HATUJA PENDA TUWE HIVI -07

Author

HADITHI,
HATUJAPENDA TUWE HIVI,
SEHEMU YA SABA, (7)
MTUNZI Deo Young Massawe
MAWASILIANO 0769297430.
                    sehemu ya saba (7)
"Mungu naomba upokee roho yangu maana mda mfupi ujao nitakua mbele ya meza ya hukunu" Farid alijisemea huku akijiweka sawa kujirusha ili adokoe bunduki na afanye mauaji,
Baada ya dakika moja na nusu tayari Farid alikua kazungukwa na magaidi kama ishirini kwani alifanikiwa  kudokoa bunduki ila alipojaribu kufyatua alishtukia ndani hapakua na risasi hivyo gaidi aliita  wenzake kwani alishangaa sana kwa kitendo ambacho Farid alitaka  kufanya kwani hakijawahi kutokea kufanywa na mtu yeyote ambae ametekwa,
"huyu alitaka  kuniua  kabisa sema bajati mbaya hapakua na risasi kwenye bunduki yangu" huyo gaidi aliwaelezea wenzake ambao hata wao walishangaa sana kitendo hicho, na kila mmoja aliwaza  nini cha kumfanya  ili awe funzo mbele ya mateka wenzake.
"kwanza huyu sindio nilitaka  kumhasi ila mungu akanijia na kuniambia nisimhasi sasa kama kajaribu  kuua basi Leo utakufa kwa mateso makali  sana"gaidi mmoja nae alisema huku akimshika na kumtundika juu kwa kumfunga  kichwa chini miguu juu, hapo Farid alianza kuteswa kwa kuminywa vipele katika sehemu zake za siri ambapo vilitoa usaha na pia hata mdomoni pia kuliminywa,alipata maumivu makali na alilia  kwa uchungu ila hapakua na msaada,
"hebu leta wembe hapo leo nataka kujua mirija ya mkojo na ya kupitisha shahawa maana nashindwa kuelewa kwa nini kama  ukiwa unaskia  mkojo alafu ukaanza  kufanya mapenzi mkojo hautoki lakini shahawa  hutoka" Farid aliskia maneno hayo kutoka kwa gaidi mmoja na hapo Farid akajua kweli mda wa mateso ndo huo unaaza, na hapo kweli akaona wembe umeletwa.
                           **********
"Sasa Miriam hapa inabidi tuhame maana kodi ya nyumba inaisha na hakuna kazi hapa na siku sio nyingi chakula kitakua  shida" mama mlezi wa Miriam alimwambia Miriam kwani ashamsubiri Farid na Farid mwenyewe haonekanai na kwenye simu hapatikani.
"Basi mimi  utanipa nauli kidogo nirudi nyumbani kwangu maana nimekufanyia kazi mda mrefu" Miriam aliongea kwa huruma sana,
"kwa kweli mwanangu sina hela yoyote kwanza hivi vitu vya ndani inabidi niviuze ili nikarudishe marejesho ya hela  nilizokopa kwa ajili ya ile biashara ambayo ugonjwa wa kipindupindu ulituharibia" mama Miriam alijibu huku akiwa na uso  wa huzuni.
Miriam aliingiwa na hofu ya kukaa bila makao kwani aliamini huyo mama akiuza vitu akimtoroka basi ataishi kwa shida maana tokea aliishi mjini aliweza kuahidiwa kusaidiwa na mtu mmoja tu ambae ni Genes ila kwa wakati huo hakujua kama Genes anamkumbuka,
"ila makosa ni yangu kwani namba ya simu nilipewa ila nikashindwa kuihifadhi,huenda hata saivi angekua kashanipa msaada wa kuenda nyumbani" Miriam alijisemea kimoyo moyo,
"Ila mwanangu usiogope nyumbani utaenda ngoja tutajua namna ya kupata hela jumamosi  ijayo tutauza hivi vitu nilipe madeni  alafu jumapili kuna mahali tutaenda kutafuta pesa usiku je utakua tayari ili upate angalau nauli ?" mama mlezi wake aliongea kwa kumnong'oneza,
"ndio mama nitakua tayari kutafuta hata nauli maana nikizidi kukaa huku nitakufa" nae Miriam alijibu kwa sauti ya upole.
