HATUKUPENDA TUWE HIVI-12

Author

HADITHI,
HATUJAPENDA TUWE HIVI,
SEHEMU YA KUMI NA MBILI (12),
MTUNZI Deo Young Massawe
MAWASILIANO 0769297430.
           sehemu ya kumi na mbili.(12)
"yaani hii barua imekujaje hapa ndani kwenye mfuko wa koti langu?" Anitha alimuuliza Miriam kwa hasira,
"hapana dada Anitha hiyo barua kwa kweli nimeiokota tukiwa njiani kuja huku na hadi mwenyewe sijaielewa ila atakua yule mchumba wangu Genes" Miriam alijibu huku akionesha uso wa kusononeka sana.
  Baada ya Anitha kuelezwa  jinsi Genes alikwishawahi kumpa Miriam namba ya simu kipindi cha nyuma basi aliamini kweli barua imetoka kwa Genes ila je kwa nn ipatikane kwenye mazingira yale?.
"Waliandaa kitanda na kujilaza ila kwa kua walikua wawili hivo usingizi ulichelewa kwa sababu walianza utani wao kwa Anitha kuanza
" kwa hiyo Miriam una uhakika Genes atakuoa ?"
"ndio dada lazima atanioa tu,nitajitahid kumtunzia  tunda lake lisije guswa na nyoka"
"kwa uchumi gani Miriam mdada mzuri kama wewe hustahili kuolewa hata siku moja kwani wanaume umekosa  Miriam yanini kuenda kunyimwa uhuru bure"
"hapana dada  Anitha mimi  lazima nitaolewa na Genes kwa maana maisha huwa yanabadilika mfano mimi  nakumbuka nikiwa mdogo mama yangu alishawahi kuumwa malaria kwa mda mrefu ila kwa kua alikua na mume basi mume ndie alietupikia na kumuogesha mama pamoja na uangalizi wake tu kwa mama ulikua mkubwa sasa kama mama yangu angekataa kuolewa angesaidiwa na nani wakati wazazi wake walishafariki na ndugu zake wote wapo na familia zao ? nisikudanganye dada  Anitha vijana tulio  wengi tunaringia uwepo wa wazazi wetu na ndugu zetu ambao hawajaanza maisha na familia zao kwani kila mtu  akiwa na familia yake hataweza kuja kukusaidia kama mpenzi wako, pia hata ukizeeka watoto wako watakuangalia je sasa usipokua na mtoto nani atakuangalia?".
Miriam aliongea maneno mengi zaid ambapo mwisho alipouliza swali hakujibiwa zaidi ya kuskia Anitha akikoroma kwa mbali kuashiria usingizi umechukua.
Baada ya Miriam kuona Anitha amelala basi Miriam aliichukua ile barua na kuweka chini ya mto wake huku mawazo yote yakiwa ni kwa jinsi gani atamuona Genes wake.
                           ******
"dada  Anitha amka tuwahi kazini" ilikua saa  kumi na mbili asubuh ambao ndio mda Miriam aliozoea kuamka  kipindi akiwa mpishi hivyo akamwamsha Anitha,
"alaa! na wewe Miriam ndo wenge  la  kazi au yaani nahisi umelala macho" Miriam alijibu huku akijigeuza na kuweka sawa nguo yake ya kulalia  ambayo kwa mda huo ilikua imeacha mapaja wazi,
"Mmh, huyu dada Anitha ana sura mbili nini mbona naona mguu unang'aa hadi gizani ila mapaja mbona meusi?"Miriam alijiuliza moyoni,
"ahaaa ni yale mafuta yanayochubua mwili jaman itakua kajipaka huyu dada  na wakati niliskia yana madhara mengi sasa huyu anaweza kosa hata uwezo wa kuzaaa mtoto kwa kuathiriwa na haya madawa" Miriam alijisemea moyoni huku akivaa koti kubwa ili aweze kutoka nje kwani aliona kukaa kitandani zaid ni kujichosha tu bure.
                           *********
Genes nae aliona mapenz ni kitu cha ovyo hivyo aliamua kutulia shule na kusoma kwa bidii na hapo ndipo alipoanza kurudi katika hali yake ya zamani.
                             ********
  Baada ya miezi miwili tayari Miriam alishakua  na hela za kuanza kupangisha chumba na kujitegemea kulipia kodi kwani mshahara wake alituumia vizuri na hapo tayari alishaanza ufugaji wa kuku kwa kutumia ile pesa ya Genes aliyoiacha kwenye pochi kwani aliona kukaa nayo tu nikuweka  hela chini hivyo alifanya vile ili izalishe ila hakuacha utani wake kazini awapo na Anitha,
