HATUKUPENDA TUWE HIVI -09

Author

HADITHI,
HATUJAPENDA TUWE HIVI,
SEHEMU YA TISA (9),
MTUNZI Deo Young Massawe
MAWASILIANO 0769297430.
                     Sehemu ya  9
"Broh vipi hapo Mianzini shilingi ngapi?" Genes alimuuliza dereva pikipiki kwani alitaka  kupanda pikipiki hadi kituo cha Mianzini ambapo angeweza kupanda daladala hadi kwako,
"Hapo buku jero tu boss wangu" dereva pikipiki alijibu,
"aah nawewe acha hizo,sinitembee na miguu" Genes nae aliongea kumaanisha kiasi alichotoswa ni kikubwa kulingana na umbali wa kutoka Aquline hotel hadi Mianzini,
"haya basi leta hiyo buku chap nikurushe kama fast jet" dereva pikipiki aliongea huku tayar kashawasha pikipiki,
"siuna chenchi ya msimbazi?" Genes aliongea huku akipanda kwenye pikipiki kwani alijua amebaki na elfu arobaini na ni elfu kumi kumi zote,
"aise asubuhi hii bado  cjakamata mpunga huo  labda ulete nicheki kwa marafiki zangu hapa kijiweni" dereva pikipiki aliongea huku akijiandaa kupokea pesa na ndipo Genes alipoingiza mkono mfukoni na kushtuka hajachukua  pesa zake pale alipoziweka kuelekea kuoga,
"mama yangu nimesahau pesa pale chumbani" Genes aliongea huku akitimua haraka kurud hotelini,
"cheki huyu bwege ananitia gundu asubuhi hii yote" dereva pikipiki alijisemea huku Genes akiishia.
"sijui kama nitazipata mungu angu kama ashaingia mtu  huko ndo basi tena" Genes alijisemea huku akipiga hatua kubwa kubwa kuelekea hotelini.
                             *******
"Kweli huyo kijana wakati anaingia  jana ni mwenzangu alikua hapa mapokezi ila kwa taarifa za hapa kwenye daftari zinaonesha aliingia mda sawa na huyo Miriam, alafu mngewahi kidogo tu mngemkuta maana kaondoka kama dakika kumi na tano zimeisha saivi"  hayo talikua maneno ya dada wa mapokezi alikua anawaelezea askari walioenda  kumchukua Genes kwa ajili ya ushahidi wa tukio la Miriam ila kwa bahati mbaya wakakuta kashaondoka.
"sasa dada hebu kama inawezekana  tukafungue chumba cha huyo Genes tuangalie kama kuna kitu chochote cha kuchunguza maana pia kwanza kwa nini mtoto mdogo hivo aje kukodi chumba huku hotelini" aliongea askari mmoja kwa sauti ya kushauri,hapo wote waliandamana kuelekea chumba namba sita ambacho ndicho Genes alicholala.
                            ********
"Miriam akiwa kituoni aliendelea kumuomba mungu amsaidie tu ili aweze kuonana na Genes 
" hakika huyu Genes nisipomwona nimshukuru na kumwonesha hisia zangu itakua nimefanya kosa kubwa ila naamini kwa uwezo wa aliye juu lazima nitafanikiwa kuonana nae leo tena mda sio mrefu"Miriam aliendelea kujipa  natumaini kwa kiasi kikubwa kwani nia yake sio kuhitaji ushahidi bali ni kumwona Genes tu basi.
                           **********
