HATUKUPENDA TUWE HIVI -11

Author

HADITHI,
HATUJAPENDA TUWE HIVI,
MTUNZI, Deo Young Massawe
SEHEMU YA KUMI NA MOJA(11).
MAWASILIANO, 0769297430.
             sehemu ya kumi na moja (11).
   "Miriam hapa ndipo nyumbani karibu sana utakaa hapa hadi upate mahali pako pa kuishi,jiskie  nyumbani" Anitha aliongea huku akimkaribisha Miriam aweze kukaa katika godoro  lililowekwa chini,
"Asante dada  nashukuru" Miriam alijibu kwa furaha kwani alimuona Anitha kama mwanake mwenye roho nzuri.
Waliendelea  kuongea huku wakipika chakula cha jioni ili waweze kula na  kulala.
"Yaani wewe mpuuzi tu mwenyewe yule msanii yule cjui nani tena na hela zake zote na umaarufu wake ila ameimba kua anajua hata demu wake kuna siku atamkimbia sembuse wewe na hicho kitambi  chako tu unasema eti siwezi kukuacha  nyoooo! pumbavu" Yalikua maneno ya Anitha akimfokea mtu  aliekua akiongea nae kwenye cm wakati Miriam akiskia  yote hayo,na wakati huo ndio walikua wanamalizia  ugali waliopika,
"nani tena huyo dada Anitha" Miriam aliuliza kiuchokozi akitaka kujua nani ameambiwa maneno hayo,
"huyu ni kinyago  fulani  ana kitambi  ila hana pesa na ananing'ang'ania kama kupe siheri  nimfute kwenye list yangu maana hata shughuli hawezi sababu ya kitambi  chake ukimuona utazania mkuu wa UN (United Nation) kumbe ovyoo" Anitha alijibu na kumalizia kwa kicheko cha zarau,
"nae Miriam alicheka  ingawa hakufurahia maneno hayo ila ilibidi ampe ushirikiano mwenzake.
Baada ya kula Anitha alikua wa kwanza kueda  bafuni,
"sasa nisome ile barua" Miriam alijisemea huku akiingiza mkono mfukoni na kutoa zile karatasi mbili akaziunga tayari na kuanza kwa makini.

Dear,Miriam.
Natumai unaedelea vizuri mpenzi wangu Miriam,mimi  tokea ile siku nimekuja kwako ndo nikapigwa na mama yako hadi leo nimekua silali wala sili chakula kwa ajili yako hata shuleni  siwezi tena  kusoma kwani nakupenda sana na wewe umekataa kunipenda,sasa naomba nikuambie tena nakupenda sana naomba nikubalie nitakupa pesa kwa sababu baba yangu ni tajiri na mama yangu ni tajiri.Hata usiku nakuona ndotoni unanijia hadi natamani kukugusa mwili wako ila nashtuka,hivyo naomba tu unikubalie niwe mpenzi wako ili niwe na raha maana hata saivi nilikunywa maji kwenye glasi nikakuona sasa nateseka sana moyoni,Miriam ukinikubalia nitakuja kulala na wewe nikufanyie kama wafanyavyo wacheza tamthiliya za kifilipino kwani nafurahi sana pale wanapokumbatiana  na kutomasana sehemu mbali mbali za mwili huku wakipigana mabusu kila mahali.Miriam naomba nikubalie jaman ila kama hutakubali basi usinichukie kwani bado nina nia ya kukusaidia  kurudi nyumbani.Ukimaliza majibu yaandike nitakuja siku ingine hapa ndo unipe au unitafute kwenye namba ile ya simu niliyokupa natumai unayo.Nakupenda sana Miriam I LOVE YOU Mwaaaah.
Wako nikupendae,
Genes.

