HATUKUPENDA TUWE HIVI-14

Author

HADITHI,
HATUJAPENDA TUWE HIVI,
SEHEMU YA KUMI NA NNE (14),
MTUNZI Deo Young Massawe
MAWASILIANO 0769297430.
            Sehemu ya kumi na nne (14)
"Waaoooooooh! dada  Anitha yaani mungu ananipigania kila kukicha  na nilikuambia lazima Genes atakua mume wangu tu" Miriam aliongea huku akirukaruka baada ya kumfuata Anitha aliyekua mapokezi,
"nawe  Miriam mbona mara nyingine unachizika mwenyewe" Anitha alimjibu huku akimtuliza kwani Miriam alikua anarukaruka kwa furaha.
"apana dada  sio ukichaa bali nimefanikiwa kumnasa tena Genes niliejua ashanipotea ila nimefanikiwa kujua namna ya kumpata" Miriam aliongea kwa sauti iliyoandamana na mihemo mikubwa,
"kivipi Miriam sikuelewi maana huyo Genes wazaidi ya miaka mitatu leo umempata wapi?"
"we dada  Anitha usiku wa leo  itabidi uje kwangu unisaidie  kazi moja tu" Miriam kutokana na Miriam  kutojua kusoma na kuandika vizuri  alimuomba Anitha msaada wa kuja kuandika barua ya kumpeleka Genes.
                                 *******
"mmh nawe Genes kiwembe kweli kweli aise kama unamiliki tena hiki chuma cha mjapani nilichokutana nacho hapo Aquline" Jesophat aliongea huku akitabasamu kwa kumsifia Genes,
"kivipi man?" Genes aliuliza kwa mshangao,
"ngoja kesho nisubirie huo ujumbe wako,maana kuna kademu fulani keusi hivi wanaita black beauty aise hapo Aquline kakanambia  kanakujua  hadi kitambulisho chako cha shule ya msingi kanacho,alafu naona kavaa sare ya uhudumu wa hapo hotelini kanambia kesho nipitie  hapo anipe ujumbe wako" Josephat alimuelezea Genes kila kitu na jinsi Miriam alivyomuita,
"achana na huyo kahaba tu bhana anajiuzaga hapo nae anataka kuniua mimi, temana nae wala usihangaike kumpitia hapo maana nitaja mzibua bure" Genes aliongea baada ya kuelezewa,
"apana man ila kako powa kama Nick Minaj,yaani anamzidi Angel sema Angel mweupe tu" Josephat aliongea kumsifia Miriam,
"eti Nick Minaj," Genes alimjibu Jesophat kwa kumzarau Miriam.
Baada ya Genes na Josephat  kukubaliana kua wasihangaike na Miriam yeye Jesophat alitaka kujua ni ujumbe gani Miriam anataka kuutuma kwa Genes,
"lazima nimpiteia huyo msichana nione ni ujumbe gani" Josephat aliwaza kisha kuagana na Genes kwani walifika  njia ya kutawanyika kila mtu  kuelekea nyumbani kwake.
                              *******
"Sasa yani nataka unisaidie  kumuandikia huyu mpenzi wangu barua moja hiyo hadi akisoma aniote usiku" Miriam alimwambia Anitha huku akiwa na uso wa aibu kwani alijidharau mwenyewe kwa kutojua kuandika vizuri,
"haya nitakusaidia best, maana nyie watu mnasema mmekufa macho eti hamuwezi kuandika ila kuhesabu pesa mbona hamtuambii tuwahesabie" Anitha nae aliongea utani huku akichana karatasi katika daftari la Miriam alilotumia kuandikia  mapato na matumizi yake kwani aliandika hata hela ya maji aliyonunua kwa siku,
"sasa mimi  nitaandika nini au wewe ndio utasema  mimi  niandike tu" Anitha aliuliza
"Ndio mimi  nitakuambia cha kuandika ila kwanza  hebu jaribu kuandika (mama anapika chakula kitamu) ili nione mwandiko wako kama una mvuto" Miriam aliongea huku akicheka na hapo Anitha bila ubishi aliandika,
"ndio ila uongeze bidii kidogo" Miriam aliongea kwa kuridhishwa na mwandiko wa Anitha,
"sasa siunajua hatua za uandishi wa barua?" Anitha aliuliza huku kalamu ikiwa tayari kuanza kazi,
"we hapa hakuna cha kufuata kanuni za uandishi ila cha kuzingatia ni uandike nachokwambia mimi,kwani siataelewa?" Miriam aliongea na kuanza kutamka  maneno ambayo Anitha alikua akisikiliza kwa makini na kuandika na maneno hayo baada ya kuandika yalisomeka hivi,

Kwako mpenzi Genes,
Natumaini wewe ni mzima wa afya na unaedelea vizuri na shughuli zako ikiwemo masomo.
Napenda kukujulisha  bado upo moyoni mwangu na pia nakutunzia penzi lako la  dhati lililopo ndani ya nafsi  yangu japo tumeonana mda mrefu ila bado upo kichwani mwangu hadi siku  tutakayofunga ndoa na kuishi wote milele nakuahidi hakuna mwanaume nitakayempenda zaidi yako nishaapa kufa na usichana wangu kuliko niishi na mwanaume mwingine zaidi yako Genes,we umekua zaidi ya mwanga moyoni mwangu kila napokuwaza napata moyo wa kufanya kazi kwa bidii.pia nataka nikuone kuna ujumbe wako mwingine ambao nadhani utafurahi sana kuuskia.
Genes sijui nikulezeje juu ya upendo wangu kwako ila napenda kukujulisha tu usome kwa bidii kwani mimi sikubahatika kupata elimu kama wewe ila najitahid kufanya kazi kwa bidii.Mpenzi wangu zingatia sana masomo ya hesabu maana nina hasira yakupambana hadi nije kua na mahoteli mengi wewe uwe mkaguzi wa mahesabu hivyo ndani ya bahasha hii naweka elfu ishirini ununue nayo kitabu cha hesabu kama zawadi kutoka kwangu.Mimi nipo katika ile hotel tuliyokutana miaka mitatu iliyopita na saiv nafanya hapo kazi kama mkaguzi wa usafi wa mazingira na vyumba.Pia ukiwa shule nakuomba ujiepushe na wasichana wenye nia mbaya na wewe kwani wengi wao hawana mapenzi ya dhati kwako tambua mimi  nipo kwa ajili yako na nitajitunza na kuliheshimu penzi langu kwako.
Wako nikupendae,
Miriam.

"haa mtoto wewe  unatoa wapi maneno haya yote?" Anitha aliumuuliza Miriam ambae kwa mda huo alikua analia kwa hisia kali,
"ichore zile alama za upendo basi" Miriam alimsihi Anitha,
"Ah zile ni za watoto hii inatosha" Anitha alijibu na kumkabidhi Miriam barua yake.
Miriam aliichukua na kuikunja vizur kisha kuchukua bahasha na kuweka huko elfu ishirini kisha kuifunga vizuri pia hakutaka kumwambia chochote kuhusu kuokota pochi yake kwani alihofia Anitha kujua masuala ya pochi.
"Haya sasa dada  Anitha kumekua  usiku nami ushamaliza kazi yangu nkupe zawadi gani?" Miriam alimuuliza Anitha,
"hapo Castle lager  mbili tu" Anitha alijibu kwa furaha kwani siku nyingi hajaonja tokea Miriam amshauri kuachana na masuala ya kugawa mwili wake ili apewe bia hivyo alikua na kiu  sana,
"jaman dada  pombe nilikuambia acha kabisa,mimi nakupa mtetea mmoja ukamfuge" Miriam alimjibu kwa huzuni,
"sina banda la  kufugia  jaman mdogo wangu" Anitha alijibu kwa aibu,
"we njoo nkuoneshe kuku wako alafu tufanye utaratibu wakutengeneza banda" Miriam aliongea huku wakielekea kwenye banda la kuku,
"unamuona  yule mweupe pale tena ashaanza kutaga mayai mawili  utachukua vyote na nitakupa jogoo pia huyo mwekundu hapo" Miriam aliongea huku akielekeza  kidole kwa kila kuku aliyemtaja,
Baada ya Miriam na Anitha kuagana basi Miriam alirudi chumbani kwake akaandaa chakula kisha akalala huku barua ikiwa chini ya mto  akisubiria kesho yake kwa hamu kubwa.

Itaendelea,

0 comments:

Post a Comment