"cheki huyu Miriam ndo mkosi wa haya yote hadi namkosa huyu dada wa mapokezi hakika huyu mwanamke anganiletea balaa kwenye maisha yangu" Genes alijisemea hayo akiwa mapokezi ili aweze kutoa maelezo ya chumba alichotoka nakusahau huko pesa zake ila hakumkukuta dada  aliyekua zamu kwa mda huo ila hakujua kama kwa mda huo ndio chumba alichotoka kinafunguliwa.Baada ya kusubira kwa dakika mbili aligundua akili aliyopewa na rafiki ake aitwae Deo kua kama ukisahau kitu cha thamani ndani alafu ukapotea ufunguo wa kufungua chumba chenye hicho kitu cha  thamani basi haraka inakupasa ukachunge hapo mlangoni ili mtu hata akiokota huo ufunguo asiweze kuja kufungua,hivyo baada ya wazo hilo aliamua kuelekea karibu na chumba alichotoka hadi dada wa mapokezi arudi.
"Haya yote ni Miriam anasababisha" Genes aliendelea kumtupia Miriam lawama huku akitoka mapokezi kuelekea chumbani ila ghafla alishangaa kuona mlango wachumba alichotoka ukiwa wazi na kwandani kukiwa na watu na hapo aliona sare ya askari.
"mmmh sio kuzuri hata kidogo" Genes alijisemea na kuwaza labda kuna namna amehusishwa katika patashika ya jana,
"hapa heri ipotee tu hiyo pesa" Genes alijesema kwani aliogopa kuhusishwa na kesi yeyote kwa maana aliogopa nyumbani akijulikana hayupo kwa shangazi ambapo jana yake aliaga kuenda huko basi nyumbani patawaka sana,ila wakati akijishauri kugeuka basi alionekana na dada wa mapokezi,
"we Genes njoo hapa unatafutwa"Dada aliongea kwa sauti kubwa ila Genes alijifanya hajaskia na akataka kukimbia ila askari mmoja alitoka na kimkamata.
Hapo wote walijiuliza kua kafuata nini kwa sababu alishakabidhi funguo na kuondoka,
" huyu itakua ana lakwake jambo"askari mmoja alijisemea kwani mda huo nae akawa anachunguzwa ingawa walimfuata kwa ajili ya kuenda kutoa ushahidi ila nae walimhisi kama mhalifu kwani alipoulizwa kuwa kafuata nini alidai kaja kumsalimia mdada wa mapokezi kitu ambacho askari walimtilia mashaka.
Gari ya police iliondoka na Genes huku Genes akiwa anaumi moyoni kwani alizidi kumchukia Miriam kwa yote yaliyokua yakitokea,
"sasa hapa nakamatwa ni lazima baba yangu atajua na mama yangu pia na jamii yote inayonizunguka itajua kua nimekamtwa mazingira ya quest tena wakati wa masomo kisa huyu Miriam na alaaniwe na hela zenyewe zitapotea aah shenzi kweli huyu mwanamke" Genes alijisemea kimoyomoyo huku gari ikiwa kasi kuelekea kituoni na mda huo ilikua ni saa moja asubuhi.
                              ********
Hapo kwanza Genes alianza kutumika katika kutoa ushahidi juu ya kesi ya Miriam ila askari walishanga kusikia  Miriam akisema,
"jaman huyu baba ingawa alitaka kunibaka nimemsamehe ila chakufanya  anilipie nauli ya kurudi nyumbani"
"we binti unajua utaratibu wa mahakama au unaongea  tu" askari mmoja alimjibu Miriam,
"siujui ila naomba mimi  ni mtoto sitaki kupambana na kesi hivyo yaishe" Miriam aliongea kwa msisitizo mkubwa kwani alikua na uso wake wake ulimwangalia Genes kwa furaha ila Genes alimkazia sura hakuamini kabisa kama mwanake huyo ndo anamletea balaa zote hizo.
Askari walishikwa hasira na hapo wakaitana pembeni na kujadiliana ambapo mkuu wa upepelezi aliongea,
"hii kesi me siielewi kabisa hapa tuchukue hapo hela ya chai tupite  zetu kushoto hawa mara  mshtaki hataki kesi mara wote hawaeleweki" baada ya kusema hayo walirudi na kuwataka kiasi cha pesa ili waweze kufuta makosa hayo ambao mhalifu wa Miriam alitoka shilingi elfu sitini kunyamazisha yote pamoja na kumpa Miriam elfu 50 kwa ajili ya kusafiria  jinsi alivyodai na kesi ikawa imeisha.
