HATUKUPENDA TUWE HIVI-19

Author

HADITHI,
HATUJAPENDA TUWE HIVI,
SEHEMU YA KUMI NA TISA,(19)
MTUNZI, Deo Young Massawe
MAWASILIANO 0769297430.
         sehemu ya kumi na tisa  (19).
"Hivi mbona Jackie Chan alilala chini siku ile alipokua anakimbika na kushtukizia gari?"ni wazo lililomjia Josephat kwa haraka aliweza  kulala kifudifudi na gari kumpita ila kwa bahati mbaya kulikua na chuma iliyokwaruza kichwani,
"nakufaaaaaaa" Josephat alitoa sauti kubwa chini ya gari na kukaa kimya akivuja damu kichwani.
Kelele za watu zilifanya magari kusimama na hapo Josephat alizingirwa na kwa sababu ya maaskari  wa barabarani kua karibu basi walifika na kupima ajali ambapo kila mtu alishuhudia kua dereva hakua na makosa,
"kaumia tena mgongoni" askari mmoja alisema baada ya kumgeuza Josephat aliekua kakwaruzwa tena mgongoni na damu ikiendelea kumtoka.
"sogea! sogea! sogea!" ilikua sauti ya mmoja wa wahudumu katika gari la  kubebea wagonjwa (ambulance).
"ni wale wale wa toyo kila siku tunawaambia wapeleke taratibu au" lilikua swali alilouliza daktari katika chumba cha wagonjwa wa ajali katika hospitali  ya Mount Meru, ambacho kilijaa vijana wengi, tena wengine wakiwa wamekatwa miguu wengine mikono na wengine wakipasuka vichwa kwa makosa ya kutozingatia sheria za barabarani kitu kilichowapelekea kupata ajali ovyo,
"hapana huyu kagongwa,alikua anatambea kwa miguu" mhudumu wa gari alijibu huku akitoka maelezo ya askari mfukoni na kumkabidhi.
Josephat alikua kimya, na hata hakua anajitambua kwa wakati huo na haraka baada ya kuanziwa matibabu alilazimika kuongezewa damu.
  "msiogope huyu mgonjwa wenu atapona kwani hakuumia sana" yalikua maneno ya daktari baada ya wazazi wa Josephat kufika pale hospitalini,
"kwanza huyu mtoto wako alitoka wapi we mama" baba Josephat amuuliza mkewe kwa ukali,
"jaman baba Josephat usiseme hivo,maana tayari yashatokea sasa cha kufanya ni kumpambania apone" mama Josephat alijibu huku akiendelea kufuta machozi,
"mimi nakwambia kila siku mtoto akae nyumbani asome huniskii sasa angalia matokeo ya kulea ujinga sasa leo tunaingia gharama"  baba Josephat alizidi kumlalamika mkewe yaani mama Josephat.
Josephat alilazimika kulazwa na mama yake akabaki nae kumuuguza.
                              *********
"Aise Genes jana best ako  kapata ajali mbona hujaenda kumsalimia hapo Mount Meru" yalikua maneno ya Florah ambae alikua jirani yake Josephat,
"ajali gani tena mbona unanitania ? au ndo maana hajaja  shuleni leo?" Genes alijibu kwa mashaka,
"jana alipata ajali ya kugongwa na gari ila hakuumia sana na hospitali wanasema anaendelea vizuri" Florah alijibu kwa masikitiko,
"embu ngoja badae utanambia vizuri" Genes alikatiza mazungumzo kwa kusema kua badae ataongea nae vizuri ili ajue jinsi ajali ilivyotokea.
"alipatia ajali wapi akati asubuhi ndo nimemkuta akiwa na Miriam kule Sakina? au walipigana sana wakaumia alafu anasema ni ajali nini" Genes alijiuliza na kuhisi jana  yake alivyowakimbia kule Sakina yalikuja kutokea makubwa zaidi,
"hebu ngoja mke wangu  Angel aje shule kwanza nimuulize nitajua nini shida,kama jana wamepigana nitajua" Genes alikaa na wasiwasi sana akimsubiri Angel aje shule,
