HATUJA PENDA TUWE HIVI -10

Author

HADITHI,
HATUJAPENDA TUWE HIVI,
SEHEMU YA KUMI (10),
MTUNZI Deo Young Massawe
MAWASILIANO, 0769297430.
                    sehemu ya kumi (10).
  "Sasa pochi yangu itakua imepotea  na kitambulisho changu cha shule kimepotea ila kwa kua kile kitambulisho kina picha yangu na jina langu basi mtu  akikipata ni rahisi kunipata,ila  namkumbuka rafiki yangu Deo ananipaga ushauri kua napopoteza kitambulisho niende kituo cha polisi kutoa taarifa maana mtu  mbaya akikiokota alafu akaenda kufanya tukio la  kihalifu kisha akitupe hicho kitambulisho basi lazima nitafutwe  ila kama ukienda kutoa taarifa wala hutahisishwa na tukio hilo"
Genes alijisemea akiwa Kwenye daladala kurudi nyumbani.
Kuanzia siku hiyo Genes aliyachukia mapenzi na aliapa  kutopenda tena kizembe kwani aliona kama vile kupenda ni kujiingiza katika matatizo maana kupenda ndiko kulimsababishia yote hayo.
"Hadi shuleni  nimeanza kupoteza raman  kwa ajili ya mapenzi, saivi shule nitakua nasoma kwa bidii mapenzi yapo tu nitaja yakuta tena nitampata  msichana mwaminifu sio huyu Miriam muuza mwili" Genes aliendelea kujisemea kwani alikua na mawazo sana na hapo alipanga akifika  nyumbani atadanganya anaumwa ili aweze kukaa tu ndani.
                             ********
"Hii pochi itakua ya nani?" Miriam alijiuliza  huku akikaa kitandani ili aweze kuchunguza vizuri pochi aliyoikuta kwenye chumba  Genes alicholala,
"heee ina hadi pesa nyingi hivi,zinatosha kwenda Manyara,ngoja nikamwoneshe dada  Anitha"
Anitha ndo dada alimchorea kazi hivyo ndo alikua rafiki yake kwa mda huo,Miriam alijisemea huku akiinuka  ila kabla ya kutoka nje alirudi kukaa kwani aliona kitambulisho ikabid akitoe na hapo hakuamini kukutana na picha ya Genes katika kitambulisho ambacho kilikua ni bima ya afya pamoja na cha shule hapo aliibusu sura ya Genes katika hivyo vitambulisho  ,
"sasa hapa mungu mkubwa jaman hata napata faraja ya maisha yangu kua na picha ya huyu mwanaume" Miriam alijisemea  moyoni na hakutaka tena kumwonesha Anitha,
"sasa Genes itakua ni mganga wa kienyeji nini?,kwani alijulia wapi kua nitakuja kufanya kazi hapa ndio aache vitu hivi vyote?,au itakua kuna sababu nyingine yayeye kuacha?,ngoja nitamuuliza dada  Anitha" Miriam alijisemea hayo wakati akificha pochi hiyo ndani ya mfuko wa sweta kubwa alilovaa kutokana hali ya ubaridi mkoani Arusha.
                             ********
  "We Genes hebu fungua mlango wako nataka nijue kwa nini hutaki kuenda shule,na nataka kujua hela zangu nani kaiba hapa chumbani kwangu" mama yake Genes aliongea kwa sauti kubwa iliyomfanya Genes ashtuke na kujifuta machozi yaliyokua yanamtiririka.
"Mama mimi naumwa",
"Unaumwa wapi",
"kichwa naskia yani homa inanijia mama"
"ahaa pole mwanangu hebu ile bima yako ya hospitali niangalie kama imeisha ila tufanye utaratibu wa kuenda kukutibu"
"Mama ile bima niliweka hapa ndani hata siioni,"
"sawa mwanangu jiandae tuende basi hapo kituo cha afya na kitambulisho chako cha shule"
"hata hicho sikioni mama"
"mwanangu siku hizi umepetwa na nini mbona sikuelewi maana hata walimu wako shuleni  wanalalamika umekua mzembe,na huku nyumbani umekua mzembe nini shida mwanangu unajua mtihani wa kuhitimu masomo ya msingi ndio unakaribia?".
