kwa habari za michezo

fahamu ya liyojiri,ratiba na matokeo

kwa miziki

taarifa za miziki,nyimbo mpya na mengineo

dunia yetu leo

fahamu ya tokeayo duniani.

Showing posts with label Photo. Show all posts
Showing posts with label Photo. Show all posts

WATANGAZAJI WA KIKE WANAVYO IPAMBA AZAM MEDIA

Author
Kila kampuni mpya inapotangaza nafasi za kazi, matarajio ni kuwa wanaume wengi ndio watakaoshinda usaili na kuajiriwa, lakini imani hii imekumbana na changamoto kwenye kampuni mpya ya utangazaji ya Azam Media.
Idadi ya watangazaji wa kike wa televisheni walioajiriwa katika mkakati wa kuiboresha Azam TV inaweza kuwa inakwenda sambamba na ya wanaume.
“Niliataka mabadiliko,” anasema Zainab Chondo (30) baada ya kuulizwa ni kitu gani kilimsukuma kuomba ajira Azam TV. “Kwa sababu nilifanya kazi ITV kwa miaka nane, nikaona ni bora niende sehemu nyingine ambapo nitakutana na changamoto mpya, watu wapya na mazingira mapya ya kazi.
“Kwa hiyo Azam tv ilivyoanza nikasema huku panaweza kunifaa nikatuma maombi yakakubaliwa na sasa nipo hapa. Nafurahi kuwa hapa.”
Chondo ni mmoja tu kati ya watangazaji nyota walioona fursa ya kufanya kazi kwenye kampuni hiyo mpya na wakaamua kupambana bila ya kujali changamoto ya idadi ya wanaume zinapotangazwa nafasi adimu kama hizo.
Orodha hiyo ya watangazaji wa kike waliojiunga na Azam TV pia inamjumuisha Fatma Almasi Nyangasa, Yvonna Kamuntu, Rehema Salum na Jane Shirima ambao wameshatambulishwa na kampuni hiyo na tayari wameanza kuruka hewani kwenye vipindi mbalimbali.
Chondo hakupata nafasi hiyo kwa sababu ya jinsi yake, bali uwezo na uzoefu wake katika tasnia ya habari.
Baada ya kumaliza mwaka mmoja katika shahada ya sanaa na habari nchini Uganda, Chondo alipata nafasi ya kufanya kazi Shirika la Utangazaji la Uganda (UBC), lakini mwaka uliofuata neema ikafunguka zaidi na akaajiriwa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) akiwa mwaka wa tatu chuoni.
“Tangu nikiwa mdogo nilikuwa napenda sana masuala ya habari. Nakumbuka hata nilipokuwa shuleni nilipenda kujishughulisha na mambo ya habari hadi wenzangu wakawa wananiambia nitakuwa mwanahabari mzuri nikiendelea hivyo,”anasema Chondo ambaye aliwahi kuwa kiongozi mkuu wa shule akiwa mwanafunzi wa sekondari.
Akiwa nchini Uganda wakati yupo chuoni anasema alisoma mwaka wa kwanza na aliopoingia mwaka wa pili alipata kazi ya uandishi katika Shirika la Utangazaji Uganda (UBC).
“Baada ya kumaliza mwaka mmoja hapo nikiwa mwaka wa tatu nilipata kazi tena katika Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC-Swahili) kama mwandishi wa habari wa kawaida.
“Kwa hiyo hadi nahitimu nilikuwa nimefanya kazi na UBC na BBC Swahili, jambo ambalo lilinipatia uzoefu mkubwa na wa kutosha kwani nilijifunza mambo mengi sana kutoka kwao,” anasema Chondo ambaye alianza kuhusudu mambo ya utangazaji tangu akiwa mdogo.
Pengine, mtu ambaye ametofautiana nao kidogo ni Fatma Almasi ambaye alisema kuwa hakuwahi kufikiri kwamba siku moja angekuwa mwandishi wa habari na mtangazaji wa televisheni.
“Sikuwa mpenzi wa uandishi wa habari. Nakumbuka wakati namwambia baba yangu nataka kuwa mwandishi wa habari akasema hataki, uandishi wa habari,” anasema Fatma ambaye ni mtoto wa kwanza katika familia yao.
Lakini anasema alifanya bidii kubw akufikia hapo alipo kiasi cha kutafutwa na Azam TV.
“Nilifanya kazi kwa bidii. Nianza kama mwandishi wa mahakamani nikiandika habari za mahakamani. Nakumbuka mkurugenzi wetu wa wakati huo alikuwa na ushirikiano sana kwetu. Alinipa moyo.
“Aliniambia Fatma unaweza, naona jinsi unavyofanya kazi ukiendelea na hizi jitihada utakuwa mwandishi mzuri sana baadaye.”
Hakuna shaka kwamba Nyangasa aliendelea na jitihada hizo na sasa ni mmoja wa watangazaji wazuri nchini.

