HADITHI,,,,
HATUJAPENDA TUWE HIVI,
SEHEMU YA KWANZA (1),
MTUNZI Deo Young Massawe
MAWASILIANO 0769297430
sehemu ya kwanza (1)
Ilikua siku ya tarehe 6 mwezi wa pili,siku hiyo kwa wanafunzi katika shule mbalimbali walifanya maadhimisho ya kupinga vitendo vya unyanayasaji wa wanawake hasa kitendo cha ukeketaji kwani tarehe hiyo ndo ilikua maalumu duniani kote.
Katika shule moja ya msingi iliyopo Tengeru mkoani Arusha basi kulifanyika maandamano ya wanafunzi huku wanafunzi wakishika mabango yenye maandishi mbalia mbali ya kukataa vitendo hivyo.
Katika maandamano hayo kulikua na mwanafunzi aitwae Genes aliekua darasa la saba, nae alikua kiongozi wa maandamano hayo yaliyokua yanaanzia Tengeru hadi uwanja wa sheikh Abed uliopakana na kituo kikuu cha mabasi ya mkoani.
Walipofika maeneo ya Sanawari basi wanafunzi wote walisikitika kumuona msichana anaeshangaa maandamano huku akilia kwa sauti ila hawakujua analia kwa sababu gani,Genes alipomchunguza aligundua ni msaidizi wa kuuza vyakula kwa mamalishe kwani alisimama pembeni ya viombo na mwenyewe alibeba vikombe na maji,
"huyu mtoto mzuri mbona analia mwenyewe,? ngoja siku nikija mjini nitampitia hapa nikuulize maana ni mzuri sana " Genes alikua tayari kashaanza kutamani wanawake kwani ndipo alifika umri wa kabalehe kwa hiyo alisemea tena
"nakuja kuongea nae tu na kigezo ni hiki hiki kumuuliza kwa nini ulikua unalia? na lazima ataongea na mimi maana huku shuleni nikiongea na akina asha wananambia bado sijakua mara sijui kaoge" alijisemea huku akiendelea kuongoza kundi la wanafunzi wenzake kuelekea Uwanja wa Sheikh Abeid,
Baada ya ule msafara kupita eneo lile la Sanawari alipokua analia mtoto wa kike mama mmoja alifoka,
"we Miriam nakufukuza kazi sasa hivi, nakwambia osha vikombe nawe unaanza kulia hebu fanya kazi wewe huoni kama nakulea kama mama yako" aliongea mama huyo mbele ya huyo msichana wa kike aitwae Miriam na hapo Miriam alijikaza na kuendelea na kazi zake huku akiomba mungu aendelee kumpigania hadi siku ya mwisho kwani aliishi maisha ya mateso na alilkua mtu kulia mara kwa mara ingawa hata mama aliyekua anaishi nae hakujua sababu ya Miriam kulia ovyo na mama huyo hakuwahi kimbembeleza kujua kinachomliza mara kwa mara labda kutokana na kua sio mama yake.
Jioni ilifika na wanafunzi wa shule ya akina Genes walikua tena katika maandamano ya kurudi kurud shuleni na hapo Genes alikaa makini kuangalia sehemu aliyopo yule msichana,
"nataka nimuone huyu mdada tena kama atakua amenyamaza" alijisemea moyoni.
Kwa mbali alimuona na ghafla akamshuhudia tena kaanza kulia na mbaya zaidi alimuona mama alietoka na mwiko na kumpiga kichwani huku akiambatanisha na maneno makali ambayo yalimsikitisha Genes
"pumbavu zako we mtoto wa kike ina maana ukiona watoto wa shule unaanza kulia hapa kazini kwangu umekuja kulilia shule au umekuja kufanya kazi? ebooooh kama ungetaka kusoma shule ungebaki kwenu usome shenzi wewe peleka wateja maji ya kunawa mikono na saiv nitakufumua futikaaaaaa!" alifoka sana mama huyo nao wanafunzi kama kawaida wakiona mtu anapigwa walianza makelele,
"oyoooooo,!! weeweee!! hasira za mumeo usimtolee mfanyakazi wako weeweeee" walicheka sana na kufurahia ila Genes pekee alidondosha chozi kuona jinsi msichana mdogo kama yule anavyoteseka kwani ingebidi mda huo awe shule.
Usiku huo Miriam alilala huku akiwa na mawazo sana kwani alijiona kama sio mtu huku duniani kwa mateso aliyokua anapata alifkiria maisha aliyopitia tokea akiwa mtoto na alifikiria kitendo kilichomfanya awe mazingira yale kwa mda ule na kuona kweli amepitia mengi,
"sasa nitateseka hivi hadi lini, heri ningebaki nyumbani tu nikakubaliana na ile hali iliyojitokeza ila huku nafanyishwa kazi ngumu huku nikiteswa kiasi hiki ni bora ningekubaliana na ile hali ya kule nyumbani" alijisemea Miriam huku akikumbuka yaliyomtokea maishani mwake hadi yeye kuwa mazingira yale hivyo kutoa machozi kwake ilikua sawa na mtoto wa tajiri kutabasamu aonapo wazazi wamemletea zawadi.