"yaani huyu Miriam sijui kanitokea wapi maana kila siku nikimuona napata mkosi,ama kweli wasichana weusi wanakuaga na mkosi nimeamini" Genes aliwaza.
  "Yaani we Genes kumbe upo hivo, yaani jana  uniache nipigane na hawara wako tu hata kumsaidia jaman,je ningemuua" yalikua maneno ya Angel alipofika mbele ya geti la shule na kumkuta Genes akimsubiri,
"we tulia Angel naskia kuna majanga" Genes aliongea huku akimhamasisha Angel atulie,
"majanga gani ? mimi ningemuua huyu hawara wako na nilijua tu unao wanawake wengi" Angel aliendelea kuongea kwa hasira,
"apana sio kuua kwani mlimfanyaje Josephat mbona naskia kalazwa?" Genes aliuliza akitarajia jibu kua tulimpiga bali alishangaa kumuona Angel alitabasamu,
"mbona unatabasamu Angel au hujaelewa nilichokuambia" Genes aliongea kwa ukali,
"nimekuelewa sana ndo maana nimefurahi" Angel alijibu huku akizidisha tabasamu,
"mbona sikuelewi Angel" Genes alionesha hali ya kutoelewa kwa kugeuzageuza kichwa,
"yeye sialijidai kutuharibia mpango wetu wa kuenda kukutana jamani my love" Angel alibadilika na kuonesha uso wa huzuni,
"nikweli  ila naskia kapata ajali eti kugongwa na gari nimeambiwa ila sina uhakika kama kagongwa kweli au ni nyie mlimpiga jana  baada kuwaacha pale" Genes alipunguza hasira na kuongea kwa upole tena kwa hali ya mahaba,
"kwa hiyo amekufa?" Angel aliuliza,
"hajafa na anaendela vizuri" Genes alijibu,
"yaani yule hata sitaki kumuona kabisa jana katukatisha utamu jamani" Angel aliongea akionesha uso wa huzuni sana,
"sasa itakua kapata ajali wapi,je jana  wewe ulimuacha wapi maana yule mwanamke alietokea pale ananitaka ila mimi  simtaki kweli hivyo nisamehe tutafanya hata wiki ijayo tu mpemzi usijali, sawa eh"Genes aliongea kwa sauti ya kubembeleza,
"kwani kile kidada kinakaa wapi" Angel aliuliza,
"Kipo hapo Aquiline hotel kinafua mashuka ya quest" Genes alijibu kwa kuonesha uso wa madharau makubwa,
"yaani Genes sasa wewe utampendaje yule mwanamke  mweusi kama kima?" Angel aliongea,
"wala hata simpendi ila yeye tu ananishobokea na sina mda nae" Genes alijibu,
Baada ya kuongea mengi kila mmoja alitawanyika kuelekea darasani na hapo ndipo Angel alipopata upenyo wa kuenda chooni na kutoa simu  aliyokua anaificha katikati ya maziwa yake yaliyofichwa ndani ya sidiria ya kubana,
"we Chris yule Josephat naskia yupo hospital jana kapata ajali, sasa sijui itakuaje maana ndie pekee aliyeona ile sindano niliyoipaka sumu ya kumuua  Genes na sasa sijui kama ni kweli kapata ajali au ukute ni ile sindano imemtoboa"
"ngoja nipo darasani,ngoja nitoke niende chooni nikupigie" Chris alimjibu na kuinuka pamoja  Brown kutoka kiti  cha nyuma kabisa ambapo walikaa.
Angel, Chris na Brown walifanya mazungumzo ambayo mwisho waliamua kufanya mpango wa kuenda kumtembelea Josephat hospital,
"tena hapo hospital ndo vizur akifa  maana hawatagundua kirahisi" Angel alisema,
"sasa sisi tukienda kutembelea mgonjwa si shule nzima itashangaa" Brown aliuliza kwani wao machoni walionekana watu wasiokua na huruma na pia hawakua tayari kumjali mtu  mwenye kasoro,
"hiyo niachie mimi, yaani hiki kipindi tutazika wengi, kwanza huyu Josephat afuate Genes mwenyewe kisha tumalizie hiki kimwanamke chake kiitwacho Miriam sijui Miraa" Angel aliongea,