                                   ********
  "Jaman wakubwa naombeni tu msinifanyie ukatili huo heri mniue tu" Farid aliongea kwa unyonge huku akiamwangalia yule alieshika wembe kwa jicho la  huruma kwani tayari uume wake ulianza kuchanwa  mfano wa mtu  anaemenya ndizi ya kupika hakika alipata maumivu makali na alizid kulia kwa uchungu,
"huyo mtu  mbona anawaangalia  kwa huruma hivyo mtoboeni macho kama Samson alivyofanyiwa" gaid mmoja alisema maneno hayo ambayo Farid aliyaskia kwa makini na hapo alishuhudia kisu kikija  karibu na jicho la  kushoto na baada ya sekunde mbili jicho lilikua lishaharibiwa na hapo alishuhudia tena kisu kikikarbia  jicho lake la kulia na baada ya sekunde mbili alikua kipofu alibaki kuskia sauti tu,
"sasa umekua Samson ila hutafanikiwa kufa na watu wengi unakufa mwenyewe" Farid aliskia maneno hayo kutoka kwa gaidi mmoja.
Farid aliteswa sana kwani alichanwa sehemu mbali mbali za mwili kwani kila alietaka kujua kiungo cha binadamu basi aliruhusiwa kuchunguza kwa Farid.
Damu ilianza kumuisha na hapo alianza kulegea kwa hakuweza kuomba msaada kwa mikono tena na hapo moto uliwashwa chini na akaungua  hadi kukata roho.
Hicho kilikua  kitendo kibaya kushuhudiwa kwani vijana wengi wa Afrika kutokana na ukosefu wa ajira walikua wakijiunga na makundi mbalimbali ya kigaidi ili kujipatia kipato ila kwa kikundi cha Mai-Mai basi vijana waliojiunga huko kwa kuahidiwa pesa nyingi walipoona  kitendo alichofanyiwa Farid asie na kosa basi waliogopa kuendelea na mafunzo waliyokua  wakipewa na walipojaribu  kutoroka basi walikamatwa na kuuawa kwani wengine walikua na nia ya kuja kutoa taarifa ya makundi yanayotafuta vijana hasa kwenye mitandao ya kijamii ila hakuna aliefanikiwa  kutoroka mzima,
"ningejua  nisingekubali kujiunga na hiki kikundi  cha kigaidi kama mambo wanayofanyia  watu ndo haya basi" yalikua maneno ya kijana mmoja aliekua anajaribu  kukwepa mishale  pale alipoonekana akitoroka kwenye mafunzo huko msituni ingawa nae aliuwa kikatili kwa kwa kukatwa  kichwa kwani haikuwezekana kwa mtu  kutoroka maana angeenda kutoa siri .
                                *******
"Weekend (mwisho wa wiki) hii nitaenda kwa Miriam liwalo na liwe sitaogopa tena lazima nikamwone mke wangu hawezi kuniumiza  kichwa changu hivi" Genes alijisemea moyoni. Alipanga safari ya kuenda kumuona Miriam ila kwa kuogopa kuenda kupigwa tena basi aliamua kukaa chini na kuandika barua  ambayo alipanga kuenda nayo ili ampe Miriam na kukimbia hivyo jumatano usiku alijifungia chumbani na kuanza kuandika barua,
"yaani leo  ndo siku ya kuandika mashairi  yenye degree na mwandiko ulioenda  shule tena leo ndo natumia ule mwandiko wa kufanyia mtihani wa taifa" Genes alijisemea huku akijiweka sawa na  kuanza kuandika,

Dear,Miriam.