"dada  Anitha leo  umekuja kazini na hasira kwa nini au kuna mwanaume kakuamsha vibaya kama kawaida yako?"
"acha tu Miriam yani kuna mwanaume alikua ananilipia kodi sasa saivi kagoma kanambia eti simridhishi hivyo kama hatalipa kweli siunamjua  yule mzee Kimario mwenye nyumba atanitoa ndugu sijui nitakuja kwako unihifadhi" Anitha alijibu kwa majonzi makubwa kwani hakuamini kumuona Miriam aliempokea mjini akiwa tayari anajitegemea kodi mwenyewe,
"tena alikuja me nikilala  chini lakini yeye analala kitandani na mimi bado najilaza chini,itakua mkosi" Anitha aliendelea kuwaza kimoyomoyo huku akiinamisha kichwa chini,
"dada Anitha ila me sinilikuambia  hawa wanaume ukiwategemea sana unaweza kufa masikini ?"Miriam alimwambia Anitha huku akimwinua kichwa alichokua amekiinamisha chini,
"mdogo wangu maisha haya naona nishakosea tayari" Anitha alijibu kwa aibu
"apana dada bado hujakosea na pia bado hujachelewa sana unaweza jirekebisha na kuja kua na maisha mazuri tu"Miriam alijibu kwa sauti ya kumtia mtu moyo,
"kwa kweli mdogo wangu nimejichezea sana kama ni starehe nimefanya sana na waume za watu saingine nimekua nimekua nikiwadharau hadharani wake za mahawara wangu saivi nahisi dunia inanicheka"Anitha alimjibu Miriam huku machozi yakianza kumtoka,
"hapana dada kikubwa ni kumuomba mungu akusamehe na uweze kuacha tabia hiyo na hapo utaanza kuona mafanikio ya kazi", Miriam alimpa Anitha moyo na hapo Anitha aliinamisha kichwa chini na kuanza kumlilia mungu amsamehe kwa aliyofanya mabaya,
" wewe ni dada angu kabisa siwezi kukuacha  ukiteseka kwani umenipa malazi kwa mda na kunionesha  upendo na sitosahau utani wetu tukianza kutaniana jaman" Miriam alisema hayo huku akiingiza mkojo kwenye sidiria na kutoa shilingi elfu hamsini na kumkabidhi Anitha kwa ajili ya kuenda kulipia chumba.
Miriam aliweza kujipatia pesa nyingi kwa sababu ya uchapaji kazi wake kwa moyo kwani hata mwenye hotel alipokuja  na kumuona anavyopambana hakusita kumuita pembeni na kumpa kitu kidogo na kwakua Miriam hakupenda starehe basi alitunza fedha kuliko kitu chochote na wakati huo alizidi kupedeza tu kwani alichomoza chuchu zake na kiuno kilikua  chembemba huku akiwa na mguu wa saizi wenye weusi wa asili na ulaini wa mafuta ya mgando hakika kila mwanaume alitamani kumuoa pia kwa heshima aliyokua nayo mzee Massawe mwenye hotel alizid kumpeda na hadi siku moja alimuita ofisini kwake na kumuambia,
"hakika mwanangu uchapaji wako kazi unakufanya uje kimiliki hotel kama yangu na zaidi"
"aaah boss na wewe kwa utani, nambie kazi gani umeniitia niifanye  maana kuna mashuka  nimeloweka nataka nifue kabla jua halijatoka" Miriam alijibu kwa kucheka kwani ashazoea boss wake kumtania mara kwa mara,
"hapana mwanangu sijakuitia kitu kingine, nenda kaendelee na kazi ila tambua siku moja utaja miliki biashara kubwa sana" Mzee Massawe alisisitiza,
"haya boss ngoja me niende kuyafua haraka maana tukikaa hapa ofisini wewe unanitania tu", Miriam aliongea huku akiinuka na kuwahi kufua.
                              *** ******
Baada ya miaka mitatu Miriam alikua kashaendelea zaidi ila wakati huo alikabidhiwa kitengo cha kukagua usafi wa kila kitu hapo hotelini, na bado mawazo yeke yote yalikua juu ya Genes,
"nitakufa  na usichana wangu kuliko nitembee na mwanaume mwingine" Miriam alijisemea akiwa nje ya hotel a kukagua mazingira yakoje.
Ghafla alishtuka kuona mtu  kwa mbali,
"yule sio Genes kweli ?" Miriam alijisemea huku akisugua macho ili aweze kuona vizur kwani hakuamini macho yake.

Itaendelea.

0 comments:

Post a Comment