchangia kwa njia ya kiingilio na hawapati zaidi ya Sh. milioni mbili.
  7. Kwanini wasanii ambao ndio wanaodaiwa kuwa waandaaji waliandaliwa kadi za mwaliko badala ya wao kumuandalia mheshimiwa rais kadi ya mwaliko?

JOKETI AMUONYA DIAMOND

Author
MWANAMITINDO maarufu Jokate Mwegelo amemtaka mwanamuzi maarufu Naseeb Abdul, ‘Diamond ‘ kutomgombanisha na Ali Kiba.
Pia amemtaka mwanamuziki huyo kuacha hulka kudhalilisha wanawake aliowahi kuwa na uhusiano nao nao.
Jokate alitoa kauli hiyo jana kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram baada ya Diamond kuweka video ya wimbo wake inayomwonesha (Jokate) akicheza wimbo wa Mdogomdogo na kuandika ‘Mtanyooka tu’.
Alisema alichofanya Diamond anachokifanya si uzalendo na kuonesha wazi wazi chuki zake.
Jokate alisema kuwa hakuna ubaya yeye kushangilia ushindi wa msanii huyo kwani ni sifa ya taifa kwa ujumla.
” Sijui kwanini ameweka video hiyo au kwasababu nipo karibu na Alikiba anataka kutogombanisha lakini kila mtu anahaki ya kumpenda ampendaye.
“Pengine ni kweli anaendeleza hukla zake za kudharirisha wanawake aliokuwa nao, ili waonekane si kitu kwasababu sasa hivi hawana mahusiano naye,”ameandika Jokati.
Hivyo amemtaka Diamond kubadilika kwani anachokifanya sio watanzania wanategemea kupata kwake, akiwa msanii ambaye anawakilisha vema muziki kimataifa.
Mbali na hayo alimempongeza kwa ushindi wake .

KUMBE BEYONCE ANAMUINGA J.LO

Author
Kila mtu anahusudu mambo ya mwingine na angependa kuwa kama huyo mtu anayemuhusudu. Suala hilo pia liko kwenye sekta ya burudani ambako katika hali ya kawaida wasanii ndiyo hupenda kufanya mambo mapya na hufurahia kuona watu wengine wakiwaida. Hata hivyo, si kwa Beyonce, mwimbaji na mwandishi nyota wa muziki wa Marekani, ambaye aliweka bayana jinsi anavyomuhudu Jenniffer Lopez, maarufu kama J.Lo, ambaye ni mcheza sinema, dansa, mtayarishaji muziki, mbunifu wa mavazi na mwimbaji.
Katika mahojiano na jarida la Espanyol, Beyonce alitoa mwangaza kidogo wa mtu anayemvutia kiasi cha kupenda mafanikio yake. “Bila shaka ni Jennifer Lopez,” alisema Beyonce alipoulizwa na jarida hilo ni mtu gani anamuhusudu maishani mwake. “Napenda historia yake ya jinsi alivyokua akiwa Bronx na mafanikio aliyopata na himaya aliyojijengea. Ni mwanamke mwenye akili. Nilipata nafasi ya kufanya naye kazi wakati wa kutengeneza tangazo la Pepsi. Ana uzuri usiofikirika na mwenye talanta.” Ingawa Beyonce alikuwa muwazi kusema hayo, imekuwa ni dhahiri anapata wapi staili zake za nguo na urembo. Kama kuiga ni aina ya kuonyesha kuhusudu, basi J-Lo atakuwa akifurahia kuona anaigwa na Beyonce. Beyonce ameshaonekana hadharani mara 23 akiwa amevalia nguo alizoiga kwa J.Lo.
Katika picha hizi, Beyonce anaonekana kwenye picha zilizo kulia akiwa amevalia vazi linalofanana na la J. Lo aliye kwenye picha za upande wa kulia.

