PRISCA
SEHEMU YA MWISHO
SONGA NAYO
Wale maaskari walindelea kutunyooshea bastoa zao huku wakiwa wamechukia kisawa sawa kuonyesha hawana utani hata kidogo, sikuwa na ujanja wowote bali niliwaacha wafanye wanachotaka kufanya kwani nisingeweza kupambana nao wakati mimi sikuwa muhalifu, walisogea mpaka pale tuliposimama na mmoja wa wale askari alikuja na kuanza kutuhoji maswali
“ninyi ni wakina nani?” aliuliza
“wala usipate tabu ya kutuhoji hapa utaenda kutuhoji kituoni kwenu” nilisema
“kijana unaonekana wewe ni jeuri sana” alisema
“hapana ,hapa siyo mahali pake na ukiangalia kuna mgonjwa nipo nae hapa naomba kwanza tumpeleke hospitali kisha tutamalizana kituoni” nilisema huku nikimungalia yule askari kwa umakini sana kujua kama atakuwa tayari kukubaliana na mimi
“sawa kijana pandeni kwenye gari” alisema huku akitunyooshea mkono kwenye gari moja ya police
Tuliingia kwenye gari la police na safari ya kuelekea hospitali ikaanza, machozi yalikuwa yananitoka kila nikiangalia hali ya Prisca ilivyokuwa inanitisha, Prisca alikuwa kimya huku mapigo yake ya moyo yakiwa yanadunda taratibu sana, moyoni nilikuwa nasali kimya kimya ili Mungu amnusuru na kifo kwani yeye ndiyo ilikuwa faraja yangu iliyobaki
“eeh Mungu naomba umnusuru mpenzi wangu kwani yeye ndiyo kimbilio langu lililobaki, sidhani kama nitapata mwanamke mwingine atakayenipenda kama anavyonipenda Prisca” nilisema kimoyomoyo
Gari lilikuwa linakimbia kwa kasi sana huku ving’ora vya police vikilia kuyaonya magari mengine kukaa pembeni ili sisi tupite, kila sehemu tuliyokuwa tunapita watu walikuwa wanashangaa sana kwani ilikuwa kama movie ya kizungu, tulifanikiwa kufika hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kuanza kumkimbiza Prisca wodi ya wagonjwa mahututi
Manesi walikuja kumpokea huku wengine wakiingia kumuita daktari aje kutoa huduma ya kwanza, Prisca alilazwa kwenye kitanda na jopo la madaktari lilifika na kumuangalia nini kilichomsibu
“please mpelekeni kwenye chumba cha operation kwani amepigwa risasi na inatakiwa kutolewa haraka sana kwani damu zinazidi kuvuja, pia naombeni kibali cha police ndipo nianze kumuhudumia huyu mgonjwa” daktari mkuu alisema baada ya kufanya uchunguzi mdogo
Manesi walichukua kitanda na kuanza kumpeleka Prisca kwenye chumba cha upasuaji, kwa bahati nzuri tulikuwa na maaskari pale kwahiyo lilikuwa swala rahisi sana kumuelewesha yule daktari ili aweze kumuhudumia Prisca. Madaktari waliingia wenye chumba cha upasuaji na kutuacha sisi tukiwa pale nje tukitafakari
Kichwa changu kilikuwa hakijatulia kwani nilihisi kama Prisca hatoweza tena kuamka sababu alikuwa na hali mbaya sana, mawazo yangu pamoja na macho yangu yalikuwa yakiangalia mlango wa chumba cha upasuaji ili nione mtu mwenye makoti meupe kama atatoka ili atupe taarifa ya nini kinachoendelea juu ya mpenzi wangu
Baada ya lisaa limoja alitoka daktari mmoja na kutufuata pale tuliposimama,kichwa kilikuwa hakifanyi kazi kwani nilikuwa sitaki kupokea taarifa itakayosema kwamba Prisca wangu amefariki dunia. Daktari alifika pale tuliposimama kasha akauliza
“nani anayehusika na huyu mgonjwa?” aliuliza
“mimi hapa daktari” nilijibu kwa haraka sana
“naomba unifuate ofisini” alisema na kuelekea ofisini
Tulianza kumfuata yule daktari tukiwa mimi, Rose pamoja na yule mkuu wa maaskari, tulipoingia ofisini kwake tulikaa kwenye viti na kutega sikio kusikiliza kitu gani anataka kutuambia yule daktari,daktari alikohoa na kuanza kuongea
“poleni sana kwa matatizo yaliyowakuta” alisema huku akirekebisha miwani yake
Muda huo wote nilikuwa nimeganda kama barafu nisijue nini cha kufanya kwani nilikuwa nataka daktari aseme nini kimemkuta mpenzi wangu
“naomba utuambie nini kilichotokea” nilisema huku machozi yakinilenga
“wala usijali kijana” alisema daktari
“naomba uniambie kama mpenzi wangu amekufa au la” nilisema kwa ukali kidogo kwani niliona kama daktari anazunguka kusema
“mpenzi wako hajafa ila yupo katika hali mbaya sana na inahitajika damu kwani jeraha lake limesababisha damu yake kupotea kwa wingi sana” daktari alisema
“swala la damu siyo tatizo hata mimi naweza kumpatia ya kwangu sasa hivi” nilisema
“ngoja tukupime ili tujue kama damu zenu zinaendana” alisema daktari
