HATUJA PENDA TUWE HIVI-02

Author

HADITHI,
HATUJAPENDA TUWE HIVI,
SEHEMU YA PILI (2),
MTUNZI Deo Young Massawe
MAWASILIANO .0769297430  
                     
  "Sasa nitaanzaje na huyu demu maana kaniingia ghafla sana hebu kwanza niandae mistari nisiende kuaibika" Genes alijisemea akiwa ndani ya daladala tena siti ya mwisho,
"kwanza nitaanza kuagiza chai ili niweze kukaa eneo lile,alafu nikinywa nitaomba maji ya kunywa,ila sasa na hivi nilivyovaa nikiomba maji kwa mamalishe sintachekwa? ila mimi mtoto wa mjini bhana hapa ni kutumia akili tu" Genes aliendelea kuwaza mwenyewe huku akijipanga kuenda kumwona  binti aliyemuona siku moja na kumpenda.
                             *********
  Miriam alikua akiendelea na kazi na wakati huo alikua anakata kitunguu kwani ilikua mida ya kutengeneza kachumari kwa wale waliokua n uwezo wa kunywa supu asubuhi.
"we Miriam hadi nikupige  pige ndo unaniskia nishakwambia uwe unakaribisha mteja sasa huyo mteja nimemuona amesimama hapo nje kwa mda na wewe upo tu" aliongea mama mlezi wa Miriam
"nisamehe mama cjamwona" Miriam alijibu huku akiangalia mlangoni,hapo alimwona kijana alievaa vizuri sana hadi mwenyewe akajiuliza "mbona tangia  nimekuja hapa cjawahi hudumia  mteja aliependeza hivi" hapo alimwonesha sehemu ya kukaa nae akakaa huku akiufunika uso wake  wake kwa kofia  na miwani kubwa basi hapo Miriam akahisi ni mtoto wa mkuu wa mkoa.
"nikuhudumie nini kaka" Miriam aliuliza kwa lugha ya kumbembeleza  mteja,
"nipe maziwa na chapati moja laini ya moto kiasi" Genes alijibu kwa sauti ya upole  hadi Miriam akafurahi kumhudumia  mteja mstarabu na msafi asiependa uchokozi kama wengine walivyokua wanamchokoza,
"alafu huyu ni mtoto mdogo tu sasa itakua katoa wapi pesa za kununua nguo nzuri kama hizi?" Miriam alijuuliza huku akimmiminia maziwa.
"we Miriam nataka nitoke kidogo nafika hapo Ngaramtoni kutoa oda ya nyama na maziwa   nakurudi hakikisha shughuli za hapa zinaenda vizur" mama mlezi wa Miriam aliaga akabaki Miriam na baadhi ya wateja walioingia kabla ya Genes hivo nawao  wangeondoka kabla Genes.
"afadhali huyu mama kaondoka sasa lazima niongee nae vizur tena huko anakoenda harudi mapema" alijisemea Genes.
Mama kuondoka pale shughuli kwa Miriam zilikua  nyingi hivyo alihangaika huku na huko,
Licha ya watu wote kuondoka na Genes kubaki tu na Miriam pale aliogopa kuongea kitu ila kwa bahati mbaya Miriam alimwagikiwa na mafuta yaliyokua yakikaanga mapaja ya kuku na hapo Genes alihitajika kumpa msaada kwani Miriam alipiga kelele za uchungu maana aliungua miguuni  kuanzia magotini,Genes aliinuka na kumfuata haraka
"hapana usinishike kaka nitakuchafua alafu mama yangu akija atanifukuza kazi we endelea kunywa tu chai yako" Miriam aliongea huku akijirusha kukataa msaada wa Genes,lakini Genes licha  ya kukataliwa masaada alifungua kabati na kwa haraka alitoa yai  bichi  na kulipasua kisha kumpaka kama huduma ya kwanza..
  "jaman angalia ukijichafua mama yangu akija akiniona ukinisaidia basi atanipiga naomba uniache tu chukua sabuni hapo unawe mikono" Miriam alimwambia Genes huku akiwa bado na maumivu,
"hakuna shida hata nikichafuka nitanawa tu kwani afya yako ni muhimu sana,kwani huyu nj mama yako au ni nani kwako sikaaga kuenda Ngaramtoni ?" Genes nae aliongea kwa mfumo  wa maswali,
"huyu mama ni historia ndefu imenifanya niwe nae" Miriam aliongea kwa upole huku machoz yakianza kumtoka upya,
"hebu niambie kwa kifupi maana leo sio mara ya kwanza kukuona,pia kwa leo  nilikuja hapa ili kuzungumza na wewe maana juzi tulipita hapa wanafunzi wengi nikakuona unalia ndo leo nikapanga nije kukuona na kukuuliza sababu ya kulia" Genes aliongea kwa sauti ya kubembeleza
"hebu vua kofia yako" Miriam aliongea kwa mshtuko huku akivuta kumbukumbu ya sura ya kundi la wanafunzi waliokua wanaandamana ambapo kuna mmoja aliemuonea huruma ambapo pia alimuota usiku huo,
"ha kumbe nini wewe hata hufananii mwanafunzi jaman umependeza sana" Miriam aliongea huku akiwa na aibu kwani hakutarajia kama angekua  yule mwanafunzi ambae ashwahi muona akipigwa na mwiko,
"asante sana ingawa sijapendeza,ondoa mikono machoni basi Miriam kwani siushapona simama ukae hapa unambie kwa nini ulikua unalia juzi maana mimi  sikufurahi hata kidogo" Genes aliongea huku akimwinua Miriam na kumkalisha kwenye kiti,
"mimi  nimekwambia ni historia ndefu sana,sasa hata nikikuelezea wewe huwezi nisaidia" Miriam alijibu kwa unyonge.