ALICHO SEMA JOKETI KWA USHINDI WA ALI KIBA

Author

Jokate na Wema Sepetu June 15 2015Mwigizaji Wema Sepetu na staa wa single ya ‘leoleo‘ Jokate ambao wamekuwa kuwa mapenzini na Diamond Platnumz kwa time tofauti baada ya kutolewa tuzo za KILI 2015 nchini Tanzania ambako Ali Kiba alipata ushindi wa tuzo nyingi kuliko yeyote mwingine usiku huo walitumia page zao kumpongeza Kiba kwa kuandika maneno yafuatayo.
Jokate ambaye anatajwa kuwepo mapenzini na Ali Kiba sasa hiv aliandika
 '‘Hongera Sana Cherie @officialalikiba Kwa Kujishindia Tuzo Sita Jana Usiku Kwenye Kiba Tanzania Music Awards (KTMA) sorry Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2015. Teh teh teh. Ni Kitu Cha Kumshukuru Mungu Ulikaa Kimya Miaka 3 Ila Ukarudi Na Wimbo Mmoja Ukatuteka Tena’'
‘Kusema Ukweli Tukiachilia Mbali Ushabiki ‘Mwana’ Ulituliza Akili Na Ukafanya Vizuri Sana Nchini. Mashabiki Wanakupenda. Sana. Mpole Hivi, Mcheshi, Mstaarabu. Na Unajua Mziki. Tunakuombea Sasa Hii Iwe Motisha Ya Wewe Kufika Mbali Zaidi. Ndio Kwanza Safari Imeanza. Uzuri Unaomba Mungu So Najua Hata Kutupa. Ila Kaza Mwana We Kazaaa!!! tuko nyuma yako 💯’  – Jokate
Wema Sepetu aliandika >>> ‘Nilitaka zote saba ila hata 6 pia sio mbaya…. #KingKiba…. Umetisha’
Baada ya Jokate kupost picha ya Kiba na hayo maneno hapo juu…… post iliyofata aliweka picha yake yeye na Wema na kuandika >>> ‘Ni kitu kizuri na chenye nguvu pale Wanawake hodari wanaoungana‘
Jokate na Wema Sepetu June 15 2015 post
Jokate M kuhusu Ali Kiba June 14 2015
Instagram Wema Sepetu June 14 2015 on Ali Kiba kushinda KTMA
Ali Kiba mwenyewe baada ya ushindi huu aliandika “Ningependa Kuchukua Nafasi Hii Kutoa Shukrani Zangu Kwanza, Kwa MUNGU Muumba Aliyenipa Kipaji Hiki, Pili Familia Yangu Kwa Kuniongoza Na Kunipa Moyo Wa Kufanya Kazi Zaidi, My Management, Asante Kwa Kuniongoza Vyema. Mashabiki Zangu Wa Dhati Asanteni Sana Kwa Kuthamini Kipaji Changu Na Kupenda Kazi Zangu! Nawapenda Na Kuwashukuru From The Bottom Of My Heart. MUNGU Awabariki Sana …#KingKiba

MFAHAMU LEYKIZ JEMBE JIPYA LA DX NA NOIZ MAKER

Author
JINA :               LEONS KENGWA A.K.A LEY KIZ

MAHALI:          ARUSHA

KAZI:              MUSICIAN/BIZZNESMAN

KUZALIWA:   04/08/1989  SONGEA



Leons ali anza maisha yake ya muziki akiwa shule ya msingi japo hakuipa uzito sana hadi alipo jiunga na shule ya sekondari ya oljoro mwaka 2004 ambapo walijiunga  wakiwa watatu
Leons Kengwa  [ley kiz]
emanuel daniel [immam daz]
johnson kitalula [black rhino]

Na kutengeneza kundi lililo jipatia umaarufu mkubwa shuleni lililo julikana kama TERO SQUARD
Japo makundi mengi yalijaribu kuleta upinzani kama vile TSUNAMI CAMP ilikuwa chini ya DIZZO BOY na FAVII bado TERO SQUARD ili ibuka mshidi hadi mwalimu wa michezo kuipa nafasi ya kutumbuiza kwenye maafali ya kidato cha nne ya mwaka 2006


Mara tu baada ya kumaliza kidato cha nne nyota ya LEIKIZ iliendelea kung'ara kwani aliendelea kupata nafasi ya kuonyesha kipaji chake katika kumbi  mbali mbali  kila mara kukiwepo tamasha ACTIVE CLUB au TRIPLE A bhasi mara nyingi kabla msanii mkubwa kupanda LEYKIZ amekuwa akipanda yeye kwanza


Leo hii ni muda umepita ila LEY KIZ bado yupo na  bado ana fanya  muziki  ana nyimbo takribani  10
Zilizo achiwa ni mbili