"sasa wewe inabidi leo  uongee na Genes kwanza mpange kesho mchukue ruhusa kwa mwalimu kisha mumtafute huyo Miriam ili achukue kesi" Chris alimpa  Angel akili ya kutumia ili asihisiwe kufanya kitendo hicho.
                             ********
  "Sasa Genes huyu rafiki yako huendi kumsalimia?" Angel alimuuliza Genes wakiwa wamekaa pamoja katika break ya saa nne,
"ndo nawaza hapa ila sinimekuambia sina uhakika sana hadi leo itabidi leo nimpitie Miriam tu nimuulize huenda anajua zaidi ingawa sitaki kuongea nae ila itabidi tu," Genes alijibu,
"powa muone basi alafu kesho tuende nae ikiwezekana ili tukapatane hapo,sio vizuri tugombane" Angel aliongea huku akionesha uso  wa huruma sana.
                              ********
"Dada Anitha yaani naskia kamgongo kanauma" Miriam alikua na Anitha wakitoka kazini,
"si kile kichapo cha jana kweli?" Anitha alimjibu,
"apana sio kichapo! mimi  ndio nilimchapa" Miriam alijibu,
"pole" Anitha alimwambia Miriam,
"sasa dada  we nenda mimi  ngoja nimsubirie yule rafiki wa mume wangu hapa"
"haa  Miriam umeanza sasa unamsubiri tena shemeji au ndo yale ya hainaga ushemela,?"
"apana dada  ndo ananiletea habari za mume wangu na jana nimeachana mchana sasa sijajua kama alifika nyumbani salama" Miriam alijibu na wakaagana Miriam akabaki njiani kumsubiria Jesophat ambae kwa wakati huko hakujua kama yupo hospital.
Baada ya kusubiri kwa nusu saa  alikata tamaa na kuanza kuondoka, ila akageuka mara ya mwisho nakuona mwanafunzi,
"waaooooh, Genes yuleeee" Miriam alianza kurukaruka kwa furaha,na kwa wakati huo Genes bado alikua hajamwona Miriam,
"acha hizo bhna" ilikua sauti ya Genes ikimkataza Miriam kuendelea kupata denda kwani tayari Miriam bila hata kusalimiana alimrukia na kuanza  kumpiga mabusu mbele za watu bila woga.
"Mimi nimeleta habari mbaya"
"zipi hizo?"
"Jesophat naskia alipata ajali na sijaamini",
" dah! sangapi alipata maana nilikua nae jana mchana?"
"hapo hata mimi  sijajua ila kesho tunaeda kumwangalia hapo Mount Meru kwani naskia kalazwa hapo"
"utanipitia basi  na mimi  niende, ila saivi Genes nataka tuende kwangu ukapaone tu tuongee kidogo" Miriam alimuomba Genes kuenda nyumbani pamoja ila Genes aligoma na mwisho walikubaliana kuenda wote hospital kwa ajili ya kuenda kumjulia Jesophat hali.
                             ********
Usiku huo bado Jesophat alikua hajitambui,na alikua bado akiedelea kupata matibabu,
"mama acha kuchati kaa makini na huyo mtoto wako naona anajaribu kunyoosha mkono" yalikua maneno ya daktari kwa mama Jesophat aliekua  anachat na kujisahau kama anamuuguza mgonjwa,kwani mda huo Jesophat alinyoosha mkono kama mtu  aliehitaji msaada,ila alirudisha mkono na kutulia.
Asubuhi na mapema, Angel alichukua sindano yake na kuichovywa kwenye unga wa sumu na kuiweka katikati ya daftari"
"mungu nisaidie" Angel alisema na kutoka nje kuanza safari ya kuenda shule.
Mchana wa siku hiyo walikusanyika wanafunzi watano akiwemo Angel na Genes kuelekea hospital.
"tununue matunda kidogo" Angel alisema na wote waliingia sokoni na kununua matunda.

Itaendelea..

0 comments:

Post a Comment