HADITHI,
HATUJAPENDA TUWE HIVI,
SEHEMU YA ISHIRINI NA TATU, (23),
MTUNZI Deo Young Massawe,
MAWASILIANO, 0769297430.
Sehemu ya 23
Taarifa za kifo cha Josephat zilizidi kuenea mtaani,
"alipata ajali ila naskia kuna msichana mwingine aliekuja kumlisha sumu"
"ha jaman binadamu hatuna huruma tena tumekua wanyama,wamuue na huyo aliyemlisha sumu basi"
yalikua maneno ya watu kila mtaa wakielezea kifo cha Jesophat, waandishimkaniueari wa baadhi ya vituo vya radio basi walifika nyumbani kwa Jesophat ili kupata habari,
"hapa unaongeoa na mwandishi wa Arusha one fm,naskia wewe ndo mama mtoto,kwanza pole sana kwa yaliyokukuta,hebu tueleze kidogo ilikuaje na je mhalifu mmeshamkamata?"
"jaman kaka yangu sijui nikuelezeje,mimi niko na mwanangu namuuguza,wanakuja watu kumjulia hali jaman wanampa sumu bila huruma,na huwezi amini huyo alomlisha sumu ndie alionesha sana masikitiko,hadi alinipa elfu hamsini ya pole,kumbe alitoa rambirambi jaman binadamu sio wema,naskia amekamatwa saiv tena amekatwa akiwa na mgonjwa mwingine huko St Thomas, saivi napigiwa simu kua huyo mgonjwa aliyetembelewa nae ndo akakata roho ndo anafanyiwa uchunguzi kama nae kalishwa sumu hii aliyolishwa mwanangu" mama josephat alitoa maelezo huku akibubujikwa na machozi ya uchungu,
"kwa hiyo mhalifu ameshakamatwa?" mwandishi aliuliza kwa mshangao,
"ndio kakamatwa mida hii,tena wanahisi kuna tukio lingine kafanya huko,maana kaenda tembelea mgonjwa mwingine akafa jaman ni shetani kabisa huyo" mama Josephat alishindwa kuongea zaidi ya hapo,
"haya mama pole sana" mwandishi alimaliza na kuanza safari ya kuelekea St Thomas hospital ili kuchukua matukio zaidi.
*******
"Wewe mtoto una baba na mama hapa mjini?"askari mmoja alimuuliza Miriam wakiwa kwenye gari chini ya ulinzi mkali,huku mwili wa mama mlezi wake ukifanyiwa uchunguzi,
"sina hata naishi mwenyewe, najitafutia maisha" Miriam alijibu bila wasiwasi,
"unajitafutia maisha yapi kwa kufanya mauaji ya watu, au ukiua unalipwa ?"
"mimi sio muuaji hata kidogo na kama mnaniona ni muuaji basi nipelekeni na mimi mkaniue basi," Miriam alijibu kwa hasira kwani aliona kama ana mkosi katika maisha yake,
"yaani wewe siku ya ajali ulitoka na huyu mtu wapi,?"askari alimuuliza Miriam,ila Miriam hakujibu kitu kwani aliona akitoa maelezo yoyote basi Genes atahusika hivyo aliamua kubeba msalaba wake mwenyewe,
"yaani kama nikisema ile jumapili kua tulikutana na akina Genes na Angel basi wataitwa na sio vizur niwahusishe kwenye hili sakata,acha wanifanye watakacho wenyewe" Miriam alijisemea moyoni kwa hasira.
*******
Daktari August ambae bado alikua akiishngaa ile sumu Josephat aliyokuja nayo siku ya jumapili kwa kutaka ifanyiwe uchunguzi,
"kalishwa sumu?" daktari August alishangaa sana kupata hiyo habari,
"hapana mimi niliskia kapata ajali bhana na yupo Mount Meru"
"ndio hivo alipata ajali,ila akiwa hospital kalishwa sumu na mtoto fulani wa kike naskia ashakamatwa tayari,tena wanadai ni sumu kali sana"
"basi kuna kitu" daktari August alisema kisha kufunga maabara kwa haraka na kuanza safari ya kuelekea Mount Meru,huku akibeba sindano ambayo Josephat alifika nayo maabara kwake kabla ya kupata ajali,
"mbona alinambia ameviokota shuleni? basi kifo chake ni mwanafunzi wa huko shuleni kwake kasababisha"alijisemea akiwa njiani.