Genes na mama yake waliongea  mengi na kutokana na mama kua na moyo wa huruma basi aliacha  masuala ya kupotea kwa hela na kumhudumia mwanae.
"Ila usikute unanionea mimi mama yako kwakua baba kasafiri ?"mama Genes alimuuliza Genes kwa utani huku akimpa maji ili ameze dawa aina ya panadol kwa ajili ya kutuliza maumivu.
"Yaani haya yote ni huyu mbwa mwitu aise Miriam siutoe huu mkosi unaoniachia kumbe hadi maza kashasanda kuwa shuleni nimekua mbulula aise" Genes alijisemea baada ya mama yake kumuacha alale.
                                ******
"Hivi dada  Anitha, leo asubuh yule kijana aitwae Genes ilikuaje  hadi akaja kukamwatwa?" Miriam alimuuliza Anitha baada ya kumaliza  usafi,
"aah kale katoto bhana kajinga sana kalianza  kukabidhi  ufunguo kakaondoka ila baada ya mda kakarudi tena ndipo kalipokamatwa" Anitha alijibu huku akicheka,
"kwa hiyo kalirudi  kufanyaje" Miriam aliongeza swali,
"hata cjui maana kana mambo ya kitoto bhana maana kalikuja kakawa kanachungulia ndo wakamshika ila mwanzo alikua ashakabidhi ufunguo kwangu"Anitha alijibu ila uso wake ulionesha kuchokwa na maswali.
"Sasa dada  Anitha huyo ndie mume wangu" Miriam alimwambia Anitha kua Genes ndie mume wake tena kwa kujiamini,
"wee kale katoto kula kwa mama yake kulala kwa mama yake hata nguo za ndani itakua anapewa na mama yake,katakupeleka wapi sasa mdogo wangu? sema mimi  nikutafutie bonge la  bwana likuvalishe na kukugharamia kila kitu,tena wewe mdogo mdogo hivi na mwili wako unavovutia na huo weusi wako wa asili lazima tupige pesa hadi za watalii" Anitha aliongea kwa kumsihi Miriam,
"hapana dada yule ni mtoto ndio ila thamani yake niliiona  siku moja tu na nikatokea kumpeda sana na sitomuacha hata kama hatanipa kitu mimi  nitampa" Miriam alijibu kwa kusistiiza,
"mdogo angu itakua umechanganyikiwa, yaani hapa mjini ni mipango hivyo unavyotaka kufanya huwezi tembea na mtoto kama yule,we kwanza unavyoniona mimi  nina wanaume sita tena wazito kihela acha hizo michepuko na hawanitoshi  bado,mungu amekupa  mwili wenye tundu  hivyo basi litumie mdogo wangu,yaani we unatembea  na mgodi hivyo uliona  wapi watoto wakiingia mgodini?, hivyo mdogo wangu angalia mwenye pesa sawa?",  Anitha alimwambia Miriam ambae kwa mda huo aliinamisha kichwa chini na kutafakari juu ya maisha  yake,
"mungu nitie  nguvu kama kila mtu  nakaa nae ananishauri juu ya kujiuza tu nitaishi na nani?,Genes pekee ndie wakunioa milele sitomsaliti na nitafanya kazi yoyote kwa malengo" Miriam alikua anajisemea kimoyomoyo huku kichwa kikiwa  chini,na hapo aliwaza baada ya mda akamwambia Anitha,
"mimi huyo Genes ni mtu  muhimu sana katika maisha yangu siwezi kumwacha  ingawa hata mahusiano hayajaanza maana sasa kama ukinambia  niwe na wanaume wengi nitaweza kupata ukimwi" Miriam aliongea kwa uso wa huzuni,
"mdogo angu ukimwi sio wa kuogopa bali inabidi uogope mimba kwani ndo itakuzuia kuendelea na kazi zako alafu ukute mbaya zaidi imekuja  kipindi huna hela ya kutoa,ila ukimwi hata ukipata bado utapiga pesa tu mdogo angu saivi wanasema hapa kazi tu sasa wewe lala ule ndoto zako,hapa mshahara ni mdogo sana hivyo ukiutegemea wala hutoki  milele" Anitha alizidi kutoa maneno yaliyompasua Miriam kichwa hadi akashindwa kujua ni wapi atapa mtu  mwenye malengo ya kufanya kazi kwa bidii,
