NIFANYE NA MIMI KAKA DICK -01

Author

 CHOMBEZO LA KUSISIMUA: NIFANYE NA MIMI KAKA DICK

IMEANDIKWA NA: JUMA HIZA

SIMU: 0712988278

_______________


SEHEMU YA 01.


Nakumbuka nilikutana naye Game, Mlimani City. Alionekana kuwa msichana mrembo, kuanzia sura pamoja na umbo lake matata. Kwa mara ya kwanza nilipomtazama nilijikuta nikitamani kuwa naye kimapenzi, sijui hata hisia hizo zilitokea wapi?

Akili yangu ikanituma nimfuate na kumueleza kile nilichokuwa nakitamani kwa wakati huo lakini moyo wangu ulisita. Ulinyong’onyea kutokana na aibu iliyonikumba ghafla!

Alionekana kuwa bize akifanya shopping lakini hilo halikunitisha hata kidogo, nilichokifanya ni kuanza kuzihesabu hatua zangu kuelekea pale alipokuwepo huku kimoyomoyo nikijisemea ‘liwalo na liwe’.

“Mambo,” nilimsalimia huku usoni nikilitengeneza tabasamu pana.

“Safi,” alinijibu huku akionekana kuwa bize na shopping yake.

“Unaonekana kuwa bize sana vipi naweza kukusaidia?”

“Hapana ahsante, nashukuru.”

“Ahsante maana yake nini?”

“Yaani namaanisha nashukuru, ahsante kwa msaada wako.”

“Okay! Vipi naweza kukuuliza jina lako?” nilimuuliza huku nikijifanya kama ninayetafuta kitu fulani hivi kwa kuzuga.

“Kwani kuna ulazima wa kulifahamu jina langu kaka?” alinijibu kwa kuniuliza swali lililonifanya nimuone kuwa msichana wa matawi ya juu sana. Alikuwa hapendi mambo kujuana juana sana, kwa kifupi naweza kusema alikuwa ni msichana fulani hivi wa gharama.

“Sio lazima kulifahamu lakini kama hutojali ningependa kulifahamu?”

“Wewe kaka vipi, hivi utafahamu wangapi wanaoingia supermarket hii au wewe ni mwizi nini?” 

“Ndiyo mimi ni mwizi, nataka kuliiba jina lako. Kwani kuna ubaya?” nilimjibu kwa kutania na kumfanya atokwe na kicheko cha bila kukitegemea.

“Wewe kaka umetumwa nini?”

“Ndiyo nimetumwa na moyo wangu nikuulize kuwa unaitwa nani?”

“Sitaki.”

Mpaka kufikia hapo nilikuwa nimeshafahamu kuwa alikuwa ni msichana wa aina gani, alikuwa ni miongoni mwa wale wasichana ambao wanapenda kubembelezwa, yaani wao kila kitu ni kubembelezwa tu. Nililifahamu hilo na sikutaka kulifanyia kazi, niliendelea kumsumbua mpaka pale uvumilivu ulipomshinda.

“Haya naitwa Evadia,” alijitambulisha huku akionekana kuchoshwa na usumbufu wangu.

“Nafurahi kukufahamu,” nilimwambia kisha nikampa mkono lakini hakuupokea, aliupuuzia. Hilo halikwa tatizo kabisa, niliendelea na usumbufu wangu kama kawaida.

“Naitwa Dickson lakini wengi wanapenda kuniita  Dick mapenzi,” nilijitambulisha kisha nikaanza kuondoka eneo lile kimitego, kuna kitu nilichokuwa nikikitegemea kwa wakati huo.

Sikumbuki ni nini kilitokea lakini nilishangazwa sana na mshangao uliomkumba Evadia mara baada ya kumtajia jina langu. Alinitazama mara mbilimbili kisha akawa kama mtu ambaye haamini kile alichokuwa akikishuhudia kwa macho yake.

Alilirudia kuliita jina langu halafu akanitazama usoni, safari hii ule ubize aliokuwa nao ulimuisha, akanitazama tena huku akiwa haamini kabisa kukutana na mimi mahali pale.

