PRISCA-17

Author
PRISCA
SEHEMU YA KUMI NA SABA

ILIPOISHIA

Yule daktari aliinuka pale kwenye kiti na kwenda kwenye kabati la mafile ili achukue file la mama yangu, macho yalinitoka baada ya kuona kitu kilichonishangaza sana kutoka kwa Yule daktari. Yule daktari alikuwa na ile nembo waliyokuwa nayo magaidi katika shingo yake

“nimekwishaaa” nilijisemea

SONGA NAYO

Nilibaki kumuangalia yule daktari kwani alishaanza kunitisha na ile alama aliyokuwa nayo mwilini mwake, niliaza kutafuta mbinu ya kumtoroka yule daktari bila hata kushtukia, ghafla nilishangaa yule daktari akinigeukia kama mwanajeshi aliyeambiwa nyuma geuka

"kijana wala usiogope mimi nipo pamoja na wewe kwani hawa jamaa wamenitesa sana mpaka kufikia hapa" daktari alisema

Nilishangaa kusikia yule daktari akizungumza maneno yale huku jasho likimtoka na mishipa ya hasira ikimsimama, daktari akaendelea kuongea kwa uchungu sana

"kijana mtandao unaokutafuta wewe ni mkubwa sana na kuuepuka ni vigumu sana, ndani ya mtandao huo kuna baadhi ya viongozi wa serikali ambao mnawaheshimu sana katika nchi hii, mimi niliingizwa katika kundi ili ili niweze kuwasaidia katika mipango yao ambayo inatokea katika misheni zao" daktari aliendelea

"Labda ikitokea wamempiga mtu risasi na kufikishwa hospitali wao walikuwa wananipa kazi ya kummalizia na ninaposema hapa nilitumwa kuja kummaliza mama yako ila kuna kitu kilichofanya mpaka nisimuue" daktari alisema

"kitu gani daktari?" niliuliza

"wewe ndiyo umefanikiwa kupata siri zote za wale jamaa na mimi nilikuwa nazitafuta ili nizifikishe mahali panapohusika ili watuhumiwa wote wakamatwe najua ni ngumu sana kujua wapi ni sehemu salama ila kwa mbinu fulani tunaweza kujua" daktari alisema

"mbinu gani hizo?" niliuliza

"wewe inatakiwa ubadilishwe sura ili usifahamike" daktari alisema

"sasa nitabadilishaje daktari?" niliuliza

"hiyo kazi niachie mimi,ila sidhani kama nina muda mrefu wa kuishi duniani" alisema

"kwanini unasema hivyo daktari?" niliuliza

"usijali nitakuambia pindi tutakapoenda nyumbani kwangu kwani hapa hakuna usalama" alisema

"sawa daktari" nilisema

Niliamua kutoka nje ili niende kwenye wodi aliyolala mama nimjulie hali jampo kidogo nilifika kwenye kitanda alicholala mama nikakuta anaendelea vizuri huku akiwa amefumbua macho na kuchezesha mdomo japo kidogo

"shikamoo mama" nilimwamkia

"marahaba mwanangu" alijibu

"vipi unaendeleaje mama?" nilimuuliza

"naendelea vizri mwanangu ila nashukuru sana kwa kunisaidia mpaka kufika hapa hospitali, kwani nilikuwa naogopa kufa bila kukuambia maneneo ya mwishi mwanangu" mama alisema huku akiniangalia kwa huruma sana

Machozi yalianza kunibubujika kila nikiangalia sura ya mama liyojaa huzuni, kichwani nilikuwa natafakari ni maeneo gani mama alikuwa anataka kuniambia, nilikaa vizuri ili nimsikilize mama alikuwa anataka kusema nini

"mama naomba uniambie" nilisema

"mwanangu naomba uwe jasiri kwa aya nitakayokuambia" mama aliema huku machozi yakimtoka

"naomba uniambie mama" nilisema

"David mimi siyo mama yako mzazi ila mimi ni mama yako mdogo na yule baba uliyemuona huko kwenye kundi la majambazi ndiyo baba yako mzazi ila alimuua mama yako wakati wewe upo mtoto wala hujielewi baada ya mama yako kugundua kwamba ameshafahamu kazi yake ya ugaidi, mwanangu mimi niliambiwa pindi nitakapoongea kitu chochote nitakuwa hatarini na ndiyo maana nilinyamaza" mama alisema

Jasho llianza kunitoka baada ya kugundua kwamba yule siyo mama yangu mzazi, hasira zilinipanda mwilini huku nikitetemeka kwa nguvu na kitu kikiwa kimenikaba kooni, nilikuwa na hasira sana na yule baba yangu

"mama wala usijali wewe utaendelea kuwa mama yangu" nilisema huku machozi yakinitoka

Ghafla nikaanza kuona watu wakipita pita kwa kasi maeneo yale huku wengine wakiwa na wasiwasi mkubwa sana, macho yangu yakagongana na ya Prisca akiwa na Rose wakija upande wangu, nilitahamaki sana kwani hata manesi nao walikuwa wanatimua mbio kuelekea nje ya ile wodi

