HATUKUPENDA TUWE HIVI-21

Author

HADITHI,
HATUJAPENDA TUWE HIVI,
SEHEMU YA ISHIRINI NA MOJA,(21),
MTUNZI Deo Young Massawe
MAWASILIANO, 0769297430.
                        sehemu ya 21.
Katika siku za furaha basi hiyo siku ya jumamne ndio ilikua siku ya iliyozidi kwa Angel kwani alijipongeza kwa kuua  mtu bila kutumia nguvu,
"yaani nimemuua kama panya" Angel alijisema moyoni.
"Yaani huyu rafiki angu namuombea  mungu apone jaman" Genes alisema kwa sauti hadi Angel akasikia,
"mimi leo usiku kabla ya kulala nitasali kwa ajili yake" Angel nae alidakia huku akionesha uso wa huzuni, lakini moyoni akiwa na furaha tena akitamka,
"tutakutana peponi".
Genes aliripoti ofisini na kueleza walimu  hali ya Jesophat,
"hakuumia sana hivyo atapona siku za karibu" Genes alielezea kwa machungu kwani Jesophat alikua rafiki yake siku nyingi.
   "We Chris mambo ni kwinei nimeua yani hadi nanuonea huruma maana atafia mbele ya mama yake" Angel alikua chooni akiongea na Chris kwa njia ya simu,
"si nakujua wewe hukosei" Chris alijibu huku akitoa pongezi kwake
"ndio hivo nimemaliza kilaini na kesi itamuangukia Miriam maana nimemuuzia msala kwa maandishi" Angel alimjibu na kukata simu.
                                  ********
"Josephat, Josephat,Josephat,Josephat mwanangu,Joseeeeeeeeeeeee, amkaaaaaaa" ilikua sauti ya mama Josephat iliyoshtua watu wote wodini na kila mmoja kuamka na kutaka kujua kimetoea nini.
Mama Jesophat hakuamini kumwona mwanae haongei na tayari ashageuza macho na mwili ushaanza kukauka,
"daktari, mwanangu kafanyaje?" Mama Josephat alimuuliza daktari aliyekua anagawa dawa,na hapo daktari alisogea karibu na kujionea,
"he mama nini tena mbona maajabu kawa mweusi hivo ghafla?" daktari alishtuka sana huku akikimbia na kuita wauguzi wakuu,
"mama usimguse tena sogea pembeni" daktari alimuamrisha mama Jesophat kusogea pembeni ili madaktari wakubwa waje kufanya uchunguzi,
"jaman mwanangu usife,mwanangu usife kwani bado tunakuhitaji,mwanangu naomba usife jaman amka" mama Jesophat aliendelea kulia  huku akirukaruka kwa machungu kwani hakuwahi kuona binadamu aliye hai akiwa katika hali ile.
"mama huyu mtoto wako hajafa usiogope" muuguzi mkuu wa wodi hiyo alimuondoa mama Jesophat woga ingawa ukweli ni kua Josephat alikufa lisaa limoja na nusu lililopita,
"kaa hapa tukamfanyie uchunguzi zaidi" muuguzi huyo alisema huku wakimtuliza mama Josephat kwani walipanga kumpeleka Josephat katika chumba cha kumfanyia uchunguzi,kwani hata wao walishangaa,
"tayari ashaanza kukauka", alisema muuguzi mmoja wakiwa katika chumba cha uchunguzi,
"hebu mfungue kwanza hivo vidonda" alisema mkuu wa uchunguzi na haraka muuguizi mmoja alianza kufungua kitambaa kilichofunika kidonda cha kichwani,
"we kiache endelea na kazi" alisema mkuu wa uchunguzi huku akiinama chini na kuokota kikaratasi kilichodondoka baada ya huyo muuguzi kufungua kitambaa cha kichwani, huyo muuguzi mkuu alikificha mfukoni bila hata kukisoma.
   Baada ya dakika 20 madaktari wote waliofanyia mwili wa Josephat uchunguzi walikua midomo wazi kwani walishindwa nani kampa Josephat sumu kali kiasi hicho,
"ona  utasema  kakaushwa na umeme" daktari mmoja alisema.
Walijadiliana wao kwa wao na kuamua baba Josephat aitwe,
"tumuite baba ndie anaweza pokea  majibu kiume" daktari mmoja alisema kwa kumaanisha kama ukimpa mwanamke majibu kama hayo basi atakumbuka hadi kilio cha wakati anajifungua hivyo atalia sana.
"amepona?" lilikua swali la mama Josephat kwa daktari,
"hajapona ila anaendelea vizuri" daktari alijibu huku akiwa na uso wa furaha uliomuondoa mama Josephat wasiwasi,
"sasa mama cha kufanya tunamtaka baba hapa,kuna mambo tuongee nae" daktari aliongezea, na hapo mama Josephat alinyanyua simu na kumpigia mumewe,
"anaendeaje huyo mwanangu?" baba Josephat alianza kuuliza mara baada ya kupokea simu,
"anaendelea vizuri kabisa ila unahitajika hapa" mama Josephat nae alijibu,
" washaanza sasa, na mimi sina pesa yani hata kidogo,maana wakishaniita ni mambo ya pesa" baba Josephat aliongea kwa kufoka,
