Wakizungumza kwa nyakati tofauti
jana, Ofisa mtendaji mkuu wa Rita, Phillip Saliboko na Meneja masoko na
mawasiliano, Josephat Kimaro walisema upekuzi wa nyaraka zilizotumiwa na
Sitti uliofanywa na wanasheria wao, tayari umekamilika.
“Kazi yetu (Rita) tumeimaliza na upekuzi wa
taarifa za Sitti umekamilika na kinachofuata sasa ni kupeleka nyaraka
hizo kwenye mamlaka inayohusika ambayo ni polisi, wao ndio wataamua nini
cha kufanya,” alisema Kimaro.
Alisema Rita haiwezi kumhukumu moja kwa moja
mrembo huyo kuwa alighushi nyaraka na kudanganya ili apate cheti hicho
cha kuzaliwa kilichotolewa na Rita Septemba na badala yake wanapeleka
vielelezo walivyonavyo polisi ili nao wavifanyie kazi.
“Sisi (Rita) jukumu letu lilikuwa ni upekuzi wa
nyaraka, kazi ambayo imefanywa kwa ustadi mkubwa na jopo la wanasheria
wetu na hadi sasa imekamilika na kinachofuata ni kuzipeleka nyaraka hizo
polisi ambao wao ndiyo wenye jukumu la uchunguzi na kumchukulia hatua
Sitti au la,” alisema.
Wakati huohuo, Saliboko akieleza kuwa bado wana
changamoto ya baadhi ya watu kudanganya taarifa zao ili wapate vyeti vya
kuzaliwa na kusisitiza kuwa wanaandaa mfumo maalumu ili kukomesha
udanganyifu huo.
“Tukibaini mtu ametumia udanganyifu ili kupata
cheti, kwanza huwa tunamfutia cheti chake na taratibu nyingine za
kisheria zinafuata. Tunafanya hivyo kwa watu wote wanaokuja kuomba vyeti
kwetu na siyo kwa Miss Tanzania peke yake japo hili la Sitti tunaiachia
mamlaka husika ifanye kazi yake,” alisema.
Sitti Mtemvu aliingia kwenye kashfa ya kudanganya
umri wake na nyaraka zake mbalimbali zilionyesha alizaliwa 1989, umri
ambao umepitiliza ule unaotakiwa kwa mshiriki wa mashindano ya Miss
Tanzania, huku cheti chake kikionyesha alizaliwa 1991, hivyo kulazimika
kuvua taji






0 comments:
Post a Comment