HATUKUPENDA TUWE HIVI-18

Author

HATUJAPENDA TUWE HIVI,
SEHEMU YA KUMI NA NANE (18),
MTUNZI Deo Young Massawe
MAWASILIANO 0769297430,
      sehemu ya kumi na nane  (18)
"Huyu mwanamke sio mtu  mzuri" Jesophat alijisemea huku bado akiwaza ile sindano na wembe ni vya kazi gani?
"au huyu mtoto ni mshirikina nini?" alijiuliza maswali mengi sana bila kupata jibu,
"ila itajulikana tu nitaanza uchunguzi kesho" alijisemea gari tayaribikiingia kituoni ambapo wangeshuka.
"We mwanamke njoo hapa  nikupe somo" Miriam alimuita Angel alieshuka kwenye gari wakwanza, na bila ubishi Angel alitii amri,
"siku  nyingine ukiwa unaenda mahali kama upo  na mtu  usikubali akae na pesa yote,je  mkipotezana utabaki bila nauli ya kurudi alafu ukikosa mtu wa kukufadhili itakuaje? kuanzia leo  uwe unatembea na pesa kidogo mfukoni,sasa kama saivi huna hata senti mfukoni,chukua hii ikusaidie njiani" Miriam aliongea kwa huruna bila kujali ugomvi walioufanya hapo nyuma,
"Asante sana ubarikiwe" Angel alijibu huku akipokea noti ya  elfu tank kutoka kwa Miriam,
"we hiyo pesa unampa ya nini siunipe mimi?" Jesophat alijisemea moyoni.
  Miriam alikua mtu mwenye uruma na mtoaji kutoka moyoni hakutaka mtu  ateseke mbele ya macho yake kama akiwa na msaada aliutoa kwa moyo.
"haya nenda  basi ila yule ni bwana angu hivyo naomba umuache la  sivyo tutatoana nyongo" Miriam alimnong"oneza Angel
"sawa nashukuru nitaachana nae sikua najua kama ni wako" Angel alijibu kwa mdomo ila moyoni akiwaza,
"wewe una bahati sana maana kesho ungezika huyu mumeo ila  hakuna tatizo utazika huyu rafiki yako kwanza" Angel aliwaza  kumuua  jesophat, sababu alihofia siri ya yeye kutembea na wembe na sindano.
Waliagana na Angel kuondoka zake,akiwaacha Miriam na jesophat kituoni,
"nishikie niende chooni nikakojoe tu" Miriam aliongea huku akimkabidhi jesophat kimkoba chake,
"haina shida" Jesophat alijibu huku akipokea kwa furaha kwani aliwaza ni kwa jinsi gani angeweza kutoa ule  wembe na sindano ila  akajua ndio mda sahihi wa kuvitoa,na haraka aliingiza mkono wake mfukoni na kutoa kitambaa chake ili kushikia,aliogopa kushika kwa mkono kabisa.
"sasa Miriam kuna kitu kingine cha kukusaidia?"Jesophat alimuuliza Miriam,
"sahivi sina" ila  basi ukitoka shule uwe unapita hapa kunipa maendelo ya huyu bwana angu kipenzi"Miriam aliongea huku akiagana na Jesophat,
"sawa  nitakua nakupitia" Josephat alijibu na kila mmoja kutawanyika.
                                 ********
"Hapa lazima itakua kuna kitu,mimi  najua mwanamke huwa anatembea na kanga ya dharura katika mkoba wake ila sio,sindano na wembe" Josephat alijisemea huku akiingiza mkono mfukoni na kuvitoa,
"tena vina kama rangi  rangi  nyeusi,kwanin? kumbe ndo naskia watu wanachanwa na wembe kwenye gesti na huyu ndo mambo yake nini ngoja kesho jumatatu maana huyu jamaa angu Genes angekufa kizembe aise au sasa walikua na nia gani ? au ni wanga nini" Josephat alijiuliza maswali na kujijibu mwenyewe.