"sio unaitiwa pesa babaa wewe njoo hata kama ni pesa ipo" mama Josephat aliongea kwa kujiamini kwani alikua na pesa ya kutosha alizopewa na Miriam pamoja na Genes,
"sawa nakuja saivi mke wangu" alijibu baba Jesophat na simu ikakatwa.
   "yaani hawa wanaume kila wakipigiwa simu wanafikiri ni hela tu" mama Josephat alijisemea huku akikaa kitandani.
                               ********
"ngoja ninunue matunda nikamsagie Josephat juyce" Miriam alisema huku akiingia kwenye kibanda cha kuuza matunda na kumuacha Anitha nje,
"haa! matunda yote hayo" Anitha alimuuliza Miriam kwa mshangao kwani alitoka na matunda mengi sana mchanganyiko,
"nataka niwe namtengenezea juyce kila siku asubuhi"
"sawa ila nawe una huruma sana na moyo wa kijitolea lazima ufanikiwe tu na utaolewa na huyo Genes" Anitha alimwambia Miriam huku wote wakitabasamu.
                               ********
Muuguzi mkuu,aliingia  katika chumba chake na kutoa karatasi aliyoiokota akiamini itakua na ujumbe wowote,baada ya kuinyoosha vizuri hakuamini baada ya kusoma maandishi haya,
NI MIMI MIRIAM NIMESABABISHA KIFO CHA HUYU JESOPHAT, NAOMBA MNIUE NA MIMI LA SIVYO NITAUA BABA NA MAMA YAKE TENA, NAOMBA MKINIKUTA TU MNIUE MAANA MKINICHELEWESHA MTAJIKUTA PABAYA.
Maneno hayo yalimtoa daktari jasho,
"ni Miriam yupi sasa maana huyu tokea aje hapa yupo na mama yake na leo  katembelewa na wanafunzi wenzake" daktari alijiuliza huku akirudisha karatasi mfukoni na kumfuata mama jesophat,
"samahani mama hivi hawa wanafunzi waliomtembelea huyu mtoto wako walijitambulisha?"
"aise kwa kweli hawajajitambulisha ila kuna mmoja aliyeandamana nao ila yeye aliwahi kuingia na pia akawahi kutoka,huyo anaitwa Miriam,tena huyo sio mwanafunzi ila ni rafiki tu na amenambia jumapili kabla ya mwanangu kupata ajali walionana" mama Josephat alitoa maelezo huku akitoa simu yake na kumuonesha picha waliyopiga pamoja,
"kwa hiyo umesema anaitwa Miriam?" daktari aliuliza huku akikaza jicho kwa kutazama picha vizuri.Mama Josephat hakuelewa sababu ya kuulizwa maswali hayo ila alishangaa kumuona daktari akitikisa kichwa kuashiria kukubali  jambo fulani,
  "basi ni yeye tu, kwanini awahi kuingia na kutoka bila hao wenzake na kwanza sio mwanafunzi mwenzake, jamani huyu binti kwa nini anaua  mtu  mgonjwa tena hapa wodini,huyu atakuja kuua  hata madaktari" alisema moyoni muuguzi huyo huku akiomba kurushiwa hiyo picha ya Miriam kupitia WhatsApp.
  "wewe naona mnapeana namba za simu, we mwanamke ushaanza kuleta biashara za umalaya huku" baba Josephat  alifoka kwa kuingia wodini na kumkuta mkewe anampa daktari namba za simu ili waweza kurushiana picha,lengo la  daktari likiwa  ni kupata picha ya Miriam na  kuipeleka kituo cha polisi ili aweze kukamatwa,
"sio umalaya jaman,kua mstarabu basi" mama Jeso alimtuliza mumewe, na mumewe akahakikisha kweli haikua lengo baya kupeana,
"sasa mzee hebu njoo na hapa" daktari alimvuta baba Jose katika chumba alicho mwanae ambae kwa wakati huo ni marehemu, huku mama akizuiwa kufuata,
"huyu mwanao ametutoka na hatuna  jinsi kwani sisi wenyewe tumeshindwa kuelewa  kauwawa kwa sababu gani," daktari alimueleza kila kitu na jinsi sumu aliyopewa inavyofanya kazi haraka, pia mwisho alimuonesha karatasi iliyokutwa katika kitambaa kilichofungia kidonda,
"kweli huyu ndie kamuua mwanangu?"
"baba Jose aliongea huku akibubujikwa na machozi,hadi akataka kuichana karatasi ile ila daktari akamzuia,
"we mwanaume jikaze,cha kufanya amini kwanza mwanao kafa na kwa sababu tayari saivi siku imeenda basi kesho asubuhi lazima tuwakamate wote waliokuja kumuona Jana yaani wale wanafunzi wenzake pamoja na huyu anayejiita Miriam ili tuwachunguze vizuri maana hata wewe na mke wako mmepokea vitisho, na kama huyu mtu anajua kwa sumu hii basi ni mtu  hatari sana.
Mama Jose alishindwa kuvumilia na kujikuta nae anasukuma mlango  wa chumba alichoingia mumewe pamoja na daktari ili kujionea kinachoendelea kwani alihisi kuna taarifa mbaya.

Itaendelea.

0 comments:

Post a Comment