KUMBE BEYONCE ANAMUINGA J.LO

Author
Kila mtu anahusudu mambo ya mwingine na angependa kuwa kama huyo mtu anayemuhusudu. Suala hilo pia liko kwenye sekta ya burudani ambako katika hali ya kawaida wasanii ndiyo hupenda kufanya mambo mapya na hufurahia kuona watu wengine wakiwaida. Hata hivyo, si kwa Beyonce, mwimbaji na mwandishi nyota wa muziki wa Marekani, ambaye aliweka bayana jinsi anavyomuhudu Jenniffer Lopez, maarufu kama J.Lo, ambaye ni mcheza sinema, dansa, mtayarishaji muziki, mbunifu wa mavazi na mwimbaji.
Katika mahojiano na jarida la Espanyol, Beyonce alitoa mwangaza kidogo wa mtu anayemvutia kiasi cha kupenda mafanikio yake. “Bila shaka ni Jennifer Lopez,” alisema Beyonce alipoulizwa na jarida hilo ni mtu gani anamuhusudu maishani mwake. “Napenda historia yake ya jinsi alivyokua akiwa Bronx na mafanikio aliyopata na himaya aliyojijengea. Ni mwanamke mwenye akili. Nilipata nafasi ya kufanya naye kazi wakati wa kutengeneza tangazo la Pepsi. Ana uzuri usiofikirika na mwenye talanta.” Ingawa Beyonce alikuwa muwazi kusema hayo, imekuwa ni dhahiri anapata wapi staili zake za nguo na urembo. Kama kuiga ni aina ya kuonyesha kuhusudu, basi J-Lo atakuwa akifurahia kuona anaigwa na Beyonce. Beyonce ameshaonekana hadharani mara 23 akiwa amevalia nguo alizoiga kwa J.Lo.
Katika picha hizi, Beyonce anaonekana kwenye picha zilizo kulia akiwa amevalia vazi linalofanana na la J. Lo aliye kwenye picha za upande wa kulia.

