HATUJA PENDA TUWE HIVI-08

Author

HADITHI,
HATUJAPENDA TUWE HIVI,
SEHEMU YA NANE (8)
MTUNZI Deo Young Massawe
MAWASILIANO 0769297430.
                    sehemu ya nane (8)
"We kijana unafanyaje hapo mlangoni,simama hapo hapo usiingize miguu yako ndani" Genes aliskia sauti nzito  nyuma yake wakati ndio anaanza kuingia chumba ambacho aliona miguu ya mtu  ikiwa chini ikimaanisha  mtu  kajiegesha tu,ila Genes alishindwa kujua kwa nini kakoromewa hivo na alipomwangalia mbaba mwenyewe alikua  kajifunga shuka la  kimasai na alikua kama anahema sana kwa hofu fulan kana kwamba anafukuzwa au kuna kitu anataka kufanya cha hatari,
"hapana baba nilikua naangalia huku chumbani maana nimeandikiwa niingie chumba namba tisa  ila nimepewa  funguo za chumba namba sita hivyo nikataka kujua huku ndani kama kuna mtu" Genes alijibu kwa hofu
"kwanza we mtoto mdogo unakuja Kulala huku kwani huna kwenu?" Genes aliulizwa  kwa hasira ila hakujibu kitu zaidi ya kurudi mapokezi ili kujua kama ni dada wa  mapokezi kajisahau.
"Samahan baba, huyo uliyekua unaongea nae hapo nje ni nani ?" Miriam alimuuliza msamaria wake aliemdhamini sehemu ya kulala,
"ni mtoto mmoja mshenz kweli hata cjui anafuata nini huku usiku huu,ila nishamtimua alitaka  kutuharibia raha zetu"
"raha gani tena baba kwani ulinambia naletewa chakula nashangaa wewe ndo unakuja" Miriam aliongea kwa hofu kwani pale tayari alijiwa na kumbukumbu ya sauti ya Genes na alitaka  kujua kama ndie yeye au ni nani na kama ni yeye amekuja kufuata nini pale,
"sasa wewe binti sikia mimi  nimekuja huku ndani kwa ujanja ujanja tu sijajiandikisha huko mapokezi hivo naomba tutulie  sauti isitoke nje" msamaria wa Miriam alimwambia Miriam kwa kumnong'oneza,
"kwa kweli baba mimi  sipo tayar kulala na wewe maana nilichokimbia huko nilikotoka ni hiki na wewe unataka kunifanyia tena hichohicho hivyo heri nirudi tu" Miriam alijibu kwa hasira huku akisimama na kuanza kuelekea mlangoni ila huyo baba alimshika na kimvutia kitandani na hapo walianza kuvutana huyo baba akitaka kumvua nguo kwa lengo la  kumwingilia kimwili.
                             *******
"Dada samahan mbona sijaelewa kuhusu huu ufunguo ulionipa na chumba ulichoniandikia" Genes alimpata dada wa mapokezi,
"kwani vipi mdogo angu" dada nae alimjibu kwa kumbembeleza mteja,
"huu ufunguo ni wa chumba namba sita ila umeniandika niingie chumba namba tisa,sasa chumba namba tisa  kuna mtu  ila pia kaja mtu  mwingine ambae sijamuelewa hebu fanyeni uchunguzi,
"ahaa kweli mdogo wangu samahani sana nimekumbuka chumba namba tisa  kuna dada mmoja kaletwa hapa na baba yake ila pia huyo baba aliondoka ili huyo binti alale hapa hivyo smahani ngoja nibadilishe chumba hapa niandike namba sita, samahani sana dogo shemeji yako ananichanganya"
"sasa dada kama hicho chumba ni binti yupo huko ndo ujue  kuna mbaba kaingia  huko sasa nendeni mkachunguze maana kila  kukicha naskia vifo kwenye vyumba  vya wageni hivyo huenda hata huyo ni muuaji" Genes aliongea kws msisitizo.
Walinzi waliitwa kuelekea chumba namba tisa ambapo Genes pia aliandamana  nao kushuhudia.
                   ********
"We baba niacheeeeee niache unaninyonga niache nakuambia niache,hata kama ni hela yako uliyonilipia basi kachukue nikalale nje mimi  sihitaji msaada wako" Miriam aliendelea kujitetea ila alizidiwa nguvu na kuvuliwa nguo,
"aliekwambia mjini kuna vitu vya bure ni nani" huyo baba alimwambia Miriam kwa kumkoromea na hapo alikua akimuweka mkao mzuri wa kumwingilia ila kabla hajafanikiwa kuanza kumwingilia kimwili aliskia mlango ukigongwa kwa kishindo,
"Nyie fungueni mlango mbona mnapigana humo ndani,mmeskia hivo vitanda ni uwanja wa mieleka?" Mlinzi aliejulikana kwa jina Chipolo aliongea kwa ukali,
"sinimesema huyu ni muuaji,sikiliza huyo anaelia huko ndani," Genes aliongea kwa kunong'oneza,
"alooo nyie hamfungui niingie na huu mlango ?" mlinzi Chipolo alizidisha mikwara,
"mimi  nataka kufungua ila huyu baba ananishika na kuninyonga hataki nifungue" Miriam aliongea kwa sauti ya juu huku akiwa bado uchi ila alijitahid kufungua  mlango ili aweze kupata msaada,hakujali yupo uchi kabisa hata blauz aliyokua amevaa alivuliwa hivyo mwili wake wote ulikua unaonekana.
Mlango ulifunguliwa na hapo Miriam alijitupa miguuni mwa mlinzi kutaka msaada,
"Hebu binti kwanza kaa pembeni tunamtaka  huyu mhalifu kwanza" mlinzi Chipolo aliongea kwa ukali na kumwamuru Miriam asogee pembeni.
