Kila mtu anahusudu mambo ya mwingine na
angependa kuwa kama huyo mtu anayemuhusudu. Suala hilo pia liko kwenye
sekta ya burudani ambako katika hali ya kawaida wasanii ndiyo hupenda
kufanya mambo mapya na hufurahia kuona watu wengine wakiwaida. Hata
hivyo, si kwa Beyonce, mwimbaji na mwandishi nyota wa muziki wa
Marekani, ambaye aliweka bayana jinsi anavyomuhudu Jenniffer Lopez,
maarufu kama J.Lo, ambaye ni mcheza sinema, dansa, mtayarishaji muziki,
mbunifu wa mavazi na mwimbaji.
Katika mahojiano na
jarida la Espanyol, Beyonce alitoa mwangaza kidogo wa mtu anayemvutia
kiasi cha kupenda mafanikio yake. “Bila shaka ni Jennifer Lopez,”
alisema Beyonce alipoulizwa na jarida hilo ni mtu gani anamuhusudu
maishani mwake. “Napenda historia yake ya jinsi alivyokua akiwa Bronx na
mafanikio aliyopata na himaya aliyojijengea. Ni mwanamke mwenye akili.
Nilipata nafasi ya kufanya naye kazi wakati wa kutengeneza tangazo la
Pepsi. Ana uzuri usiofikirika na mwenye talanta.” Ingawa Beyonce alikuwa
muwazi kusema hayo, imekuwa ni dhahiri anapata wapi staili zake za nguo
na urembo. Kama kuiga ni aina ya kuonyesha kuhusudu, basi J-Lo atakuwa
akifurahia kuona anaigwa na Beyonce. Beyonce ameshaonekana hadharani
mara 23 akiwa amevalia nguo alizoiga kwa J.Lo.
Katika
picha hizi, Beyonce anaonekana kwenye picha zilizo kulia akiwa amevalia
vazi linalofanana na la J. Lo aliye kwenye picha za upande wa kulia.
0 comments:
Post a Comment