Genes nae usiku kama kawaida kitanda kimoja na mtoto wa Mjomba wake aitwae Dany hivyo alilala huku akiwaza kwa nini yule msichana aliwaona akalia na alitamani sana kujua kwa nini na pia alimtamani hadi awe mpenzi wake, alipotelea usingizini huku mawazo yakiwa kwa yule msichana. Mwendo wa saa kumi na moja asubuhi Dany aliamka kukojoa katika kopo lilokua mvunguni na kurudi kulala ila kabla ya kupotelea usingizini aliskia Genes akiwa anaongea ndotoni ila aliskia maneno yake tu nayo yalikua hivi
"jaman mbona mchana ulilia hapa ulipigwa na mama yako kwani umemfanyaje ??"
"aah unadanganya sasa we umenionaje kwenye kundi la watu wengi vile na ukiniona sasa unalia ?"
"me nilikupenda sana na nikasema nitakuja kukubembeleza ndo mana leo nikaja hivyo tusogee hapo nyuma ili mama yako asije kunipiga mwiko"
"sogea basi nikusalimie kwa busu kwani wewe huangalii tamthiliya za wazungu wanavyosalimiana"
usinishike kidudu changu jaman naskia mkojo wa ghafla achia huko toa mkono wako nitakukojolea ondoaaa"
Dany aliogopa kusikia kaka yake anataka kukojoa kitandani hivyo akaamua kumshtua.
Genes alishtuka na kumkumbuka mwalimu wake wa darasa la tano wa sayansi alivyowafundisha kuhusu kubalehe na kuota ndoto pevu ambazo huja wakati asubuhi,
"kweli mwalimu hakudanganya" Genes aliongea huku akikagua nguo yake ya ndani na kuikuta imechafuka.
Dany yeye alikua hajui chochote kwani alikua anasoma darasa la tatu.
"hakika huyu mwanamke lazima nitamtafuta tu aniambie sababu za kulia na kama ni msaada nitampa maana kaniotesha ndoto tamu huyu Dany hata amenishtua wa nini angeniacha nimalize hata kumpigia busu" alijisemea Genes huku akijiandaa na shule na siku hiyo ilikua ijumaa na jumamosi ndio alipanga kuenda kwa msichana aliemwotesha ndoto nzuri na tamu,
"hii ndoto itakua Kweli tu siku moja ngoja kesho nimuibukie pale anapokaa ila sasa huyo mama yake hatanitoa na mwiko kweli ? ila me ndio chali ya Arusha naweza kukuibia soksi bila ya kukuvua viatu au kukuvua shati kabla ya koti" hakika Genes alipagawa ghafla kwa huyo binti hivyo alienda shule kisha jioni alirudi nyumbani mawazo yote yakiwa kwa huyo binti na kabla ya kulala akamuonya Dany,
"we Dany siku ukiskia naongea usiku usinistue tena"
"apana kaka niliogopa usije kukojoa kitandani maana niliskia unasema unakojoa" Dany alijibu
"hata nikikojoa kwani we unafua mashuka ?we usiniamshe tena"
Wote walilala huku Genes akiomba mungu aote tena ndoto ya usiku uliopita.
Usiku huo ulikua zamu ya Miriam kuota jinsi alivyolia mbele ya wanafunzi waliopita barabarani na aliota akisema hivi,
"we hapo mbona wenzako wananicheka na wewe unanililia au unanionea huruma?"
"njoo nkupe mkono wa hongera"
Miriam aliota akitamka maneno hayo ila alipotaka kunyoosha mkono basi aligusa ukuta na hapo akashtuka kwani alilala akiwaza kitendo kila na hapo sura ya Genes ilikua kichwani mwake..
Asubuhi ya tarehe 8 mwezi huo wa pili palikucha vizur na hali ya barid ilizoeleka katika jiji la arusha ila kwa Miriam kukaa jikoni mda mrefu alipenda kuvaa nguo nyepesi zilizoonesha chuchu kuchomoza kama mkuki ikilinganishwa ndio kipindi alivunja ungo. Wateja wakiume waliokuja kula chakula kwake walimtania kwa kusema
"ziwa konzi mama kila saa ni saa sita je ukikua kidogo hatutauana kweli?".
Maneno hayo yalimfanya Miriam awe anacheka cheka na kukimbia kuogopa mtu asimguse maana kila alipokua anaosha mteja wa kiume basi mteja hufanya kumgusa kwa mbali kitu kinachofanya aruke kama chura na anapomwaga maji basi mama mlezi wake humgombeza kwani pia mama aliona wivu kwa kila mwanaume kumtamani mtoto huyo,
" yani kila mwanaume anamuona tu huyu mtoto ambae hajui hata kufua chupi na mimi mama lao nikiwa hapa?".
Jumamosi hiyo Genes aliamka mapema akavaa zake ambazo Dany ndo alifanya kazi ya kumwambia umependeza au la hivyo alibadili nguo hadi pale alipojiona ametoka bomba,
"huyu mtoto lazima anisikilize tu" aliongea Genes huku akitinga kofia yake na kuondoka hakika kwa uvaaji wake basi hakua mtindo wa mwanafunzi kwani alivaa suruali ya kubana na viatu vikubwa akawa anatembea kama mwanapolo alietoka Mererani kukagua migodi ya Tanzanite akapanda daladala ya kuelekea Sanawari....
Itaendelea
0 comments:
Post a Comment