Katika hospital ambazo daktari August alikubalika kwa umahiri wake kazini ni Mount Meru, kwani kabla ya kuamua kufungua maabara yake basi alihudumia pale Mount Meru kwa mda mrefu,alipendwa na wafanyakazi wenzake hata wagonjwa walivutiwa na huduma kutoka kwake,alikua habagui pia alikua daktari asiependa hongo,
"habari ya kazi daktari"
"nzuri daktari mwenzangu"
"sasa hapa nifanye kwanza kilichonileta,naskia kuna kijana mmoja anaitwa Josephat amezusha hali ya kusikitisha hapa hospitalini kwenu"
"ndio mkuu,hapa bwana wamekuja wenzake kumtembelea kumbe wauaji kabisa wamelisha sumu,ila naskia mhalifu kashakamatwa huko St Thomas yani katupagawisha kweli maana alitaka kutushushia heshima kazini tuonekanae sisi wauaji",
"Ila sasa daktari mimi nimekuja na jipya maana niliposkia hii taarifa nimepatwa na mshtuko maana siku huyo kijana alipata ajali alikua katoka maabara kwangu,na alinishangaza sana kwani alikuja na sindano na wembe, na Mimi nilivyovifanyia majaribio nikakuta vina sumu kali sana pia akanambia ameviokota shuleni,baada ya yeye kuona jinsi nilivyomchoma panya hiyo sindano na panya kufa pale pale basi huyo kijana alitoka kwa haraka huku akiongea maneno ambayo sikuyaelewa, sasa maana huyu mtoto ni jirani yangu nashindwa kujua ni kitu gani kimesababisha kifo chake" daktari August alitoa maelezo hayo,na kuonesha hiyo sindano na wembe kisha waliingia maabara na kuvifanyia uchunguzi,
"kweli ni sumu hiyo hiyo" daktari wa Mount Meru alisema baada ya kufananisha majibu ya uchunguzi wa mwili wa Josephat,uliokua chumba cha kuhifadhia maiti.
*******
Baada ya dakika kumi na tano uchunguzi ulimalizika juu ya mwili wa mama mlezi wa Miriam,
"huyu Israel kachukua roho yake" daktari alitoa majibu baada ya kuthibitisha mwili wa huyo mama hauna tatizo lingine zaidi ya virusi vilivyomuua.
Waandishi wa habari walizidi kuchukua matukio na kumpiga Miriam picha akiwa katika gari ya polisi, hadi taarifa zikafika kazini kwake,Anitha hakuamini kile kilichokua kikiendelea kwani alianza kumlaumu Miriam kwa kupenda,
"namwambia aachane na haya mambo ya mapemzi ila hata haniskii sasa anataka nini huyu mtoto jaman ona sasa jina lake linavyochafu kuitwa muuaji,na mimi navomjua Miriam sio mtu wa kuua mtu" Anitha alijisemea moyoni.
Kila kona habari zilienea na hatimae zilifika hadi shule ya sekondari ya Arusha (Arusha sec) kwani katika mfululizo wa habari hadi akina Genes walitajwa kama watu waliomtembelea marehemu mara ya mwisho,na walioandamana na mhalifu,
"haa! kumbe huyu mwanamke ni katili hivi, tena muuaji kabisa,auawe na yeye,ndo maana nasema hawa wanawake wote wanaofanya kazi katika mahotel ni wahuni wote" Genes alijisemea moyoni huku akimuita Angel,
"kumbe ndo maana tukaja kuchunguzwa na askari"
"aise yule mwanamke nyoka" Angel alijibu.
********
Daktari August alijua kuna kitu kimefanyika tu kwani kutokana na utaalamu wake katika kazi na umekini wake achilia mbali uelewa wa kufananisha matukio alijua kuna kitu tofauti na hicho kinachoendelea yaani aliamini huyo aliyekamatwa atakua hahusiki.
"sio huyo mwanamke aliyekamatwa twende tukamuokoe kwanza tuchunguze vizuri" daktari August alimsihi mwenzake wachunguze hicho kitu kwani inaelekea kuna siri kubwa ndani ya hayo mauaji,
"angalia na maelezo aliyoacha maana nimwyapiga picha" daktari wa muhimbili alionesha maelezo hayo yaliyohifadhiwa katika picha kwani karatasi ishakabidhiwa kwa askari,
"mimi sijaamini haya,maana huyu Jesophat ni jirani yangu na jumapili kabla ya kupata ajali alikuja na vifaa vyenye sumu ofisini kwangu nimsaidie kuvipima,hivyo kuna kitu hapa,naomba tukalifuatilie hili jambo kwa umakini zaidi watu wasije kuuawa zaidi.
Mzee Massawe ambae ndio mmiliki wa Aquline hotel,sehemu ya Miriam ya kazi alipata hizo taarifa kua Miriam kwa wakati huo yupo kituo cha Central,
"sio Miriam huyu wakwangu mfanyakazi nayemuamini mpambanaji kuliko wote,itakua wamekosea naona" Mzee Massawe alijisemea baada ya kusikia taarifa hiyo nae alitoka haraka na kuwasha gari yake kumfuata Miriam kwani alimpenda kama mwanae.
Baada ya mda daktari August nae alisikilizwa na wenzake wa Mount Meru wakaamua kuchunguza upya hali iliyotokea,
"sisi tuchunguze kidaktari na polisi wachunguze kipolisi ila huyu mtoto wakike sidhani kama ana kosa,tena inabidi apewe dhamana kwanza.
Baada ya dakika ishirini gari ya madaktari ilifika kituo cha central, ili kuweza kumchunguza Miriam mwenyewe kwa ambao walikua hawamjui,
"haa! hadi mzee Massawe yupo" daktari mmoja aliongea baada ya kumuona mzee Massawe nae akiulizia kuhusu Miriam.
Itaendelea.
0 comments:
Post a Comment