KICHWA KINAUMA   ft  YOUNG  CASH
BOUNCE LIKE THIS    ft  ODINARI
 
Hits zote zimefanywa kwa mkali DX studio ni NOIZ MAKERS 

 BOUNCE LIKE THIS aliyo mshirikisha ORDINARI wa JAMBO SQUARD ikiwa ndiyo habari ya mjini kwa sasa ikipigwa na radio station karibu zote za hapa ARUSHA na kufanya interview na RADIO kadhaa  leo nakuomba uitafute uisikilize kisha utoe maoni yako

kusikiliza nyimbo zote za LEY KIZ ingia hapa

 www.mkito.com
 
0784002688 , 0759428656 ,  UTUMIWE WHATTSAPP

SPECIAL   TENX  KWA CLASS 2007 OLJORO SEC

MAONI /USHAURI

LEONS KENGWA AKA LEY KIZ

  0759428656

                                                                                                  




Msimu mpya wa tuzo za KTMA umezinduliwa rasmi leo

Author
Msimu mpya wa tuzo za KTMA umezinduliwa rasmi leo
Kampuni ya bia ya Kilimanjaro ambayo ndiyo mdhamini mkuu wa mashindano ya tuzo za Kilimanjaro Music Awards wamezindua msimu mpya wa tuzo za Kilimanjaro Music Awards zinazofahamika kama KTMA2015.
Msimu mpya wa tuzo umezinduliwa rasmi leo na kuwa na maboresho kadhaa ikiwepo njia zitakazotumika kupendekeza wasanii na nyimbo kushiriki katika mchakato huo ambapo kwa mwaka huu kutakuwa na njia tatu tofauti na mwaka jana ambapo kulikuwa na njia mbili za kupendekeza na kupiga kura kupata washindi wa tuzo hizo.
Kwa mwaka kuu kuna maboresho katika mapendekezo hivyo mashabiki wanaweza kupendekeza nyimbo au msanii kupitia tovuti,SMS pamoja na Whatsapp.
Monday , 23rd Mar , 2015
Kampuni ya bia ya Kilimanjaro ambayo ndiyo mdhamini mkuu wa mashindano ya tuzo za Kilimanjaro Music Awards wamezindua msimu mpya wa tuzo za Kilimanjaro Music Awards zinazofahamika kama KTMA2015.
Wasanii mbalimbali katika uzinduzi wa tuzo za Kilimanjaro Music Awards (Picha:Library)
Msimu mpya wa tuzo umezinduliwa rasmi leo na kuwa na maboresho kadhaa ikiwepo njia zitakazotumika kupendekeza wasanii na nyimbo kushiriki katika mchakato huo ambapo kwa mwaka huu kutakuwa na njia tatu tofauti na mwaka jana ambapo kulikuwa na njia mbili za kupendekeza na kupiga kura kupata washindi wa tuzo hizo.
Kwa mwaka kuu kuna maboresho katika mapendekezo hivyo mashabiki wanaweza kupendekeza nyimbo au msanii kupitia tovuti,SMS pamoja na Whatsapp.
"Mashabiki watapewa nafasi ya kupendekeza majina ya nyimbo na wasanii wanaostahili kuingia katika kinyang'anyiro na Njia za kupendekeza ni kupitia: Tovuti, Whatsapp na SMS,Mashabiki watapewa nafasi ya kupendekeza majina ya nyimbo na wasanii wanaostahili kuingia katika kinyang'anyiro"
Lakini pia wadhamini hao wakuu wa Tuzo za Kilimanjaro Music Awadrs wamesema kuwa zoezi la kupendekeza msanii na nyimbo yataanza rasmi Machi 30 hadi April 19 huo ndio muda wa mashabiki kupendekeza majina ya nyimbo na wasanii wanaostahili kuingia katika tuzo.


MKUBWA NA WANAE

Author

USIHOFIE WACHAGA BY RAMA DEE

Author


KESI YA CHID BENZ YAHAIRISHWA TENA

Author

Kesi inayomkabili mwanamuziki wa Hip hop nchini, Rashid Makwiro ’Chid Benz’, imeahirishwa tena leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam mpaka Januari 21, mwaka huu.
Mwanamuziki huyo anakabiliwa na kesi ya kukamatwa na madawa ya kulevya katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar wakati akisafiri kuelekea mkoani Mbeya kwa ajili ya kutumbuiza mwaka jana.

#TANZIA AISHA MADINDA AFARIKI DUNIA!