"we nieleze tu hata kwa kifupi alf  tuangalie namna ya kukusaidia kwani nitaongea na baba yangu akisaidie" Genes aliongea kwa huruma na hapo Miriam alipata moyo wa kumuelezea kwa kifupi,
"ngoja tukae basi hapa vizuri nikuelezee japo kwa kifupi ili niweze kuendelea na kazi zangu maana mama akija atanichapa" Miriam alisema
"we nielezee tu maana mama yako huyu hatarudi mapema sababu Ngaramtoni ni mbali kidogo kutoka hapa" Genes alimuelewesha Miriam umbali wa pale Sanawari na Ngaramtoni na hapo ndipo Miriam akaamini mama hatarudi mapema hivyo alizima majiko  yote tayari kwa kuongea,hivyo walikaa kwenye kiti kikubwa cha wateja na hapo ndipo Miriam alianza kumuhadithia.
                                ********
  Katika barabara ya kutoka Sanawari kuekekea  Ngaramtoni mama mlezi wa Miriam alipanda daladala ambapo alikaa kiti cha dirishani kwa huku akiongea  na mtu  kwenye simu,
"Sasa hapa nipo kwenye daladala  mataa ya Mianzini, naomba uwe makini kunisubiria kwa simu  maana mwenyewe............" kwa bahati mbaya kumbe aliongea na simu huku kioo cha gari kikiwa  wazi hivyo simu yake ikawa imedokolewa na vijana waliokua wanatega maeneo yenye foleni  hasa hasa kweye  taa za barabarani, hapo hapo mama hakua na sababu ya kuendelea na safari tena kwani alikua anaenda kuonana na mtu ambae wamejuana tu kwenye simu na alimfuata kufanya nae ngono ili aweze kujiingizia kipato kwani kazi yake ya kuuza chakula haikukidhi mahitaji  yake kutokana na kunyanyaswa na viongozi wa jiji na manispaa.
Alishuka kwenye gari na kuvuka  upande wa pili kupanda daladala  ya kuenda Sanawari,
"huyu binti nimemuaga naenda kuchukua nyama sasa narudi  bila simu hakika mungu hapendi haya mambo ya kujiuza" Mama mlezi wa Miriam aliongea huku akizipongeza sehemu zake za siri kwa kuponea chupuchupu kwa siku hiyo na hapo akapata fundisho  la  kuongea na simu pindi awapo kwenye gari,
"twende twende twende Sanawari Maji ya chai Tengeru hadi USA tunafika  panda mama malizia siti moja hapo twende twende mama ingia na viatu" yalikua maneno ya konda ambapo mama Miriam akipanda daladala hiyo,
"huyu mtoto sijui nitaeda kumkuta  kaunguza au kaepua kibichi alisema mama huku akiwa kakunja uso  kwa hasira.
                               **********
"kwa kifupi mimi  naitwa  Maria Lizery, nilizaliwa Manyara,na kuanza kusoma huko huko ila nilipofikia darasa la  nne nilikimbia  nyumbani kwa kuogopa kufanyiwa  tohara yaani walitaka  kunifanyia mila ya kumkeketa mwanamke lakini nilikichukia sana kitendo hicho ambacho dada yangu alifanyiwa ila kwa bahati mbaya akavuja damu hadi akafa,pamoja na kitendo hicho kulikua na mbaba aliekuja  kwetu kuniandaa kua mke wake ndio maana niliamua kukimbia na kuja hapa Arusha mjini kukwepa mila hizo, najuzi mlipopita hapa na mabango yenu nililia  sana hadi usiku nilikuota  kwa kitendo chako cha kunionea huruma  klinifariji sana sababu tokea naishi  mimi sijawahi onewa huruma na mtu  zaidi ya kuchekwa na kila mtu" Miriam alishindwa kuendelea na maongezi akajikuta anainama chini akilia machozi.
"sawa Miriam usiogope nitakusaidia kwani kuna shirika la  afya linaitwa WHO (world Heath organization) na lilituma mwakilishi wake alietuachia namba zake za simu katika tamasha la  juzi sasa nitawasiliana nae aweze kunisaidia usiteseke tena kwani alipinga  sana kitendo cha ukeketaji kwani huhatarisha sana maisha yako" Genes aliongea kwa huruma sana akilengwa lengwa na machozi kwa kujua tatizo la  msichana yule ila pia alifurahi kusikia Miriam kamuota usiku kama yeye pia alivyomuota. Waliendelea kuongea hadi Miriam akajisahau kuendelea na kazi.
                                ********
"We mama vipi tunaenda ofisini haupo mbona unatukalisha na njaa?" aliongea kijana mmoja alipokutana na mama Miriam
"kwani msichana wangu hayupo hapo ? nilieda  hapo Mianzini kwa haraka ila mbona ofisini msichana nimemwacha!?" alijibu mama Miriam kwa mshangao,
"msichana wako  wako yupo ndio ila yupo na kisharo fulani  hivi wanapiga stori namuuliza ugali upo anasema mama hayupo eti,kijana mwenyewe ni mdogo tu ila anampapasa miguu" huyo kijana alimueleza mama Miriam.Kumbe wakati huyo mteja anaenda ndipo Genes alikua anampaka Marian yai  bichi.
"haa anapapaswa miguu ?hebu twende nikamuone huyo mwanaume mwenye jeuri ya kucheza na binti angu ina  maana nae huyu binti anaanza kunizibia riziki  zangu? huyo mwanaume angekuja kupapasa hii yangu iliyoshiba" alifoka mama Miriam huku akiongeza mwendo kwani alikasirika zaidi ukizingatia kaibiwa simu.........

0 comments:

Post a Comment