Hayakua  maneno mengi sana hivyo aliweza kumaliza kabla hata Anitha hajarudi.
"mungu wangu jaman hii barua imetoka  wapi na kwa nini niliiokota mazingira yale tena ikiwa kama imetupwa vile mbona nashindwa kujua" Miriam alijisemea huku akijizungusha zungusha kwenye godoro kwani tokea azaliwe alikua hajawahi kuandikiwa  maneno mazuri kama hayo tena kilichoyafanya yakawa mazuri ni kwa vile alijua imetoka kwa Genes mwanaume wandoto zake, hapo hadi alijihisi kuloa  baadhi ya sehemu za mwili wake kwa furaha aliyoipata ingawa alishindwa kujua kwa nini itupwe mazingira yale?
"labda aliniona nikija ndo akaitupa ili niokote?ila hapana  mbona karibu hapakua na mtu ?na kama aliitupa ili niokote aliitupa lini mbona inaonekana imechafuka kidogo pia inaonekana haijatupwa siku hiyo.
Miriam alifurahi sana hapo akatoa  kitambulisho katika pochi ya Genes na kuibusu mara tatu huku akitoa  machozi ya furaha kwani tokea avunje ungo  ndo aliskia hisia zimempanda hadi kumloanisha nguo ya ndani,
"huyu mwanaume nampenda   jamani ila yeye sijui kama ananipenda au la  maana mara  anaacha pochi yake chumbani naikuta mara  anatupa barua njiani naipata  sasa kwa nini anafanya haya ? na je anakua na uhakika gani kama mimi ndie nitakaeipata ?" Jaman mme  wangu Genes nakupenda"Miriam aliongea huku akirudisha barua kwenye mfuko wa koti na pochi akaificha kwenye nguo ya ndani kwani nguo yake ya ndani ilikua yakumbana hivyo haikua shida pochi kukaa sawa mahali hapo kwani aliamini ndipo mahali salama,
"hawa wanawake wanajiita watoto wa mjini wanaopenda pesa zaidi ya utu hawachelewi kuzichukua" Miriam alijisemea aliposkia vishindo vya Anitha akitokea  bafuni.
"haya ndoo hiyo hapo mimina maji hapo jikoni  bafuni ni nyuma ya chumba hicho hapo cha mbele" Anitha aliongea huku akimwelekeza mahali bafu ilipo.
Miriam alivua  nguo na kujifunga  kaka kisha kumimuna maji jikoni
"Miriam una viziwa mchongoma wewe mwanaume gani atavinyonya ?" Anitha aliuliza kwa uchokozi,
"heee mamae vina mwenyewe wakuja kuvimeza kabisa" nae Miriam alijibu kwa furaha,
"yule dogo mwenzako unamwita sijui Genes?"Anitha alizidi kuuliza,
" haswaaa kama ulikuepo vile"Miriam alijibu kwa kuringa  huku akimwonesha Anitha maungo yake yalivyoumbika kwa kuchezesha kiuno kwa kumringishia Anitha kisha kutoka na maji na kuenda bafuni.
"ila ukae makini hiyo bafu haina bati kwa hiyo ukiweka sabuni hapo juu watapita nayo njia" Anitha aliongea kwa sauti,
"Powa dada" Miriam alijibu nae kwa sauti akiwa anasukuma mlango wa bati ili aweze kuoga.
Kama kawaida yake ya kujijali kiafya basi alianza kwa kumwaga maji bafuni ili kuua baadhi ya bakteria,
"sina baba wala mama mjini hivyo lazima nijitahidi kujikinga na haya magonjwa kwani nikija kushikwa  na haya wanayoita sijui UTI na mengineyo hadi nije kupata msaada ni mbali sana"Miriam alijisemea kwa kujijali na kuanza kuoga.
Anitha alibaki chumbani ila hapo akapata wazo,
"hivi kwenye mfuko wa koti  la  Miriam kuna nini? maana hawa watoto wanaweza kua na fungu  ila wakawa wanakuchora" Anitha alijisemea huku akilivuta koti la  Miriam na kuanza kulipekua,
"haa kweli huyu mtoto siyo  barua hii kaletewa wapi duh, hebu ngoja niisome Anitha aliongea huku akiunganisha vipande viwili na  kuanza kusoma.
"Jamani huyu dada  Anitha ananambia ana wanaume sita tena wazito kipesa sasa mbona maisha yake ni ya chini tu,au wanampa hela yeye anapeleka wapi, chumba chake hakina hata kitanda jaman simcheki ila kwanini anakubali kujiumiza  sehemu zake za siri bure ? maana hata wasomi wanakwambia  kama biashara unayofanya haikulipi basi achana nayo" Miriam alijisemea kimoyomoyo kwa kumhurumia dada Anitha kwa maisha anayoishi,
"ila ngoja nitaenda kuongea nae maana anaonekana ni mtu  anaependa maongezi tushauriane namna ya kutumia mishahara yetu kwa kuifanya  izalishe pesa nyingi" Miriam alijisemea akipiga  hatua za madoido kwani hakutaka anapotoka bafuni achafuke hata kidogo.
"Dada nishamaliza kumuoshea Genes tunda lake" Miriam aliingia ndani na kuanza kuongea utani ila kwa wakati huo Anitha hakumjibu kitu zaidi ya kumkazia jicho,
"We dada  Anitha unataka kusema mwanaume kakuuzi unaniletea hasira hadi mimi?unaloo" Miriam alizidi kuongea utani wa kumchokoza Anitha ila alishangaa Anitha kuzidi kumkazia jicho.
Miriam alipomwangalia Anitha mkononi alishtuka kumuona na vile vipande viwili vya karatasi ambavyo vilikua  na ujumbe kutoka kwa Genes..

Itaendelea.

0 comments:

Post a Comment