Author


Aliyekuwa mnenguaji wa bendi tofauti hapa nchini Tanzania Aisha Madinda afariki dunia na mwili wake wakutwa umehifadhiwa katika hospitali ya Mwananyamala.

Akiongea na EATV Mkurugenzi wa bendi ya Twanga Pepeta amesema kuwa alipewa taarifa na Daktari mmoja kuwa wameona kama mwili wa Aisha Madinda hospitalini hapo, ndipo akatuma watu kwenda kuangalia akiwemo Luiza Mbutu ili kuhakikisha kama kweli ni yeye ndipo walipogundua ni yeye.

“ Mimi nipo njiani natoka Kigoma kuja Dar es Salaam, ni habari ya kusikitisha sana maana Aisha amefariki katika mazingira ya kutatanisha sana, jana alikuwa mzima na anachati na watu kwenye simu leo napigiwa simu mwili wake umekutwa umehifadhiwa kwenye hospitali ya Mwananyamala, hata sielewi nini kimetokea”. Amesema Asha Baraka

Mungu ailaze roho ya Marehemu Aisha Madinda mahali pema peponi , Amina




INABIDI UKUBALI TU

Author
NAWASILISHA KAMA NILIVYOPOKEA Wow, worth sharing: HONGERA DIAMOND PLATNUMZ! Ngoja niseme kidogo kitu nilichojifunza kwa huyu kijana. Kuna wakati fulani Hezron Michael (Paul Mashauri) aliwahi kuandika kuhusu msanii wa muziki wa bongofleva Diamond akisifia bidii yake lakini sasa naelewa zaidi. Diamond huyu alikuwa hana hela ya kwenda studio mara ya kwanza (mtaji wa biashara) lakini hii hai kuwa kizuizi kwake. Kwa kuwa alitaka kutoka moyoni aisee hela ilipatikana! Ilikuwaje? Mama yake alimpa mkufu akauze ili apate hela ya studio. Na alienda studio. The rest is history. Sasa ili unielewe hapa naomba unisikilize kidogo. Unamjua Joseph Kusaga? Labda humjui. Huyu ni mmiliki wa Clouds FM na Clouds TV. Niliwahi kumsikiliza LIVE akisema kuwa wakati alipopata wazo la kufungua kituo cha redio mtaji "uligomba". Kwa kuwa alitaka saana kufungua redio alimfata mzazi wake akaomba HATI YA NYUMBA ili akakope pesa benki! Can you imagine? Mzazi alimpa akijua hiyo dream ikifa nyumba hawana. Hela ilikopwa nyumba ikawekwa rehani and the rest is history! Unamjua Jeff Bezoz? Kama humjui nisaidie tu kugoogle. Lol. Anyway. Huyu ni moja ya matajiri 20 wakubwa duniani. Hivi sasa akiwa No. 18 kwenye Forbes list utajiri wake ukiwa $32 billion! Lakini huyu bwana wakati anataka kuanzisha mtandao wake wa Amazon..com hakuwa na mtaji. Sasa huyu alichofanya aliwafata wazazi wake ambao walikuwa ndo wamestaafu. Akawaomba pensheni yao ili afungulie biashara. Can you imagine wazazi waliwaza nini? Wanamuuliza biashara gani anawambia ni mambo mapya ya internet nataka niuze vitabu kwa kutumia internet. Hawakuelewa lakini kwa vile alitaka wamkopeshe hiyo pensheni by hooks and crooks aisee walimpa! And the rest is history. Hebu jiulize leo wazazi wake wanaishije? Jiulize mzazi wa Jay Kusaga leo kama anashida ya nyumba (kama yupo hai.. Na kama yu hai aishi miaka mingi zaidi). Jiulize mama wa Diamond Platnumz leo anaishije. Kwanza tunavyoongea hayupo bongo yuko zake Sauzi na mwanaye! Yes. Jiulize kama ana shida ya hela ya kunulia mkufu tena. Sasa wengi mna woga! Ndoto unayo lakini ukiulizwa kidogo tu: We Salome unaomba hela ya biashara ukishindwa hela yangu itakuwaje..? Au ukiambiwa elimu ulishindwa biashara utaweza? Unajiinamia kesho unaenda kwenye mkesha kuomba Mungu afungue njia nyingine! Pshuuu! Hivi humo kichwani kuna maji au? Afu ukisikia watu wanafanikiwa ooh Freemason ooh one day nitamiliki na kutawaka. Tawala