HATUKUPENDA TUWE HIVI-22

Author

HADITHI,
HATUJAPENDA TUWE HIVI,
SEHEMU YA ISHIRINI NA MBILI (22)
MTUNZI Deo Young Massawe,
MAWASILIANO, 0769297430.
                       Sehemu ya 22.
Usiku wa jumanne Miriam alitembelewa na dada  mmoja,
"Miriam mambo"
"safi dada mzima wewe?
" mimi mzima kabisa,nimeagizwa hapa kwako kuna ujumbe  nilete,si unamkumbuka yule mama uliyekua unakaa nae kipindi cha nyuma ?"
"ndio yule mama mbaya sana kwangu siwezi kumsahau,namkumbuka vizuri"
"sasa basi tunavyoongea basi anaumwa sana,amenituma nikutafute akuombe msamaha kwa makosa yote aliyowahi kukufanyia,hivyo basi kesho anaomba ukamtembelee  hapo St Thomas"
"jaman poleni anaumwa wapi?"
"yule alikua mwathirika na saivi kazidiwa sana sijui kama atapona,hivyo anakuhitaji kesho,tena asubuhi ikibidi"
"sawa basi asubuhi unipitie hapa,tuelekee kazini kwangu niombe ruhusa ndo tuende"
"sawa usiku mwema jaman ulale unono".
     Miriam aliskia uchungu kwa taarifa hiyo kua mama mlezi wake anaumwa sana,hapo aliinamisha kichwa na kukumbuka baadhi ya vitu alivyowahi kumfanyia vya kikatili,
" yaani siku ile alingiza kidole kwenye uchi wangu ina maana alijua sitaumia,? na je siku alitaka kuniuza ili nikafanye ngono alifkiri jaman mimi  nimeshindwa kujiuza mwenyewe? ona sasa yeye kajiuza lakini hatua ya mwisho ndo hii kaathirika" Miriam aliwaza hayo kisha machozi yakaanza kumtoka.
"Sasa sijui nianzie wapi maana kuna Jesophat na huyu mama tena, ila nitaanza kwa huyu mama alafu nimalizie kwa Jesophat" Miriam alijipanga ratiba ya kesho yake kisha kuanza kuandaa vinywaji vya matunda.
Mwendo wa saa tatu Miriam alikamilisha kazi yake ya kusaga matunda,alihifadhi sehemu nzuri, akala na kusali kisha akalala.
                               ********
Jumatano asubuhi taarifa za kifo cha Josephat zilianza kuenea mtaani kwao,
"hapo itakua kuna mkono wa mtu  maana niliskia kapata nafuu sasa itakuaje tena afe" ni maneno ya watu waliosema mtaani kwani hakuna mtu  aliyembiwa kafa kwa sumu,hiyo ilikua siri ili uchunguzi ufanyike, hivyo kila mtu  alijua ni ile ajali imemuua.
  Nae Miriam aliamka asubuhi na mapema ila yeye hakua na taarifa yoyote na alipanga ratiba yake mchana ataenda kumtembelea Josephat hospital,
"ahaa  Miriam kumbe ushsjiandaa tayari, ama kweli unazingatia mda" yule dada  wakuelekezana nae kwenda St Thomas alifika na kumkuta tayari Miriam anamsubiri nje,walianza safari kwanza kuelekea kazini kwa Miriam kuchukua ruhusa.
  Miriam kila alipoomba ruhusa alipewa bila pingamizi kwani alikua mfanyakazi mzuri aliyependwa na kila mtu  kwa ukarimu wake wa kujitoa kwa watu,yaani hakufurahi kumuona mtu  analia njaa ingali yeye ameshiba,lazima angempa chakula,hapo alipata umaarufu kwa moyo wa utoaji.
                             ********
Kabla taarifa za kifo cha Jesophat kufika shuleni tayari askari polisi walikua shuleni hapo,
"samahani mwalimu tunawaomba wanafunzi wa nne waliotoka hapa jana  na kuenda kumsalimia mwenzao anaeunwa hapo Mount Meru" alisema askari mmoja alievalia kiraia,