ratiba ya UEFA baada ya draw

Author

MANCHESTER City imepangwa kuikabili Barcelona katika hatua ya 16 bora ya Ligi ya soka ya Mabingwa Ulaya kwa mwaka wa pili mfululizo. Chelsea itacheza na Paris St-Germain, na Arsenal imepangwa dhidi ya Monaco katika mapambano hayo yatakayochezwa Februari na Machi mwakani.
Mabingwa watetezi, Real Madrid wataikabili Schalke 04, huku timu iliyopoteza fainali ya msimu uliopita, Atletico Madrid ikikabiliana na Bayer Leverkusen.
Bayern Munich itacheza na Shakhtar Donetsk, Juventus itaivaa Borussia Dortmund na Basel imepangwa na Porto. Mechi za kwanza zimepangwa kufanyika kati ya Februari 17, 18, 24 na 25 na marudiano ni Machi 10, 11, 17 na 18.
Manchester City ilifuzu kwa bahati, ikihitaji ushindi katika mechi ya mwisho dhidi ya AS Roma kufuzu, lakini ilimaliza ikiwa nyuma ya Bayern Munich hivyo kuwa na maana kwamba itapangiwa miamba ya Ulaya kama vile mabingwa mara nne, Barcelona ya Hispania. Katika mtoano msimu uliopita, timu ya Catalunya ilishinda kwa jumla ya mabao 4-1.
Chelsea iliyomaliza mshindi wa kundi mbele ya Schalke 04 ya Ujerumani, imepangwa kuikabili Paris St-Germain kwa mwaka wa pili mfululizo, baada ya kuwatoa mabingwa hao wa Ufaransa kwa bao la dakika za mwisho katika robo fainali mwaka jana.
Kuna utamu zaidi katika pam-bano hilo kwani Chelsea imemuuza beki wake, David Luiz kwa PSG kwa ada inayoaminika kuwa pauni milioni 40 msimu huu. Arsenal iliyomaliza nyuma ya Borussia Dortmund katika kundi lao, imepangwa dhidi ya timu iliyowahi kufundishwa na kocha Arsene Wenger kuanzia mwaka 1987 hadi 1994.
Monaco ilifunga mabao manne tu katika kundi lake, lakini ilimaliza ikiwa kileleni. Mkurugenzi wa Soka wa Manchester City na mchezaji wa zamani wa Barcelona, Txiki Begiristain aliiambia Sky Sports News: “Kila pambano katika ratiba hii linafanana. Ni la kuvutia, kwa hiyo tunajiandaa kwa hilo.
“Tunajiamini sana kwa jinsi tulivyofuzu kwa kuishinda Bayern Munich nyumbani na Roma ugenini, kwa hiyo wachezaji wanajituma sana kujiweka fiti na kujiamini kwa ajili ya mechi hizo.
“Tumeimarisha kikosi chetu kuanzia msimu uliopita na tunao wachezaji mahiri mbele.” Katibu Mkuu wa Klabu ya Arsenal, David Miles alisema: “Wakati ratiba ikiendelea kupangwa, timu nyingi kubwa zilikwishatoka.
Tuna furaha kupangwa hapo. “Tunajiandaa kwa hamu kubwa kwa mechi hizo. Tumepangwa na baadhi ya timu kubwa Ulaya kwa miaka kadhaa iliyopita, lakini hatutadharau. Monaco imejipatia haki ya kuwa katika hatua hii.
“Mashabiki wana matarajio makubwa, na itakuwa jambo zuri kuvuka hatua ya 16 na kuendelea kutoka hapo.” Katibu Mkuu wa Chelsea, David Barnard alisema: “PSG inafahamika kwetu kwani tumecheza nao katika robo fainali mwaka jana na wanaye David Luiz ambaye naye anacheza kwao. “Ni ratiba nzuri pia kwa mashabiki wetu.
Timu zote mbili zina vikosi tofauti na vile vya mwaka jana, kwa hiyo kama ingekuwa PSG au mwingine yeyote, ingekuwa hali ile ile.” Aidha, katika Kombe la Europa hatua ya 32 bora, Tottenham imepangwa kuikabili Fiorentina, Everton dhidi ya Young Boys, Celtic itacheza na Inter Milan wakati Liverpool iliyotolewa katika Ligi ya Mabingwa, itacheza na Besiktas.
Mabingwa watetezi wa kombe hilo, Sevilla ya Hispania imepangwa na Borussia Monchengladbach. Ratiba kamili ya timu za hatua ya 16 bora Ulaya ni: Paris St-Germain v Chelsea Manchester City v Barcelona Bayer Leverkusen v Atletico Madrid Juventus v Borussia Dortmund Schalke 04 v Real Madrid Shakhtar Donetsk v Bayern Munich Arsenal v Monaco Basel v Porto

neno moja kwake

Author

HUYU NDIYE MLIMBWENDE WETU

Author