Labda nikuambie kitu ndugu msomaji, nilikuwa na jina kubwa sana mitandaoni, hakukuwa na mtu ambaye alikuwa ni mtumiaji wa mtandao wa Istagram na Facebook halafu akawa halifahamu jina langu. Wengi walikuwa wakinifahamu kutokana na hadithi zangu aina ya chombezo nilizokuwa nikiziandika katika mitandao hiyo, nilikuwa nikiongoza kuwa na wafuatiliaji wengi (Followers).

“Dick,” aliniita kwa mshango.

“Naam,” nilimuitikia halafu nikamgeukia, akazidi kunishangaa tu.

“Ni wewe kweli?” aliniuliza.

“Yeah! ndiyo mimi,” nilimjibu huku nikimrudia, safari hii nilijifanya kubadilika kidogo, sikutaka anielewe nilikuwa ni mtu wa aina gani.

“Kwani unanifahamu?” nilimuuliza.

“Ndiyo nafuatilia sana simulizi zako mitandaoni yaani kila siku nilikuwa natamani siku moja nikuone maana sio kwa simulizi zile za mapenzi unazotunga,” aliniambia kisha akaja na kunikumbatia.

“Siamini,” aliniambia wakati huo nilikuwa nimekumbatiana naye.

“Huamini nini?” nilimuuliza.

“Yaani kukutana na wewe kwangu ni bahati kubwa sana.”

“Usijali,” nilimwambia kisha nikajitoa katika kumbato lake.

Evadia hakutaka kuamini kama alikutana na mtu kama mimi ambaye nilikuwa nikisifika sana, wasichana wengi walitamani kuniona lakini lilikuwa ni jambo gumu, hii ilitokana na ubize niliyokuwa nao, nilishindwa kukutana nao kwa wakati.

Niliishia kuzungumza na wasichana hao kwenye simu huku wengine niliishia kuchati nao tu. Kila msichana alikuwa akionekana kunipenda na hilo ndilo lilikuwa kosa kubwa walilolifanya na wote ambao walijilengesha mtegoni sikuweza kuwaacha salama, nilihakikisha nafanya nao mapenzi.

Alichoamua kukifanya Evadia kwa wakati huo ni kuitoa simu yake aina ya I phone 6 yenye  gharama ya zaidi ya shilingi milioni moja kisha akaniomba kupiga selfie na mimi, sikuwa na sababu ya kumkatalia, nilikubali na picha zikaanza kupigwa mahali hapo.

Nilichokuwa nikikiwaza kwa wakati huo ni jinsi gani ningeweza kumpata msichana huyo ambaye alikuwa amenivutia kupita kawaida.

“Unajisikiaje?” nilimuuliza huku nikimtazama, alionekana kuwa mwenye furaha sana.

“Nimefurahi sana Dick yaani sikutegemea kama kuna siku ningekuona,” alinijibu.

“Unaweza kunipa namba yako ya simu?” nilimuliza lakini kabla ya kunijibu nikashangaa akiingiza mkono katika pochi yake ndogo kisha akatoa ‘business card’ halafu akanipa.

“Utanitafuta,” aliniambia.

“Muda gani nikutafute?” nilimuuliza.

“Muda wowote kuwa huru Dick,” aliniambia.

“Ahsante sana,” nilimjibu.

Sikutaka kupoteza muda, nilimuaga kisha nikataka kuondoka mahali hapo.

 “Kwani unaenda wapi?” aliniuliza.

“Kuna sehemu nataka kwenda,” nilimjibu.

“Kwahiyo umeghairi kufanya shopping?”

“Hapana nitafanya nikirudi,” nilimjibu kisha nikaanza kuondoka eneo hilo.

Evadia alizidi kunitazama, nililifahamu hilo pale nilipogeuka na kumuangalia, alikuwa akinitazama muda wote. Nilichukua maamuzi ya kuondoka lakini akilini nilikuwa nikiwaza ni njia gani ningeitumia ya  kumpata.

Niliamini kupitia kipaji changu cha kuandika simulizi na machombezo ndicho ambacho kingeweza kunirahisihia kazi yangu hiyo na kuwa nyepesi kabisa.

“Msichana mrembo kama wewe lazima nikumiliki tu,” nilijiambia kisha nikatabasamu.

Nilipotoka nje ya supermarket hiyo eneo la kuegeshea magari, macho yangu yaliendelea kushuhudia wasichana wengi warembo waliyokuwa wakiingia na kutoka ndani ya jengo hilo la Mlimani City.