"vipi kuna nini kimetokea?" niliuliza

"David hali ni mbaya" Prisca alisema

"kuna nini kimetokea tena" niliuliza

"umesikika mlio wa risasi" alisema

Nilitoka pale na kuanza kukimbilia ofisini kwa yule daktari ili nikaangalie nini kimetokea huku nyuma nikiwa nafuatwa na wakina Prisca, macho yangu hayakuamini baada ya kumuona yule daktari akiwa amegemea kwenye kiti huku damu zikiwa zimejaa kwenye shati lake alilolivaa

Wakati naendelea kutahamaki kuhusu kilichomkuta daktari, nilishangaa kusikia kelele za watu kutoka kule wodini nilipomuacha mama , machale yalianza kunicheza na kutoka mbio haraka haraka kuelekea kwa mama yangu, masikini ya Mungu nilikuwa nimeshachelewa kwani mama yangu alikuwa ameshapigwa risasi tatu za kifua, ila nilibahatika kusikia neno moja tu kutoka kinywani mwake

"nakupenda mwanangu"

Moyo uliniuma sana kusikia maneno kama yale kutoka kwa mama yangu wa kunilea, mwili ulikuwa unatetemeka sana kusikia neno lile la uchungu kutoka kwa mama, nilimfunika mama yangu macho kisha nikaanza kwenda pale walipokuwa wakina Prisca

"Prisca we must find those people who killed my mother (Prisca lazima tuwatafute hao watu waliomuua mama yangu)" nilisema huku hasira zikiwa zimenikaba kooni

"usijali David nipo pamoja na wewe" Prisca alisema

Tulianza kutoka pale huku tukitafuta upande gani palipokuwa na fujo, hali ya pale ilikuwa kimya kwani hakukuwa na sauti ya nesi kuongea au sauti ya mgonjwa yoyote kukohoa, tulitembea kwa mwendo wa tahadhali sana huku tukipepesa macho yetu kulia na kushoto kuangalia kama kutakuwa na maadui eneo lile

Wakati nipo kwenye kutembea nilishangaa risasi mbili zikinikosa katika kichwa changu na kugonga kwenye ukuta, kwa mbali nilimuona mtu akikimbia kuelekea nje ya ile wodi, tulianza kumfuata kwa speed ili kujua anaelekea wapi, nilimuona yule jamaa akipanda kwenye gari na kutoka kwa speed ya ajabu

"shit huwezi kuondoka kizembe namna hii" nilijisemea huku nikitafuta njia ya kumfukuzia yule jamaa

Niliangalia pembeni na kuona mtu akishuka kwenye pikipiki, nilimfuata na kuchukua ile pikipiki na kuanza kuondoka nayo kwa kasi kumfukuzia yule jamaa, Prisca na Rose nao walichukua nyingine ili kunifuatilia, mwendo ulikuwa mkali sana kiasi kwamba kila tulipokuwa tunapita watu walikuwa wanapiga milunzi wakidhani tupo kwenye mashindano

Kwa mbali nilianza kusikia ving'ora vya Police vikija upande wetu, yule jamaa alianza kuelekea barabara ya Morogoro, tulitembea kwa muda mrefu sana mpaka alipokata maeneo ya Shekilango na kuelekea barabara ya Mwenge, nasi tulikuwa tukimfuatilia kwa makini sana ili kujua wapi anaelekea, yule jamaa aliendelea na speed mpaka kwenye barabara ya kuelekea Bagamoyo

Aliendelea kuingia ndani ya mapori mpaka alipokuwa anakaribia kwenye jumba moja kubwa la kifahari sana, nilisimamisha pikipiki ili niwasubiri wenzangu tujue nini cha kufanya kwani yule jamaa aliingia kwenye ile nyumba kubwa ya ghorofa

Prisca na Rose walipofika tukaanza kujadili wapi tuanzie na wapi tuishie ili tuweze kujua nini kinachoendelea mule ndani, wakati tunamfukuza yule jamaa sidhani kama alikuwa anafahamu kama kuna mtu yoyote anamfuatilia kwani tulikuwa tunapita njia tofauti na yeye

Tulikaa pale mpaka giza lilipoanza kuingia katika lile eneo, taratibu tulianza kuingia ndani ili tukajue nini kinafanyika pale, ile nyumba ilikuwa na walinzi wengi sana kiasi kwamba kuingia mule ndani ilikuwa ngumu sana, ilitubidi kutumia akili nyingi sana ili tuweze kupenya mule ndani

Kwa mbali niliona bomba la moshi likiwa linatoa moshi nje, nikaona ile ndiyo sehemu pekee ambayo itatufanya tuweze kuingia mule ndani, kikwazo kilikuwa kimoja ni njia gani tunaweza kupita mpaka tuweze kulifikia lile bomba la moshi, tulizifuata senyenge na kuanza kuzitanua kisha nikaanza kupenya kuingia ndani, mara nikasikia sauti nzito ikisema

"Karibu kwenye kifo chako"

ITAENDELEA..............

Je, David atakamatwa?
Nini kitatokea hapo?

posted from Bloggeroid

0 comments:

Post a Comment