"Ngoja kwanza niende maabara nikavipime maana huyu msichana hata kwenye gari niliona  anavokaa na wasiwasi nikahisi tu kuna kitu"Josephat alijisemea huku akieleka hospitali moja iliyokua karibu na makao makuu ya PPF tawi la kaloleni.
Josephat aliingia moja kwa moja hadi kwa daktari tena ambae alikua jirani yake na kwakua ilikua siku ya jumapili maabara hiyo haikua na foleni kubwa hivyo aliweza kuonana na huyo daktari mapema.
"aah Mr Jose! naona leo umetoka mchicha unaenda kwa demu ako nini" moja kwa moja doctor aliyeitwa August aliongea baada ya kumuona Josephat,
"awapi doctor niko mzunguko tu ila  nkaona  nkupitie hapa nikupe hata salamu tu,sema kuna kitu nilitaka kukijua kutoka kwako maana wewe ni mtalaamu wa mambo haya" Josephat aliongea huku akiingiza mkono mfukoni na kutoa kitambaa chake huku akikikunjua kwa umakini,
"umevitoa wapi kwani" daktari August aliuliza,
"nimeviokota juzi darasani sasa nikashindwa kuvielewa" Josephat alijibu kwa kutumia uongo huo kwani yeye alichokua anatafuta ni ukweli kuhusu hivyo vitu.
"hebu ngoja nivipeleke kwenye vipimo" daktari August aliongea huku akielekea kwenye vipimo kwani hakua mtu wa kupuuzia kitu chochote.
  "leo  nitajua  tu maana mimi  nilihisi tu huyu Angel sio mtu  mzuri" Josephat alijisemea huku akipanguza kiti ili akae.
                                 *******
"Yaani dada Anitha leo  ndo kitu cha kihistoria kabisa" Miriam alianza kuongea kwa hasira baada ya kukutana na Anitha,
"kunani kwanza mbona kama umeparuliwa uso? au umefumaniwa?" Anitha aliongea huku akimkagua Miriam jinsi alivyochafuka,
"heri ingekua fumanizi! hii ni zaidi ya fumanizi" Miriam alijibu na kumwelezea Anitha kila kitu kilichotokea.
"Jaman Miriam utakufa ujue kua mapenzi sio mazuri,mwenyewe unaona mwanaume mwenyewe hakupendi ila  unajilazimisha kwake tu huoni ni ujinga huo mdogo angu,achana na hayo mambo kaa mwenyewe tu" Anitha aliongea mengi ila msimamo wa Miriam ulikua ule ule,
"mimi  nikishapenda nimependa sitaki mchezo kwenye mapenz yaani hako kamwanamke nimekafinyanga kama tonge  la ugali na weupe wake kama mdoli kamekua kekundu kama nyanya" Miriam aliongea kwa dharau.
"Sawa mimi sina usemi kaa makini lakini na biashara zako na hawa kuku wako maana yule mtetea na jogoo ulonipa napambana nazo tu.Waliongea mengi na waliagana huku Miriam akikaa na mawazo mengi kichwani kumhusu Genes,
" sasa huyu mwanaume atafanyaje ili ajue nampenda,au kwa sababu mimi ni mweusi nini, ila mbona wanasema cheusi dawa, na wengine husema weusi asili weupe hutafutwa, mimi  ni mzuri bhana" Miriam alijipa moyo  huku akijiangalia kwenye kioo.
                              *******
"Aise sikaniponyoka alafu Jose ndio kavuruga mpango mzima aise"
"hatujakuelewa unamaanisha nini maana saivi haistahili  awe duniani"
"ndo hivo aise yenyewe nimedundwa  na mwanamke mwenye nguvu utazania anakula ugali wa zege yaani ila naona Josephat ashaharibu mpango wote"
"kwa hiyo sasa kama Jesophat kashtuka lazima aje kuropoka na akiropoka lazima wakubane na ukibanwa utatutaja sasa inabidi huyo Jesophat aanze kufa".