Macho yangu yalitua kwa msichana mmoja ambaye alikuwa akilielekea gari aina ya Land cruser prado lenye rangi nyeusi. Alikuwa na sura ya mvuto, kiuno kichoingia ndani kama mdudu nyigu. Alitamanisha kupita kawaida.

Nilipomtazama nilikumbwa na mshangao wa ajabu, niliendelea kumtazama mpaka pale alipogundua nilikuwa nikimtazama.

“Wewe kaka vipi?” sauti yake nyororo ndiyo iliyonigutua kutoka katika bumbuwazi zito lililonikumba muda huo.

“Vipi kuhusu nini?” nilimuuliza.

“Mbona unanitumbulia mimacho yako muda wote?” 

“Kwani kuna ubaya nikikutazama?” 

“Hakuna ubaya lakini umezidi kha!” aliniambia kisha akaubetua mdomo wake, alizidi kuonekana kuwa mrembo mno.

“Yaani siamini hata kidogo,” nilimwambia huku macho yangu yakiendelea kutalii vyema kifuani mwake, alikuwa na chuchu zilizosimama dede.

“Huamini nini?” aliniuliza.

“Hivi kumbe Tanzania bado kuna wasichana warembo?” nilimuuliza swali la kizushi lililomfanya anishangae.

“Kwani umesikia hawapo?”

“Nina miaka kama kumi hivi sijawahi kumuona msichana mrembo kama wewe, wote naishia kuwasoma katika simulizi,” nilimuambia maneno yaliyomfanya atokwe na tabasamu lililotengeneza vishimo vidogo mashavuni mwake.

“Halafu kumbe unajua kuficha siri?” nilimuuliza huku nikijifanya kama nimeshtuka kwa kuona kitu ambacho sikukitegemea kwa wakati huo.

“Siri gani tena?” aliniuliza.

“Nimesimama na wewe muda wote huo kwanini hujaniambia kuwa una dimpoz?” nilimuuliza swali lililomfanya acheke.

“Mbona unanicheka sasa?”

“Hapana sikucheki.”

“Ila?”

“Umenifurahisha tu.”

“Halafu hujaniambia kitu?”

“Kitu gani?”

“Jina lako?”

“Oooh! Sorry naitwa Precious.”

“Precious ndiyo jina lako?”

“Ndiyo Precious Kamba.”

“Aliyekupa jina wala hakukosea yaani limefit mahali pake kabisa.”

“Kwanini?”

“Jina zuri halafu na wewe mwenyewe pia ni mzuri.”

“Ahsante na wewe unaitwa nani?”

“Mimi naitwa Akili za wote.”

“Ndiyo jina lako?”

“Ndiyo.”

“Unaishi wapi?”

“Tandale kwa tumbo.”

“Tandale?”

“Ndiyo kwani vipi?”

“Hamna!”

“Sawa haina noma.”

“Haya kwahiyo unaingia au unatoka.”

“Nipo katikati.”

“Niambie bana ili kama ni lift nikupe kama hutojali maana naelekea Magomeni napitia Tandale.”

“Dah! nashukuru Precious umeiokoa nauli yangu ya ngama maani sisi wengine kuja supermarket mpaka pawe na sababu maalum,” nilimwambia Precious kisha akacheka.

Tulipanda kwenye gari na safari ikaanza, barabarani hakukuwa kuna kitu kingine nilichokiwaza zaidi ya mapenzi, yaani kwa muda mfupi niliyomuona msichana huyo nilitamani kuwa naye kimapenzi na siku hiyo hiyo pia nilipanga kumlaghai mpaka akubali nimpeleke nyumbani kwangu japokuwa alionekana kuwa mwenye haraka mno.

_________________


HUU NI MWANZO TU. 


Wewe unayesoma kimyakimya hau-Like, ku-Share wala kuComment chochote ndiye unaweza kunifanya niache kuipost simulizi hii hapa niendelee kwenye WhatsApp tu. Nipe ushirikiano nijue uwepo wako humu. FANANI BILA HADHIRA haina maana.😎


Unajua nini kilitokea?

Hebu bashiri, niambie unahisi nini kitatokea?


SHARE KWA MARAFIKI ZAKO ILI TUZIDI KUSONGA MBELE.

0 comments:

Post a Comment