HADITHI,
HATUJAPENDA TUWE HIVI,
SEHEMU YA ISHIRINI (20).
MTUNZI Deo Young Massawe
MAWASILIANO, 0769297430.
sehemu ya 20.
"Samahani mama! mwanano naona kidogo kapata tatizo katika ubongo hivyo usishangae anaweza kuongea kitu usichokielewa" yalikua maneno ya daktari kwa mama Josephat akimtoa hofu juu ya Jesophat aliyekua anatamka vitu bila mpangilio.
******
"Kalazwa wodi ile pale" Genes alitamka huku akinyooshea mkono wodi aliyolazwa Josephat lakini kabla hawajaingia mmojawapo ya mwanafunzi aliyeandamana na Genes basi alitaka kwanza wasimame,
"asa Genes hapa tumekusanya pesa zaidi ya laki mbili ina maana tutazipeleka zote?"
"ndio itabid tuzipekeke zote" Genes alimjibu huyo rafiki ake alietaka wagawe pesa waliyokusanya kama mchango wa kuenda kumuona mgonjwa.
Miriam hakuwa anasikia chochote kwa sababu waliitana pembeni na kumuacha Miriam mlangoni.
Baada ya mabishano ya mda basi Genes hakutaka kuwakwaza wenzake na hapo waliamua kurudi nyuma kidogo ili wapunje kiasi cha pesa ili wagawane japo Genes hakufurahishwa na kitendo hicho.
"Hawa mbona hawaji" Miriam alijiuliza baada ya kusimama zaidi ya dakika mbili pasipo akina Genes kurejea,
"we anti ingia kama unaenda mwona mgonjwa maana zoezi la kuona wagonjwa litasimama mda sio mrefu" ilikua sauti ya mlinzi ikitoa maelezo juu ya utaratibu wa kuwaona wagonjwa,
"ngoja kuna wengine nawasubiri" Miriam alijibu huku akipapasa macho walikoelekea akina Genes,
"we ingia kumuone mgonjwa,wao wakija watasubiri mda mwingine" mlinzi alijibu na Miriam kutowaona akina Genes wakitokea basi aliingia wodini.
"shikamoo mama na pole kwa kumuuguza mwanao"Miriam alikua anamsalimia mama Jesophat aliemtambua kwa sura kwani alifanana sana na Jesophat,
"marahaba mwanangu nishapoa karibu" mama Josephat alijibu huku akimwelekeza Miriam sehemu ya kukaa,
"asante mama, mimi naitwa Miriam nipo na wanafunzi wanaosoma na mwanao Josephat, mimi pia huyu ni rafiki yangu nimesikitika sana siku anapata ajali nilionana nae" Miriam aliongea huku akitokwa na machozi.
Genes alikua kajilaza tu na kufunikwa lakini ghafla alianza kuonge bila kupangilia maneno,
"mama Angel anaua, mwanake ni sumu sitaki aje karibu mama mwanao watamuua nawaona hao na sumu zao hawana nia nzuri mama" Josephat aliongea kwa kukatakata maneno na hatimaye alikaa kimya,
"mama mbona sasa anatamka maneno hayo"Miriam alishtuka sana kusikia maneno ya Jesophat hasa alipotaja jina la Angel,
"huyu tokea jana anaongea utumbo sana ila daktari amenambia ni kawaida kwa mtu kupata ajali na kuongea hivi" mama Josephat alijibu huku akiwa makini kuangalia picha za umbea katika mtandao wa Instagram,
"ila umemsikia maneno anayosema?" Miriam alizid kuuliza,
"wala sijamsikia mimi,maana anavyoongea kila kitu nitasikiliza kipi na kipi niache?" mama Josephat alijibu.
Miriam alikaa na kuwaza mengi kuhusu jina la Angel kutamkwa kama muuaji,
"au kwa sababu nilipigana na huyo Angel juzi" Miriam alijiuliza maswali mengi ila hakupata jibu zaidi ya kuona sababu ya Josephat kusema hayo ni kwa kupigana kwao.
"Atakua alichukia sana kile kitendo cha mimi kupigana na Angel ndo maana anasema Angel ni muuaji" Miriam alijisemea.
Ukweli wa Jesophat kusema vile ni pale aliposkia sauti ya Miriam na hapo akakumbuka alichotaka kuwahi ndo akapata ajali hivyo Miriam pia hakuelewa ukweli wa mambo hayo.
********
"Subirini baada ya lisaa limoja ndio mda wa kuwaona wagonjwa" sauti ya mlinzi ikiwaamrisha akina Genes kusubiri na hiyo ilitokana na wao kuchelewa walipoenda kugawana kiasi cha pesa walizopunja kutoka kwenye fungu alilotumiwa Josephat,
"afadhali huyu Miriam kaanza kuenda kumwona mgonjwa ndo kazi yangu sasa itafanyika bila shida" Angel alijisemea kimoyomoyo.