Yalikua mazungumzo katika njia ya simu katibya Angel na Chris.
                                ********
" Huyu Josephat sio mtu  mzuri hata kidogo ingawa ni jamaa yangu ila leo  nimemshutuka sio rafiki wa kweli,yaani ametoka wapi na Miriam mazingira yale isipokua ni mtu  anaeng'ata  na kupuliza?" Genes alijisemea huku akiapa kuuvunja urafiki wake na Jesophat kwani alimatisha kuenda kufanya mapenzi na mtoto mzuri Angel,
"sasa kama sio Jesophat kuja na huyo kima wake wake Miriam siungekuta saivi nishajua ladha ya mapenzi tena  kwa mwanamke mzuri vile ungekuta leo  nimepata joto la kutosha" Genes alimlaumu sana Josephat pamoja na kumchukia zaidi Miriam.
                             *********
"We Jose umesema umetoa wapi?" daktari August aliuliza kwa mshangao na wasiwasi mkubwa,
"Nimeokota" Josephat alijibu kwa hofu,
"hebu njoo hapa" daktari August alimuita pembeni, na Josephat alimfuata haraka na kuingia nae chumbani,
"Hebu angalia huyu panya" daktari August aliongea huku akimchukua panya alieko hai na kumtoboa na ile sindano,
"hebu hesabu sekunde katika hii saa yangu"daktari August aliongea huku akimsogezea Josephat mkono wenye saa ili ahesabu sekunde bila kujua  huyo daktari anamaanisha nini.
"Mama yangu inaua ndani ya sekunde 30 ?" Josephat aliongea huku akitaka kukimbilia nje kwa woga kwani hakuamini kuona  panya anakauka kwa kuchomwa sindano aliyoitoa ndani ya mkoba wa Angel,
"aise nilihisi hiki sio kitu kizuri" Josephat aliongea kwa sauti kubwa mbele ya daktari August,
"kwanini ulihisi?" Daktari August alimuuliza kwani aliona jinsi Josephat alivyobadilika na kua katika hali ya wasiwasi,
"yaani nilivyoikota darasani nilijua sio kitu kizuri" nae Josephat aliongea kumuondoa wasiwasi daktari.
"ngoja mimi  niende kesho nikienda niangalie vizuri kama kuna zingine" Josephat alimuaga daktari kwa haraka.
"ngoja nifike nyumbani haraka nikaende kwa Genes nikampe taarifa ya hiki kitu maana nahisi kuna kitu Angel anataka kumfanyia huyu rafiki angu" Josephat alitembea  kwa haraka sana huku akiwa na mawazo mengi kichwani.
  Doctor August alibaki akiwaza kwa jinsi ile sumu iliyopakwa kwenye sindano na wembe ilivyo na nguvu kubwa ya kuua,
"kama imeua panya kwa sekunde 30 sasa ukimchoma binadamu hata atafika hospital kweli ?" August aliedelea kuishangaa sumu ile.
                                ********
"hapa naenda kwa Genes namtaarifu hiki kitu kisha nitarudi kwa Miriam nimpe taarifa kua huyu mtu sio wakuchezea" Jesophat alizidi kusema huku akipiga hatua kubwa kubwa.
Alipofika katika njia panda ya Sanawari basi kwa mawazo aliyokua nayo alijisahau kuzingatia taa za barabarani,
"we kijana  rudi" sauti ya mbaba mmoja ilitoka kwa ukali ikimwamuru Josephat arudi,
"pita haraka" mama mmoja nae alisema kwa sauti kwani mbele ya Josephat kulikua na lori  linakuja kwa kasi  na hapo Josephat alipoliona limemkaribia basi alinyoosha mikoni juu kama mtu  anaetii amri ya polisi kwani hakuweza kuendelea mbele wa kurudi alikotoka.

Itaendelea.
Jumamosi tuwe sote..

0 comments:

Post a Comment