kwanza fikra zako! Fursa zinazidi kuja na kukupita uko tu reception unapata laki tatu kwa mwezi na degree yako ya Mass Communication! Pshuuu. Diamond alipouza mkufu hela nyingine alipeleka studio kurekodi nyingine akaenda British Council kusoma English! Mambo ya "Good morning" mambo ya "let me read the contact once again.." nini. Huyu ni mtu anayeona mbali. Wasanii Wangapi walikuwa maarufu kabla yake but hawakuwaza kama yeye. Niwataje? Halafu haohao wanamsengenya na kumponda. Hivi wasomi wangapi wanajua lugha zaidi ya Kiswahili. Honestly. Hivi nitajie wasomi wangapi wameitangaza nchi hii kimataifa kama Diamond Platnumz. Kila siku wasomi tunapost picha za graduation. "Thank God I have made it. Xoxo". You have made what? Joho au? Joho hata wanafunzi wa Nursery School wanavaa mbona. Ilipotokea uvumi kuwa anapewa degree ya heshima kila mtu alisema ooh sijui nini.. Umeitangaza nchi wewe?!! Diamond anasomesha watoto watatu IST. Unajua ada ya IST lakini? Au unadhani naongelea gari IST. Naongelea International School of Tanganyika ambao watoto wa mabalozi wa nchi za nje ndo wanasomeshwa na nchi zao! Huyo ni Diamond Platnumz! Wewe umesomesha wangapi hata shule ya Kata na una Masters ya UDSM sijui ya Mzumbe sijui ya Edinburgh, nk. Mentality is everything. Sasa Mungu akubariki wewe au yeye? Kila siku uko kwenye maombi ya kufunguliwa na kuinuliwa unarudi nyumbani saa tano usiku Diamond anatoka studio saa saba za usiku. Who is hard working? Siku ya mwisho walokole tutaabishwa na watu tunaowaona "namna gani vipi". Mungu atupe ujasiri wa kufanya makuu! Mentality ya utajiri haiangalii elimu. Shigongo na wewe nani kasoma zaidi. Nani tajiri? Nani anaweza kuitwa na rais awambie vijana kwenye TV kuhusu biashara Shigongo au wewe mwenye Degree ya biashara kutoka CBE? Jiulize maswali magumu. Usijipe FALSE HOPES. Ati hata nikikosa hela mbinguni naenda. Sikia wewe, kuna watu hawakwendaga mbinguni kwa sababu tu hawakumvisha mtu aliyekuwa na uhitaji wa Nguo. "Nalikuwa uchi...." Hilo tu. Nilikuwa namchekesha cousin wangu Haruni Leonard kuwa unaweza kwenda mbinguni ukamkuta BOB MARLEY na huku wewe ulikuwa unaimba gospel. Kama unataka kufanikiwa hebu acha excuses. Sina mtaji. Sina muda. Kwani kuna mwenye kiwanda cha kuzalisha muda? Muda
 wa Escrow uliupata. Muda wa kukaa kubadilishana mawazo na watu upate mtazamo mpya huna eti. We kaa hapo? December ndo hiyo imefika! Diamond akirudi hukawii kusikia kaenda ikulu. We roho inakuuma hata kazini kwako tu hutambuliki. Hukawii kusikia kaenda Marekani kufanya shoo. We mwisho wako Tabata Bima Buguruni Posta hata huko hawakujui. Success has nothing to do with your religion but your MENTALITY. AGM

 Diamond Naseeb Platnumz

DIAMOND NA TUZO ZAKE TATU

Author

BAADA YA MAPOKEZI MAZITO HAYA NDIYO MANENO YA DIAMOND
Maneno hayawezi kuelezea ni kias gani nawashkuru kwa support na Mapenzi yenu kwangu.... daima ntaendelea kujituma na kuhakikisha nafanya kazi kwa kiwango changu cha juu ili kwa pamoja tuweze kuleta sifa na Heshima Nyumbani...
( Back from @channeloafrica Music Video Awards...)


CHOAMVA 2014: All the winners

Author
AKA winning Most Gifted Hip Hop

Africa's biggest night in music, the 2014 Channel O Africa Music Video Awards, was once more a massive celebration of the crème de la crème of the music industry.