"sasa nyie kila mtu  aondoke  kwa amani hapa ila wewe dada tutakurudisha hadi pale Aquline hotel maana tulikutoa hapo" aliongea askari mmoja kwani kufanya hivo kungeimarisha usalama wa Miriam,
"na wewe kijana utabaki hapa hadi wazazi wako waje kutoa maelezo yako maana kwanza bado unaonekana unasoma ila mara  unatoka  hotelini na kurudi hivyo wewe utabaki hapa" askari mmoja aliongea huku akiinuka  kwa kumwita Miriam ili aweze kumrudisha Aquline hotel,
"sitaki nimwache huyu Genes mikononi mwa askari" Miriam aliongea kwa sauti mbele ya askari wote kwani Miriam alipandwa na hasira kuona akili aliyotumia hadi Genes akafika pale inataka  kuzuiwa tena wasiongee hivyo Miriam aling'ang'ania kuondoka na Genes yaani warudishwe pamoja pale Aquline hotel.
Baada ya mvutano wa muda basi askari walimtosa Genes shilingi elfu 30 ili waweze kimruhusu atoke ila Genes alidai hana hela na hapo Miriam aliamua kutoa elfu 30 kwenye elfu 50 aliyopewa ili kumlipia Genes kisha wakarudishwa wote pale Aquline hotel.
"Hata unichangie figo sitaweza kukaa na wewe" Genes akijisemea moyoni.
Genes aliwaza  kua atafikaje nyumbani kwani alishatoa sadaka zile pesa alizoacha chumbani sababu aliogopa sana hata kukaa mazingira ya pale hotelini.
"Yaani hii gari ikisimaa tu natoka nduki leo natembea kwa miguu hadi nyumbani" Genes alijisemea alipoona  geti la  hotel Aquline,
"yaani mungu mkubwa leo  nitaongea na mume  wangu kila kitu" Miriam nae alijisemea moyoni kwa furaha gari ilipokua  ikiingia getini.
Baada ya kushuka  askari waliwaaga kwa amani ila Miriam kwa haraka alitoa ile elfu 20 iliyobaki na kumkabidhi Genes elfu 10,
"Mume wangu tugawane hii" Miriam aliongea kwa  tabasamu huku akimkabidhi Genes hiyo pesa ambapo baada ya Genes kupokea alianza kuondoka kwa kasi,
"kumbe ulijua sina hata nauli?" Genes alijisemea baada ya kumshinda Miriam mbio na kupanda pikipiki ambapo alimwacha Miriam pale getini.
Miriam hakuamini macho yake kwani aliona kama mtu aliyeokota dhahabu na kuipoteza,
"sasa hii elfu kumi haitoshi hata kunifikisha nyumbani Manyara" Miriam alijisemea huku akiwaza kurud hotelini na kuomba msaada mwingine lengo lake likiwa  kuongea na Genes tu,hivyo alielekea mapokezi.
Miriam aliongea na dada aliyekua mapokezi kwa mda mrefu ambapo Miriam aliongea historia yote ya maisha yake na hapo huyo dada alimfanyia mpango akapata kazi ya  kufua mashuka  na kufanya usafi katika vyumba, na hapo Miriam aliwenza kuanza kazi siku hiyo hiyo.
"We Miriam ukifanya usafi uhahikishe unainua magodoro na kuangalia kwenye machaga vizur kwani kuna wanaume wengine wasio wastarabu wanaweza lala na mwanamke alafu  wanaficha huko mampira yaliyotumika" Miriam aliambiwa huku akiwa kubeba maji na dekio kuelekea kwenye baadhi nyumba ambavyo  tayari watu washatoka.
"Tena naanza na hiki chumba mme wangu alicholala" Miriam alijisemea huku akifungua chumba alicholala Genes...

Itaendelea,

0 comments:

Post a Comment