"nini kwani wamefanyaje na wewe ni nani " mwalimu aliuliza kwa mshangao,
"mimi ni askari kuna uchunguzi tunafanya  hivyo nawaomba" askari huyo alijibu huku akimuonesha mwalimu kitambulisho cha kazi,
"ahaa sawa,ngoja niwaite" mwalimu alijibu na kunyanyuka kuelekea darasa alilokuepo Genes maana ndie aliefahamika kama kiongozi wa msafara huo,
"we Genes njoo hapa," mwalimu aliita
"naam mwalimu" Genes aliitika huku akinyanyuka haraka na kumfuata mwalimu,
"hebu njoo na kundi lako mlioenda kumtembelea Jesophat jana"
"sawa ngoja niwaite" Genes alijibu na kuelekea madarasa ya kidato cha nne kumchukua  Angel,
"naona zile pesa tulizopunja jana  ndo kimesanuka leo" Genes aliwaza kabla hawajajua kua wanitwa na maskari.
"Hebu wewe njoo hapa" askari mmoja alisema huku akimnyooshea Genes kidole,Genes aliinuka na kumfuata huyo askari kwani mda huo walishajua wanaongea na maaskari,
"hebu eleza jinsi mlivyotoka hapa jana  hadi wakati mnafika hospital na jinsi mlivyomuona mgonjwa na hadi kurudi hapa shuleni" aliuliza askari huyo alieshika karatasi na kalamu, huku akina Angel wakiwa kama umbali wa mita kumi hivyo hawakusikia kinachoongelawa.
Genes alitoa maelezo jinsi walivyoondoka na jinsi walivyonpitia Miriam na walivyopitia kibandani  kununua matunda ila hakusema jinsi walivyomuacha Miriam kasimama  mlango wa wodini na kuenda kugawana pesa hapo aliongea uongo,
"tulipofika nje ya wodi,huyo mwezetu alitangulia kuingia na sisi tukabaki nje,na kwabahati mbaya mlinzi akatuzuia kuingia,hivyo tulibaki nje na badae tuliporuhusiwa kuingia nae huyo mwezetu alitoka" Genes alieleza hayo yote na mengine yaliyotokea,
"Ahaa sawa" alisema askari na kumuamuru kukaa sehemu tofauti na wenzake,
"Njoo wewe" askari alitamka  huku akimnyooshea  Angel kidole ishara ya kumuita,
"hebu nielezee jinsi mlivyotoka hapa kwenda kumtembelea huyu mwanafunzi mwenzenu hadi kurudi" askari huyo alimuuliza huku akikaa  tayari kuanza kuandika,
Angel aliwaza kwa sekunde kumi, bila kusema kitu,
"sasa hapa nitasemaje,niseme ukweli alafu ukute Genes kadanganya,au nidanganye  ukute Genes kasema ukweli" Angel aliwaza
"eleza basi dada"askari aliongea kwa kuamrisha ,ila angel aliwaza na kuamua kuutumia uzuri wake kumchanganya yule askari  hapo akaanza kutabasamu na kulegeza macho na kusimama upande kidogo, askari yule alianza kuvutiwa jinsi Angel alivyojiweka,Angel aliona sehemu ya suruali iliinuka taratibu na akajua  askari ashapitiwa na hajielewi tena,
"unajua sisi tulitoka hapa tukaeda tukafika na kulikua na msichana fulani hata cjui kwa nini aliandamana na sisi,ndie alianza kuingia na kuwahi kutoka tena alitoka  akiwa na wasiwasi" Angel alipomaliza kuelezea basi askari moja kwa moja aliamini kua muuaji ni Miriam,hivyo hakua na haja ya kuuliza tena wengine,
"hebu naomba namba yako ya simu" huyo askari alimuomba Angel namba na bila ubishi Angel alitoa namba na kuiandika  hapo hapo alipokua  anaandika maelezo yao,hivyo hakuna aliyejua kitu chochote.