East and Southern Africa reigned supreme in the form of South Africa's Cassper Nyovest and Tanzania's Diamond who scooped the most awards on the night.

Cassper - who has been on a winning streak this year and most recently celebrated his debut album Tsholofelo going Gold - his catchy club banger "Doc Shebeleza" earned him a win in the Most Gifted Male, Most Gifted Southern and the biggest award of the night the Jameson Most Gifted Video of the Year categories.

Beating the likes of DJ Clock, Tiwa Savage, K.O, Riky Rick, Burna Boy, Emmy Gee including the Prince of Hip Hop himself A.K.A who were also nominated in the latter category.

Bongo Flava recording artist Diamond Platnumz proved that he too is a force to be reckoned with when he took home the Most Gifted Newcomer, Most Gifted Afro Pop as well as Most Gifted East awards for his breakout hit "Number One".

Up against Thembi Seete, Bucie, Lizha James and Seyi Shay, "Eminado" featuring one of the continent's well-respected producers Don Jazzy garnered a win for Tiwa Savage in the Most Gifted Female category.

KCEE won the Most Gifted Duo, Group or Featuring award for his song "Pull Over" which features one of Nigeria's best selling artists Wizkid, beating K.O, who undoubtedly has had one of the biggest songs of the year.

The awards for the equally competitive categories Most Gifted Kwaito and Most Gifted Hip Hop went to Uhuru featuring Oskido and Professor for "Y-Tjukutja" and A.KA for "Congratulate" beating Khuli Chana and Cassper Nyovest respectively.

Other winners included Busiswa (Most Gifted Dance – "Ngoku"), Buffalo Souljah (Most Gifted Ragga/Dancehall– "Turn Up"), Donald (Most Gifted R&B – "Crazy But Amazing") and Olamide (Most Gifted West – "Turn Up").

The only award not determined by public votes, the coveted Special Recognition Award went to Boom Shaka. Channel O paid homage with an honorary performance to the pioneering group that dared to be different and ultimately shaped the Kwaito genre in the '90s.

Bucie and Busiswa took to the stage and joined remaining group members Junior Sokhela, Theo Nhlengethwa and Thembi Seete and paid tribute to fallen band member Lebo Mathosa with an emotional rendition of the group's song "Free", concluding with a spectacular trip down memory lane with the mega hits "Thobela" and "It's About Time".

In their 11th year running and hosted by Siyabonga Ngwekazi and Eku Edewor, the 2014 Channel O Africa Music Video Awards were broadcast LIVE from the sold out mammoth Nasrec Expo Centre.

If you missed it, check out the show repeats on Channel O, DStv channel 320 on:

Monday, 1 Dec at 20h00
Friday, 5 December at 14h00
Tuesday, 30 Dec at 10h00

2014 Winners

Most Gifted Male

Cassper Nyovest - Doc Shebeleza
Davido - Aye
Riky Rick Ft Okmalumkoolkat - Amantombazane
K.O. Ft Kid X - Caracara
Sarkodie - Illuminati

Most Gifted Female

Thembi Seete - Thuntsha Lerole
Bucie Ft Heavy K - Easy To Love
Lizha James Ft Uhuru - Quem Ti Mandou
Tiwa Savage Ft Don Jazzy - Eminado
Seyi Shay - Irawo

Most Gifted Newcomer

Dream Team Ft Tamarsha, AKA & Big Nuz - Tsekede
Cassper Nyovest - Doc Shebeleza
Emmy Gee Ft Ab Crazy & Dj Dimplez - Rands And Nairas
Diamond - Number One
Patoranking - Girlie O (Remix)

Most Gifted Duo, Group or Featuring

Uhuru Ft Oskido & Professor - Y-Tjukutja
Dj Clock Ft Beatenberg - Pluto (I Remember)
R2bees Ft Wizkid - Slow Down
K.O. Ft Kid X - Caracara
Kcee Ft Wizkid - Pull Over

Most Gifted Dance

Uhuru Ft Oskido & Professor - Y-Tjukutja
Davido - Skelewu
Dj Clock Ft Beatenberg - Pluto (I Remember)
P Square - Personally
Busiswa Ft Various - Ngoku

Most Gifted Ragga Dancehall

Buffalo Souljah - Basawine
Orezi - Rihanna
Jesse Jagz Feat Wizkid - Bad Girl
Patoranking - Girlie O (Remix)
Shatta Wale - Everybody Likes My Ting