Natumai unaedelea vizuri mpenzi wangu Miriam,mimi  tokea ile siku nimekuja kwako ndo nikapigwa na mama yako hadi leo nimekua silali wala sili chakula kwa ajili yako hata shuleni  siwezi tena  kusoma kwani nakupenda sana na wewe umekataa kunipenda,sasa naomba nikuambie tena nakupenda sana naomba nikubalie nitakupa pesa kwa sababu baba yangu ni tajiri na mama yangu ni tajiri.Hata usiku nakuona ndotoni unanijia hadi natamani kukugusa mwili wako ila nashtuka,hivyo naomba tu unikubalie niwe mpenzi wako ili niwe na raha maana hata saivi nilikunywa maji kwenye glasi nikakuona sasa nateseka sana moyoni,Miriam ukinikubalia nitakuja kulala na wewe nikufanyie kama wafanyavyo wacheza tamthiliya za kifilipino kwani nafurahi sana pale wanapokumbatiana  na kutomasana sehemu mbali mbali za mwili huku wakipigana mabusu kila mahali.Miriam naomba nikubalie jaman ila kama hutakubali basi usinichukie kwani bado nina nia ya kukusaidia  kurudi nyumbani.Ukimaliza majibu yaandike nitakuja siku ingine hapa ndo unipe au unitafute kwenye namba ile ya simu niliyokupa natumai unayo.Nakupenda sana Miriam I LOVE YOU Mwaaaah.
Wako nikupendae,
Genes.
Baada ya kumaliza kuandika Ali tafuta bahasha ya kaki akaiweka na hapo hakutaka kuipeleaka tupu aliingia  chumbani kwa mama yake ambapo aliinua godoro  na kuchukua noti saba za elfu kumi kumi ambazo alizimbatanisha na barua na kuziweka Kwenye bahasha,
"aah mama hatajua bhana maana hizi noti zipo nyingi hapa" Genes alijisemea kwani mama yake alikua na tabia ya kuhifadhi pesa ndani.
Baada ya kuifunga  bahasha vizuri aliinua godoro na kuiweka  tayar kusubiri  jumamosi  ili aende nayo kwa Miriam.
                                ****
"We Miriam amka tuanze kuandaa mazingira ya kuondoka hapa" mama mlezi wa Mirian alimwamsha Miriam ili waweze kuandaa vitu kwani vitu vyandani  vilikua  vinapelekwa kwenye mnada, wote walishirikiana kusafisha  mazingira hayo ili waache nyumba ya watu ikiwa safi,
"sasa mama nitapata wapi hiyo pesa kesho" Miriam aliuliza kwani alishindwa kujua hela itapatikana wapi siku hiyo ya jumapili wakati vitu vinauzwa jumamosi.
"we nishakwambia kesho usiku kuna mahali nitakupeleka na pesa itapatikana tena kwa wewe itapatikana haraka na utaenda kwenu" mama Miriam aliongea kwa hasira hadi Miriam akaogopa na kukaa kimya.
                                *******
Genes aliamka asubuhi na mapema ila akajisema "leo  jumamosi sitoki nyumbani kabisa hadi kesho jumapili ndo nitaenda kwa Miriam" hivyo alirud  kitandani na kuendelea kulala kwa kukusanya nguvu za jumapili hiyo.
                                 *******
  Mama Miriam na Miriam waliuza kila kitu katika nyumba yao na kulipa  madeni  yote hivyo wakabaki mifuko  mitupu na wakapewa nafasi ya kulala kwa usiku huo wa jumamosi ili jumapili asubuhi waondoke.
Asubuhi hiyo ya jumapili waliamka asubuhi na mapema na hapo Miriam alizid kushangaa ni wapi pesa zinaenda kupatikana
"kwani mbona naambiwa nivae  chupi nzuri nakupuliziwa marashi  na mbona navalishwa nguo fupi kama za mtoto" Miriam alijiuliza maswali hayo bila kupata majibu na hapo walianza safari ila Miriam hakuelewa wanaelekea wapi kwani ilikua ni jumapili mida ya saa  nne  asubuhi.
Mama Miriam alimpeleka Miriam katika bar moja iliyokua Kaloleni ambapo ilisifika kwa wanawake kujiuza na hapo alikaa na kumwagizia soda. Hadi kufika saa  tisa  mama Miriam alikua ashapokea oda tatu za wanaume wakimtaka  Miriam,
"hapa lazima nipate hata elfu 40 nimpe hapo 20 za nauli" alijisemea mama Miriam akisubiria usiku ufike ambapo ndo wanaume hao walikua wameahidi kuja.