Pamoja na kufuatwa hadi shuleni Genes hakuelewa sababu yao kuja kuchunguzwa,ila Angel alijua kila kitu ila hakusema chochote.
"Tunashukuru mwalimu" askari aliaga na kuondoka.
"Ni yule Miriam bhana,unajua hawa wahudumu wa bar wana roho mbaya sana wanakuua huku wakikuchekea" alisema askari mmoja wakiwa njiani kuelekea hotel Aquline kumkamata Miriam.
Baada ya dakika kumi tayari gari ya polisi ilikua kwenye maegesho na askari tayari wameshuka kwenye gari,
"jaman tukae makini maana akikudunga na kitu chenye hiyo sumu basi hufiki hata pharmacy ( duka la dawa)" askari hao walipeana tahadhari kwani tayari washamchukulia Miriam kama muuaji hatari.
"Yupo wapi huyu" askari mmoja aliulizia mapokezi huku akionesha picha ya Miriam, na mapokezi walikutana na Anitha,
"katoka kidogo" Anitha alijibu,
"kaenda wapi muuaji mkubwa huyu" askari aliuliza kwa hasira,
"muuaji??" Anitha aliuliza kwa mshangao,
"wewe tuambie kaenda wapi,utajua ni muuaji au la" askari alisisitiza,
"kaenda hapo hospital ya St Thomas kumwangalia mgonjwa,ila mimi  namjua huyo sio muuaji" Anitha alijibu ila alizid kushangaa kwani askari waliondoka kwa kasi ya ajabu,
"endesha haraka kabla hajamuua mwingine" alisema askari mmoja kwani waliamini basi Miriam huulia watu wodini,gari ilitembea mwendo mkali kuelekea hospital ya St Thomas,kila askari akijihami kudungwa hiyo sumu.
                               **naumia Miriam alilia  sana baada ya kufika St Thomas na kukuta hali ya mama aliyemlea ilivyo mbaya,alikua anaharisha hadi amefungwa nepi kama mtoto,
"mwanangu ulinisaidia sana kwenye kazi zangu,uliniingizia faida kubwa sana ila nina  uchungu  kwasababu nilikudhulumu mshahara wako,mbaya zaidi natumia sana kwa kuwa nilitaka kukufanyia biashara ambapo kama ningefanikiwa kukufanyia biashara basi ungekuta umethirika kama mimi, mwanangu naomba unisamehe sana,mimi  sina cha kukulipa zaidi ya mungu ndie muweza wa yote atakulipa,kingine mwanangu naomba usiwe na tabia ya uasherati naomba ufanye kazi kwa bidii na kama ni hisia za mwili basi utafute mume maana ukahaba sio mzuri,ona  navyoteseka yote ni kwa sababu ya ukahaba,fanya kazi kwa bidii mwanangu usimtegemee mwanaume" baada ya kuongea hayo mama huyo aligeuza macho na kukata roho,Miriam hakuamini kilichotoea mbele yake,
"mama usife,mama usife jaman,mama usife" Miriam alilia kwa uchungu huku akiinama na kujaribu kumuamsha lakini hakuamka,madaktari walikuja na kitambaa kwa ajili ya mtu  aliyeaga dunia.
"huyo huyo,chini ya ulinzi haraka nyoosha mikono  juu" ilikua sauti ya maskari polisi walioingia hospitalin  hapo na kinyooka moja kwa moja hadi kitanda  alichokuepo Miriam,
"ameshammaliza tena huyu mama wawatu" askari mmoja alisema baada ya kumuona mama aliyekua kitandani hapo amekufa.Kila mtu wodini pale alishangaa kwani Miriam alikua kashafungwa pingu....

Itaendelea.

0 comments:

Post a Comment