Most Gifted Afro Pop

Davido - Aye
Mafikizolo Ft May D - Happiness
Diamond - Number One
Flavour - Ada Ada
Iyanya - Jombolo

Most Gifted Kwaito

Uhuru Ft Oskido & Professor - Y-Tjukutja
Character Ft Mono T & Oskido - Inxeba Lendoda
Big Nuz Ft Khaya Mthethwa - Incwadi Yothando
Dj Vetkuk Vs Mahoota - Khaba Lenja
Dj Cndo - Yamnandi Into

Most Gifted R&B

2face Ft T-Pain - Rainbow
Jimmy Nevis Ft Kwesta - Balloon
Gb Collective Ft Brian Temba & Reason - Chocolate Vanilla
Donald - Crazy But Amazing
Niyola - Toh Bad

Most Gifted Hip Hop

Cassper Nyovest - Doc Shebeleza
Khuli Chana Ft Da L.E.S & Magesh - Hape Le Hape 2.1
Phyno - Alobam
K.O. Ft Kid X - Caracara
AKA - Congratulate

Most Gifted Southern

Dj Clock Ft Beatenberg - Pluto (I Remember)
Cassper Nyovest - Doc Shebeleza
A.K.A. - Congratulate
Zeus - Psych
K.O. Ft Kid X - Caracara

Most Gifted West

R2bees Ft Wizkid - Slow Down
Davido - Aye
Burna Boy Ft D’banj - Won Da Mo
Olamide - Turn Up
Dr Sid Ft Don Jazzy - Surulere

Most Gifted East

Sauti Sol - Nshike
Diamond - Number One
Navio - No Holding Back
Eddy Kenzo - Sitya Loss
Elani - Kookoo

Most Gifted Video of the Year

Emmy Gee Ft Ab Crazy & Dj Dimplez - Rands And Nairas
Davido - Aye
K.O. Ft Kid X - Caracara
Burna Boy - Run My Race
Tiwa Savage Ft Don Jazzy - Eminado
Dr Sid Ft Don Jazzy - Surulere
Riky Rick Ft Okmalumkoolkat - Amantombazane
Cassper Nyovest - Doc Shebeleza
Sarkodie - Illuminati
Dj Clock Ft Beatenberg - Pluto (I Remember)
AKA - Congratulate
Diamond - Number One

Special Recognition Award

Boom Shaka
 Photo: Kiukweli, haikuwa rahisi kabisa.. lakini kwa uwezo wa Mwenyez Mungu na support kubwa mliyonipa iliwezesha Bongo Flavour yetu kuandika Historia mpya kwenye Ramani ya mziki wa Africa...Hii inaonyesha ni jinsi gani Umoja ni nguvu na pia jins gani mziki wetu ukisupportiwa na kupewa kipaumbele unaweza kufika mbali zaidi... Shukran sana kwa @channeloafrica @channelotv kwa kuniona na kuthamini kipaji changu, My Family, Management, Media zote zilizokuwa zikinisupport, Watangazaji, Wasanii, Wadau na bila kuwasahau wapendwa wangu  #TeamWasafi #TeamChibu #TeamPlatnumz #TeaMMondi toka instagram, Facebook, Whatsapp, Twitter na kadharika, wakiongozwa na kamanda langu @kifesi ... Nawashkuruni sana sana 󾍄󾰟...najua nikiwatag mimi wenda nikasahau mmoja, tafadhali naomba nisaidieni kuwatag hapa waweze kuona shukran zangu kwao....

Wimbo mpya wa Kala Jeremiah

Author
Wimbo mpya wa Kala Jeremiah ft Nuruwell - Usikate tamaa

Download Kala Jeremiah Fa Ft. Nuruwell - Usikate Tamaa - Arusha Yetu

Jose Chameleone sina mpango wa kufanya ngoma na Diamond Platnumz

Author
Msanii Jose Chameleone wa Uganda amekanusha habari zilizoandikwa mitandaoni kuwa amemuomba Diamond Platnumz kufanya collabo

" Siko katika level ya kuomba collabo kihivyo, sio kwamba sina heshima yake (Diamond) ila hiyo sio sahihi na haiwezi kuwa hivyo. Nimekuwa nikifanya muziki kwa miaka 14 na mimi sio msanii mchanga wa kuhangaikia collabo" amesema Jose Chameleon