Walirudi katika viti vya kusubiria wagonjwa ili lisaa litimie. Na hapo Angel alitoka haraka na kuenda chooni kwa lengo la kujisaidia ila haikuwa hivyo kwani alitoa kikaratasi na kalamu na kuandika maneno fulani ambayo alipanga kuyaacha kitandani kwa Josephat bila mtu yeyote kumuona, baada ya kuyaandika vizuri alikunja karatasi na kuiweka mfukoni,kisha kurudi pale walipokua wamekaa kuendelea kupiga hadithi za uongo na kweli kusudi lisaa liishe.
"Baby una furaha leo" Genes alimnong'oneza Angel baada ya Genes kushindwa kuelewa kwanini Angel ana furaha kiasi hicho,
"kweli baby nikiwa nawe najiskia sana furaha,yaani siwezi kununa nikiwa na wewe hata kwenye msiba natabasamu" Angel alijibu kwa furaha na kuzidisha tabasamu,
"sawa mpenzi basi potezea kidogo maana hapa ni kumuona mgonjwa hivyo tabasamu na furaha sio vizuri" Genes alimshauri nae Angel akajitahid kuonesha uso wa huzuni.
********
"mama mda wa kazini kwangu unakaribia maana nimeomba ruhusa tu haraka" Miriam aliongea hayo wakati akimuaga mama Jesophat,
"chukua hii kidogo mama,nitakua nakuja kukusalimia hapa" Miriam aliongea huku akiingiza mkono wake wa kulia kweye sidiria na kutoa noti kadhaa za elfu kumi kumi bila kuzinyoosha akamkabidhi mama Josephat,
"asante mwanangu wewe nenda hawa wanafunzi nahisi wamezuiwa kidogo kwani huu mda sio wa kuona wagonjwa ila wataruhusiwa mda sio mrefu" mama Jesophat aliongea huku akitoa simu yake ambayo aliomba kuchukua picha na Miriam nae Miriam alikubali na wakachukua picha tena sura ya Josephat ikionekana imejilaza kitandani,Miriam kuona jinsi picha ilivyotoka vizuri,
"hebu nipige nikiwa namshika kichwa" Miriam alisema huku akipeleka mkono pale kweye kidonda kilichofungwa kwa kitamba.
Baada ya hapo Miriam alitoka na kukutana na akina Genes mlangoni,
"samahan Genes nakuomba kidogo" Miriam aliongea kwa uso wa huruma akitaka mazungumzo ya pembeni kidogo na bila kubisha Genes alisogea nae pembeni ili kumsikiliza,
"sasa tutaonana lini maana sasa tumepatwa na tatizo kidogo la huyu Jesophat" Miriam alianzisha maongezi,
"ndo ulichoniitia?" Genes alijibu kwa hasira,
"ok babaaa samahani basi,tutaongea siku nyingine" Miriam aliongea kwa huzuni.
"jaman mimi acha nirudi kazini" Miriam aliwaaga akina Angel,
"sawa tutaonana siku nyingine" Angel alijibu kwa mdomo ila moyoni akijisemea,
"nenda kahaba wewe, sikiliza kesa itakatokujia pumbavu wewe".
*********
Genes na kundi lake waliingia wodini kila mmoja akionesha uso wa huzuni,
" mama pole sana"kila mmoja alimtakia mama Josephat neno hilo ila kwa mda huo Josephat alikua katulia tu hakuongea hata yale maneno akiongea bila mpangilio.
Walikaa nae wakimfariji na kumpa matunda na kiasi cha pesa walizokuja nazo kama kuendelea kumuuguza mwanafunzi mwenzao,
"inabidi tuwahi kurudi tuje siku nyingine" Angel alisema,
"sawa wanangu jaman tuombeane uzima" mama Josephat aliongea huku akiwapa mkono wa shukrani, na Genes aliinama na kumshika Josephat sehemu ya kichwani palipofungwa kama ishara ya kumtakia pole na wengine wakafuata kwa kumshika hapo hapo kichwani na hapo Angel aliingiza mkono mfukoni nae pia akamshika hapo tena kwa bahati mbaya au nzuri wakati Angel anamshika kuliingizwa mgonjwa aliekua anapiga makelele sana kiasi kwamba kila mtu aliekua amelala basi aliamka kumtazama na hadi Genes nae alipiga kelele,hivyo hakuna mtu alieshuhudia kitendo Angel alichokifanya pale.
Genes na kundi lake wakatoka nje kila mmoja akiwa na majonzi ya hali ya juu.
Baada ya masaa mawili daktari alikua anapita kugawa dawa kwa wagonjwa,
"sasa huyu daktari atamuamsha tena mwanangu aanze kusumbua tena" mama Josephat alijisemea baada ya kumuona daktari anakaribia kumfikia,kwani tokea akina Genes waondoke yamepita masaa mawili bila Genes kusema wala kujigusa.
"mama muamshe mwanao" muuguzi alisema na haraka mama Josephat alianza kumgusa kwa mbali ili ashtuke.
Itaendelea.....
HATUKUPENDA TUWE HIVI-20
19:39:00
No comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment