HATUKUPENDA TUWE HIVI -13

Author

HADITHI,
HATUJAPENDA TUWE HIVI,
SEHEMU YA KUMI NA TATU (13).
MTUNZI Deo Young Massawe
MAWASILIANO 0769297430.
               Sehemu ya kumi na tatu (13).
Baada ya Genes kuweka pembeni mapenzi na kuzingatia masomo alifanikiwa kuhitimu masomo yake ya msingi nakufaulu kujiunga katika shule ya sekondari ya Arusha iliyokua ikijulikana kwa umaarufu Arusha sec,ambayo ni shule aliyosoma waziri mkuu  mstaafu Edward Lowassa na wengineo  kwani ni shule kongwe sana.
Genes alipoanza kidato cha kwanza ndipo alipoanza tena kuwaza mapenzi kwani aliona wanafunzi wakike walivyovutia kwani wengine walivaa sketi juu ya magoti na wengine walijipaka mafuta ya kujing'arisha nyuso  zao nakuonekana walaini kama watoto  wadogo.
"hakika sekondari sijui kama hawa watoto wanasoma" Genes alijisemea baada ya kuona mdada mmoja wa kidato cha pili akiongea na simu chooni.
Genes aliendelea kusoma kwa bidii na katika mitihani ya muhula wakwanza alikua wakwanza kwa alama kubwa kitu kilichompa umaarufu shuleni hata wanafunzi wa vidato vya juu kumfuata kwa ajili ya kusomea nae.
"Genes mbona we unafaulu sana darasani" Genes aliulizwa  swali na msichana wa kidato cha pili aitwae Angel,
"kwa sababu nasoma kwa bidii pia napenda kuuliza maswali darasani" Genes nae alijibu kwa ucheshi,
"yaani nataman niwe kama wewe" Angel aliongea kwa tabasamu huku akimuonesha Genes mwanya wake wa wastani na kwa kua walikaa kwa kuangaliana  basi Genes alijikuta akimkagua kila kitu kwa mbele ambapo alianzia  paji la  uso  akafurahi kuona mwanya na na meno masafi meupe,lips nyekundu zisizo hitaji make up, shavu pana kiasi.Alihamia kifuani akafurahi kuona Angel akiwa na maziwa madogo yaliyosimama na kuchongoka vizuri ukizingatia na shati alilovaa kuyaonesha vizur ila ghafla Genes alishtuka kuona Angel alipandisha sketi yake na kuacha mapaja wazi,
"mmh huyu ni malkia au binadamu" Genes alijisemea baada ya kuona mapaja meupe yaliyoendana na nguo aliyovaa ndani yenye rangi ya pinki.
Hapo Genes alishindwa kuendelea kuangalia ikabidi  arudishe macho yake usoni kwa Angel na hapo Angel alizid kumchanganya Genes kwa kuonesha tabasamu zaid huku akipenyeza ulimi wake wenye kidoti cha rangi  nyeusi kwa mbali kwenye lips zake.
Genes alisisimka mwili wote na hapo alikumbuka filamu za kizungu mwanamke anapomwonesha mwanaume ulimi hivo mwanaume humfuata  na kumbusu ila kwakua walikua darasani basi Genes alibakia kula kwa macho,
"ama kweli kuna wanawake huku duniani, sasa yule Miriam kitu gani mweusi kama mkaa ?" Genes alijisema huku Angel akisimama tayari kuondoka kuelekea darasani kwake kwani mda wa mapumziko  uliisha  ila alipoanza kutembea na Genes kuangalia jinsi Angel alivyokua na makalio mazur yaliyobinuka basi Genes aliita,
"we Angel"
"abee" Angel aliitikia kwa heshima huku akimsogelea Genes kiasi cha baadhi ya viungo vya Angel kumgusa Genes,
"aise ukitembea una makalio mazuri yanadundika kinoma" Genes aliongea kwa utani,
"Uzuri wa nyumba choo eti" Angel alijibu kidogo kwa uso wa aibu na kugeuka kuelekea darasani kwake, hapo alizidisha manjonjo ya kutembea, kwani aliamini tayari ashamteka Genes akili yake na atafanikiwa kutimiza kazi aliyopewa na marafiki wa Genes waliokua na wivu wa kuongoza kwake kiakili darasani hivyo waliamini wakimtumia mwanamke wakumteka atajisahau na kudorora.
                            *******
Ilipita mwaka na nusu bila Genes kumuonesha Angel kua amempenda ingawa bado Angel alizid kumtega kwa kila njia ila Genes aliogopa sana kujihusisha na masuala ya kupenda kwani alihisi yanaweza yakaja kutokea kama ya Miriam.
Alipofika  kidato cha tatu huku Angel akiwa kidato cha nne basi akina Genes katika somo la  biology walifika  mada ya Human Reproductive System (mfumo wa uzalishaji wa binadamu) ambapo kila mwanafunzi alitega sikio kwa makini ili kusikia jinsi mwalimu alivyoongea mambo ya wakubwa nao wanafuzi wa kike walikaa makini kusikiliza jinsi ya kujikinga na mimba zisizotarajiwa kwa kuzingatia kalenda iliyochorwa ubaoni ikieleza namna ya kuzingatia mzunguko wa hedhi,
"dah kumbe ni rahisi hivi namimi nitajaribu kufanya maana yule boy wangu ananisumbua tufanye kila siku nambania kuogopa mimba ila saivi nitakua nazingatia huo mchoro"
"aaah mimi  boy wangu hatakagi kutumia kondom  ananilazimisha tuende kavu kavu nambania ila saivi naanza kumpa kavu ili afurahi kwani nitakua nazingatia hili duara vizuri".
Hayo yalikua baadhi ya maneno ya watoto wakike baada ya mwalimu kutoka darasani wengine ambao hawajawahi kujaribu kufanya mapenzi basi walitamani kuanza kufanya kwani walipatwa na mvuto fulani kuhusu mada hiyo.
Genes pia aliingiwa na ile mada kichwani na kukumbuka miaka minne iliyopita alivyoota akiwa amelala na Dany alivutiwa sana na kitendo cha  mwanaume kutoa shahawa na akawaza kujaribu nayeye kuonja penzi.
"Leo mmesoma ule mchoro pale ubaoni?" Angel alimuuliza Genes alipoingia darasani kwake,
"ndio tumesoma" Genes alijibu huku akifunika kitabu chake alichokua akisoma,
"vipi umeionaje hii mada" Angel aliuliza kwa tabasamu kama kawaida yake,
"aise kwa kweli hii mada ya reproduction ni nouma sana" Genes alijibu kwa uso wa aibu,
"hata sisi kipindi tunaisoma tulifurahi sana tena  mwalimu wetu alitufundisha kipindi cha likizo kwa kutuchangisha hela kwa sababu alijua atapata  pesa nyingi maana wanafunzi wote waliipenda sana" Angel aliongea huku akizidi kusogea karibu na Genes hadi wakakaa kwa kugusana,
"wewe Angel usinisogelee hivo bhana unajua unanipandishia stem ?" Genes alimnong'oneza Angel,
"mimi mwenyewe stem zimenipanda mbona kitambo" Angel nae alijibu kwa kunong'oneza,
"basi ngoja tutajua  cha kufanya" Genes aliongea kwa sauti ya chini na hapo kengele iligongwa kuashiria mda wa mapumziko  umeisha hivyo Angel alinyanyuka taratibu na kurudi darasani kwake.
                               ********
"Aise Genes huu mlupo ni wako nini maana naona unauimbisha zaidi ya mwaka sasa" Genes aliulizwa na rafiki yake aitwae Jesophat,
"wala mwangu huyu demu ananishobokea kichiz yani,ila saivi nataka nimuwekee heshima maana nikimuacha hivo anaweza enda nitangaza kwa wanawake wenzake kua mimi  ni bwege" Genes alijibu,
"ila mwangu angalia maana hivi vident  vizuri vizur hapa skuli vinatoka na waalimu sana sasa ukija kugonganishwa na master lazima ufukuzwe shule man siunajua tena hiki kidemu kina mashauzi sana kila mtu maarufu hapa shule anamshobokea hata yule mcheza mpira maarufu wa kidato cha pili naskia anatoka na huyu  demu  tena hivyo kaa makini man" Josephat  aliongea kwa kumshauri rafiki yake,
"sawa Jesophat nitakaa makini kwani mimi sitacheza peku" Genes alimjibu rafiki ake,
"powa leo nataka tupite  maeneo ya stand aise nikanunue mkanda kisha tupandie gari Mianzini" Josephat  alimuomba Genes kampani,
"Ahaa mwangu ule mtaa mimi sipiti kabisa maana kuna msala ulinipata nikiwa nasoma la  sita pale hotel Aquline, hivyo mimi  sitofika kule,
"haina kwere mkuu wangu wewe kama unapaogopa hotel Aquline basi utapitia hii road ya kaloleni tukakutane pale corner Florida" Jesophat aliongea huku  akimwelekeza njia atakayopitia ili asipite pale Aquline.
                             ********
"Samahan kaka",
"bila samahan ",'
"nilikua nimekufananisha",
umenifabanisha na nani maana nilikuona kwa mbali unanitazama tu",
"nimekufananisha na mwanaume mmoja anaeitwa Genes"
"Genes yupi? kwani wewe ni nani?"
"Mimi naitwa  Miriam huyo Genes nilijuana nae kipindi cha nyuma sana ila nina picha yake hii hapa" Miriam aliongea huku akitoa kitambulisho cha Genes chenye picha ya passport ambayo Jesophat alishangaa kuona,
"ahaa mimi  pia naitwa  Josephat, hiki kitambulisho umekitoa wapi maana huyu jamaa namjua nasoma nae tena ni rafiki yangu sana" Jesophat aliongea kwa mshangao,
'sasa nitakupa zawadi yako kama kesho utanipitia  hapa jioni nikupe ujumbe wake' Miriam aliongea kwa furaha,
'sawa nitapitia hapa sema sasa wewe mida kama hii utakua wapi?au ni hapa hapa utakua?"Jesophat aliuliza,
"ndio nitakua hapa hapa we pitia nitakuona" Miriam alijibu kwa furaha,
"sawa sawa" Jesophat alijisemea huku akiagana na Miriam.
Jesophat aliongeza  mwendo ili kuenda kumpa Genes taarifa kwani aliamini mda huo Genes atakua Florida akimsubiria  kwani alikuwa amegoma kupitia hotel Aquline.
"itakua huyu demu amemfanyaje?Jesophat aliwaza baada ya kumuona Genes akimsubiria  kwa mbali..

Itaendelea..

0 comments:

Post a Comment