Mhalifu alikamatwa na askari waliitwa na kumtia  mikononi tayar kwa uchunguzi pamoja na Miriam alichukuliwa  kupelekwa kituoni kwa ajili ya uchunguzi.
Genes alipomuona Miriam mazingira yale  alishindwa kuelewa ni kwa namna gani Miriam  kule na kufanyaje ,ingawa mimi ndio nimemwokoa lakini kafuata nini huku,
" basi huyu demu  atakua malaya tu mimi nilijua nimepata demu kumbe kahaba tu anajiuza sasa itakua wamerushana pesa" Genes alijisemea kimoyomoyo huku akifungua chumba alichopewa ili alale,
" kesho asubuhi hata siendi nyumbani ili nikaende shule nitalala hadi saa  mbili asubuhi maana kweli nimekubali usilolijua ni sawa na usiku wa giza"Genes alijiongea kwa sauti hata mtu  angemuoa angedhani anaongea na mtu.
Baada ya dakika ishirini Genes alipitiwa na usingizi.
                           ********
"Yaani kweli Genes ndo mwanaume wakuja kunioa kama ameweza kuniokoa kupatwa na majanga yaleo basi ndio mwanaume nitakaemkabidhi moyo wangu hata kama atakua na maisha ya namna gani, yaani nilikua nishakata tamaa ila mungu mkubwa kanioneshea tena,kazi ni moja tu kesho asubuhi lazima nitamtafuta katika hotel niliyomwacha ili niweze kuongea nae machache pamoja na kumshukuru kwa kuniokoa" Miriam aliwaza  hayo wakiwa njiani kuelekea kituoni kwa ajili ya mahojian na polisi kwani kwa kipindi hicho kulikua na matukio mengi yalikua yakitokea kwenye nyumba za kulala wageni hivyo kesho la polisi lilikua makini kupambana na matukio hayo ili yasiendelee kutokea.
"we mtoto mbona unaonekana mdogo sana na mnakuja kwenye vyumba  vya wageni kutishiana kuuwana?" askari mmoja alimuuliza Miriam wakiwa bado njiani kuelekea kituoni,
"kwa kweli afafande mi mimi cjajauwawana na huhuyu ila yeye ndio alilitaka kunibaka" Miriam alijibu huku akitetemeka kwa woga kwani kitendo cha yeye kukaa na askari wakiume pamoja na mhalifu wake kulimpa wasiwasi wasije mgeuka na kumbaka  tena,
"aha we kama unasema ulikua unabakwa uliingia chumbani kufanyaje?" askari alizidisha swali ila Miriam alipofika kituoni alieleza yote ndo hapo walipowekwa chini ya ulinzi hadi pakuche ambapo ndipo Genes alitakiwa kuitwa kituoni kutoa ushahidi kwani Miriam alisisistiza huyo Genes atafutwe kumbe nia yake ilikua kuja kumuona na kumshukuru na kumuahid panzi la  dhati kwani alimuona kama mkombozi wa maisha yake.
                            ********
"aha saiv saa  kumi na mbili kumbe bado hapajakucha vizur" Genes alijisema pale aliposhtuka na kuangalia saa yake.Alivuta blanketi ila usingizi haukumjia tena zaid ya kuwaza tu kuhusu Miriam,
"lakin huyu mwanamke hivi jana hajalala hapa tena kweli,au  itakua alienda kulala sero na huyu bahasha wake walioshindwana bei, ingawa nilisema nalala mpaka saa  mbili aise silali tena maana anaweza amka tukutane na mimi  sitaki kuonana nae kabisa hata watu wakiona nasalimiana nae watanicheka sana,kumbe ningempa hii misimbazi yangu ningekua natunza mali ya watu pumbavu zake ngoja nitoke  saivi kwanza asije kuniona hapa"Genes alijisemea kimoyomoyo huku akiamka  kuingia bafuni ili aweze kutoka kwani alitokea  kumchukia Miriam ghafla sana hivyo hakutaka hata waonane,
"ngoja niweke hizi hela zangu zilizobaki hapa maana nikienda nazo bafuni zinaweza kulowa na mimi sipendi kutembea na pesa chafuchafu" Genes alijisemea hayo huku akiinua  godoro  na kuweka hapo pochi yake.
                             *******
" jaman wahini  kule hotelin kabla yule Genes hajatoka ili aje kuelezea jinsi alivyoonana na huyu mhalifu alietaka kunibaka" Miriam aliongea kwa ukali kupitia dirishani alipomwona askari akikatiza njia karibu na chumba chake maalumu cha watoto alimohifadhiwa
"we turia mtoto acha mawenge  yako" askari alitoa jibu kwa Miriam,
"kweli yule ataondoka na mtakosa  ushahidi tena jitahidini kuwahi saivi" Miriam alisisitizwa na hapo alisikilizwa na askari waliwasha gari kuelekea hotel Aquline kumtafuta  Genes.
Miriam alifurahi sana kuona Genes atakua nae baada ya muda mfupi ili aweze kumwonesha hisia zake.
                         ******
"Me nilijiuliza kwa nimpe namba ya simu alafu asinitafute kumbe ndo kazi yake hii hadi akasahau kunitafuta,sasa kama jana  yupo na baba yangu kabisa si hatari kabisa yaani mahali wababa wanapita na mimi  nipite? asante mungu kwa kuniepusha na hili janga" Genes aliongea maneno hayo huku akifunga  mlango ili akakabidhi ufunguo mapokezi tayari kuelekea nyumbani.

Itaendelea,

0 comments:

Post a Comment