"Dada Anitha mimi nitajitahidi kufanya kazi kwa bidii hadi nifanikiwe, maana mimi nauogopa  sana ukimwi ingawa wanasema kuna kinga  ila mimi  heri nisifanye kabisa kwani mtu  akiamua kukuambukiza ukimwi atakuambukiza tu hata akivua hizo mipira utajulia  wapi ?, we hujui wanaume wengi wana malengo mabaya na sisi kinadada ?,na pia hata kama mshahara wa hapa ni mdogo nitajitahid kuufanyia  kazi uwe mkubwa kwani hela nikipata nisipotumia ovyo nikikusanya na kufuga  hata kuku sinitakua  na kuku wengi nikija kuwauza nitakua tajiri tu," Miriam aliongea kwa kujiamini kwani hakutaka kufanya kitu cha kujiharibu mwili wake, yeye aliamini kazi yoyote inaweza kukufanya kuwa tajiri na hata hapo aliwaza kuhusu watu wanaodharau kazi za ndani eti ni za kijinga na mshahara mdogo,
"hivi kwa mfano hata ukifanya kazi za ndani kama unakula na kulala bila kukatwa mshahara alafu ukalipwa elfu sabini ina maana ukinunua kuku wa elfu arobaini na chakula cha elfu ishirini ukatafuta  kaeneo  ka kufugia  siutafanya hivyo kila mwezi na hatimaye utakua tajiri? kikubwa ni kufanya kazi kwa bidii bhana na kuepukana na kutumia hela ovyo kwa kujiepusha na starehe na anasa" Miriam alijikuta akiwaza kwa hasira moyoni kwani alikua na moyo wa kufanya kazi kwa bidii.
"Mdogo wangu ila wewe jitahidi kujitunza na kufanya kazi kwa bidii tuone kama utatoka,wewe mimi  nitakusaidia sehemu ya kulala baada ya kutoka hapa kazini" Anitha alimwambia Miriam,
"nitashukuru dada Anitha kwa kunipa hifadhi mimi  nitafanya kazi kwa bidii nakuomba unihifadhi kwa miezi miwili tu", Miriam aliongea kwa kushukuru  kwani kupata sehemu ya kulala ilikua furaha sana kwake,
"Ila kama ana wanaume sita tena wazito kihela basi atakua ana nyumba yake" Miriam alijisemea moyoni kwa kuhisi Anitha atakua tajiri sana kwa kua ana wanaume wengi wenye pesa wanaoutumia mwili wake.
  Jioni ilifika ambapo Anitha na Miriam waliongozana kuelekea nyumbani ambapo Anitha alipanga chumba chake maeneo ya Sekei karibia na hotel ya Mount Meru.
Wakiwa njiani Miriam alikua na mawazo ya kwa jinsi gani ataweza kuonana na Genes kwa mara  nyingine ili aweze kumkabidhi pochi yake yenye pesa na vitambulisho  kwani alishajua  aliisahau ndo maana alirudi kuichukua ndipo akakamatwa.
Wakiwa wamefika Mount Meru hotel hapo Miriam aliona karatasi iliyochanwa vipande viwili  na kuviringishwa pamoja,kutokana na tabia yake ya kupenda usafi basi aliliokota ili kulitupa,sehemu husika ila alitembea umbali kidogo  bila kuona sehemu ya kulitupa hivyo akajikuta analifumua ili aweze kusoma kilichoandikwa,
"ha mbona jina langu?" Miriam alijisemea baada ya kukutana na neno
"Dear Miriam" ambalo ndio neno la kwanza aliloona  katika kipande cha kwanza cha karatasi na hapo akasema,
"ngoja nikifika nyumbani nitasoma vizur" kisha aliviweka vipande hivyo mfukoni na kua na hamu ya kufika nyumbani kwa Anitha mapema ili kuweza kuona faida ya kuwa na wanaume wengi jinsi Anitha anavyodai kua na watu wazito pamoja na kujua nini kilichoandikwa katika karatasi aliyoiokota njiani..

Itaendelea,.

Kama hujasoma hadithi zangu zilizopita waweza kuzipata kirahisi katika page yangu #Deo_Massawe,, katika hiyo page utaziona kirahisi zaidi.

0 comments:

Post a Comment