                            ********
"Yaani hapa nipo tokea saa  tano na saivi ni saa  tisa huyu Miriam kaenda wapi sasa alafu sijui itakua wamehama hapa mbona pako  ovyo hivi hata zile meza hakuna tena" Genes alijisemea huku akiwa kachoka kwa machungu ya kumkosa Miriam,
"yaani narud na hii barua niliyoiandika kwa ustadi hivi" Genes aliendelea kujisemea,
"ila kwa kua nimeaga naenda shangazi basi sirudi nyumbani naenda kutafuta gesti huko mjini nilale huko nitumie hii pesa" Genes aliongea huku akitoa ile bahasha na kuchana ile barua na kuweka pesa yake mfukoni akapanda daladala kuelekea katikati ya mji kutumia pesa.
                                 *******
"Mama huyu ni nani?" Miriam aliuuliza alipoona mama yake mlezi akipokea hela kisha kumkabidhi kwa mwanaume  ambae tena alikua mlevi sana,
"we nenda nae" mama Miriam alimjibu Miriam.
Ila Miriam tayar aligundua yale mazingira ni ya wanawake kuuzia  mwili kwani kila mwanamke aliyeonekana maeneo yale  alikua kavaa  nusu uchi.
Miriam alichoropoka katikati yao na akatokomea gizani.
"acha nikafie sehemu ingine na sio hapa" Miriam alijisemea huku akikimbia kuelekea asipokujua tena usiku wa saa  mbili.
"Bila shaka hapa ni kituo cha mabasi" Miriam alijisemea pale alipoona mabasi yaliyojipanga na mengine kuingia na kutoka.
"Shkamoo baba naomba msaada wako" Miriam alimfuata baba mmoja na kumsemesha
"msaada gani binti" huyo mbaba alimjibu kwa uso wa huruma,
"kuna mama yangu alikua ananiuza ila nimemtoroka na hapa sina kiasi chochote cha pesa na nahitaji kufika kwetu kwa hiyo naomba unisaidie,
"sawa binti  nitakusaidia mahali pa kulala" huyo baba alimjibu kwa uso  wa huzuni ila moyoni akiwa na furaha kwani alijua siku hiyo kapata binti mzur tena mdogo wa kulala nae.
"Twende nikupeleke mahali ukalale" huyo baba aliongea huku akitembea kuelekea hotel Aquline iliyokua karibu na kituo kikuu cha mabasi ambapo ambapo alipanga kumchukilia chumba kisha badae aje kumfuata huko.
"Dada kuna chumba hapa nataka huyu binti alale hapa",
"ndio chumba namba tisa",
"nashukuru sana ngoja nimpeleke huyu binti"
Yalikua mazungumzo kati ya dada  wa mapokezi na baba aliyejitolea kumsaidia  Miriam na hapo Miriam aliingizwa  chumba namba tisa  ila huyo baba akamsihi asifunge mlango kwani atatuma chakula kiletwe,hapo alidanganya kwani alitaka  akaage nyumbani kua ampata safari kisha kurudi huko na bila kupinga  Miriam aliacha mlango wazi kwa  kuurudishia huku akimshukuru mungu kwa kupata msaada.
                             ********
"Sasa mda wa kulala umefika ngoja nitafute pakulala ila sijaamini kama ndo Miriam sitamuona  tena" Genes alijisemea huku akimfuata  dereva boda  boda na kumuuliza
"Vipi broh,hapa wapi nitapata chumba cha kulala?"
"Hapa karibu ni hapo Hotel Aquline arifu,nipe buku langu nikurushe hapo fasta" dereva boda boda aliwasha pikipiki na kuelekea hotel Aquline.
"dada  vipi chumba nitapata"?
" ndio lipia chumba namba tisa"
Genes alikua tayari Kwenye lifti akienda  chumba namba tisa  kama alivyoambiwa ila ghafla alichunguza ufunguo aliopewa
"huyu dada nae vipi mbona ameniagizia chumba namba tisa ila ufunguo huu ni wa chumba namba sita ?" Genes alijiuliza  swali hilo akiwa mlangoni wa chumba namba tisa  ambapo ndipo Miriam alikua ndani  akisubiria chakula ale ndo alale hivyo kwa mda huo alikua kajilaza na mgongo  akiendelea kumshukuru mungu kwa kumuepusha na yule mama.
"Ila huyu dada itakua kachangaya funguo ngoja niangalie hiki namba tisa  mbona hakijajifunga vizuri huenda kipo wazi" Genes alijisemea huku akisukuma mlango wa chumba namba tisa..

Itaendelea....

0 comments:

Post a Comment