Nilichukuliwa na kuingizwa kwenye chumba kisha nikaanza kutolewa damu, bahati ilikuwa upande wangu kwani baada ya kuchunguzwa ilionekana kama damu yangu anaweza kuwekea Prisca, lakini kichwani nilijiuliza
“hivi hospitali kubwa kama hii wanakosa damu ya kumuwekea mgonjwa?”,
niliamua kulipuuzia hilo swali a kuendelea na kitu kilichotupeleka pale hospitali
Prisca alifanyiwa huduma zote huku mimi na Rose tukiwa makini sana katika kumuangalia,hospitali ilijazwa maaskari kwaajili ya kuweka ulinzi ili asije akatokea mtu yoyote akamdhuru mgonjwa, hali ya Prisca bado haikuwa nzuri sana kwani alikuwa bado hajapata fahamu
“kijana unahitajika kituo cha police ili kutoa maelezo ya kitu kilichotokea” Mkuu wa wale askari alisema
“ok mimi nipo tayari, vipi kuhusu huyu mgonjwa wangu?” niliuliza
“kuhusu mgonjwa wako wala usijali kuna walinzi wengi sana wamewekwa ili kudumisha usalama” alisema yule askari
“sawa tunawezaa kuelekea” nilisema
“okey” alijibu yule mkuu
“Rose naomba nikuache hapa kwani siwezi kuuamini ulinzi wao moja kwa moja, nakukubali jembe langu” nilimuambia Rose kwa kumnong’oneza
“sawa David wala usijali” Rose alisema
Tulitoka pale wodini a kuingia kweye gari, nilipoangalia nje kweli ulinzi ulikuwa mkubwa sana kwani walikuwa askari wengi na wanajeshi wachache, wote walikuwa makini kwa kuzunguka zunguka huku bunduki zao zikiwa tayari kwa mapambano, kichwani nilijiliza kwanini ulinzi umekuwa mkubwa hivyo wakati sisi tulikuwa raia wa kawaida sana
“samahani mkuu” nilisema kwa kusita
“bila samahani” alisema na kuniangalia
“kwanini mmeweka ulinzi mkubwa sana wakati sisi ni raia wa kawaida sana?” niliuliza
“kila kitu kipo wazi kwa sasa, na huko unaenda kutuambia kiundani mambo yanayoendelea, information tulizozipata bado hazijakamilika vizuri sana kwani wale watu mliowaokoa kwenye ile nyumba wametuambia vitu vichache sana kuhusu hao magaidi” alisema yule mkuu
“sawa nitawaeleza kila kitu ila pindi mtakapofuata nini nataka” nilisema
Safari iliendelea huku tukisindikizwa na magari matatu yaliyojaa mapolice pamoja na wanajeshi, tulifika kituoni na kuongozwa moja kwa moja mpaka kwenye chumba kimoja kilichokuwa na watu wachache waliozunguka meza, baadhi ya watu walikuwa wamevaa suti huku wengine wakiwa wamevaa mavazi ya kipolice pamoja na yakijeshi, kichwani nilijuwa wale watukuwa ni watu wakubwa katika Taifa hili
“karibu kijana” nilikaribishwa kwenye kiti kimoja wapo
“asante” nilisema
“sasa kijana unaweza kutuambia vitu vyote unavyofahamu kuhusu hao magaidi” alisema mtu mmoja aliyekuwa na nguo za kijeshi
“nitawaeleza kila kitu ila naomba usalama kwa mpenzi wangu” nilisema
“usijali mpaka hapa tunapoongea mpenzi wako amehamishiwa katika hospitali ya Jeshi na wapo madaktari bingwa walioletwa kwaajili yake” alisema yule aliyevaa nguo za kijeshi
“sawa hapa naweza kuwaleza kila kitu” nilisema
“okey tuambie” walisema huku wakikaa kwa makini sana
Nilianza kuwaeleza kila kitu kilichotokea tangu nilipokutana na Prisca mpaka hapo tulipokuwa, niliwaeleza kila ninalolijua bila kuruka kitu chochote kwani nilikuwa na hasira sana na wale watu, wote walikuwa wananiangalia kwa makini huku baadhi yao wakiandika kwenye makaratasi, niliwaeleza kila mtu anayehusika na ule mtandao wa magaidi wala sikuficha kitu chochote
Baada ya kumaliza kuongea nilitoa Flash na kuwakabidhi ili waangalie kulikuwa na nini katika ile flash, waliiweka kwenye computer na kuwasha Projector ili kila mmoja aone nini kinachoendelea
“please mkuu wa kitengo cha IT aitwe upesi kwani hii flash imefungwa” alisema yule mkuu wa wanajeshi
Ilipigwa simu haraka kwa muhusika na kuitwa haraka pale kwenye chumba cha mahojiano, yule mtu wa IT alifika na kuanza kushughurika na ile flash, kila mtu alikuwa anamuangalia yeye kwani akishindwa yeye kila kitu kitakuwa kimeharibika,yule mtu wa IT alianza kutabasamu na kutufanya wote tuanze kumuangalia yeye kwa umakini
“mchezo umekwisha” alisema huku akimkabidhi yule mkuu computer
Mkuu alianza kufungua file moja moja na kushuudia vitu vyote vilivyoandikwa pamoja na picha za kutisha zilizokuwepo mule ndani, alifungua file moja lililoandikwa *NEXT MISSIONS*, humo ndipo kila mtu alikuwa makini katika kuangalia nini kilichoandikwa humo, kila mtu alitikisa kichwa kuona maeneo ambayo yalikuwa mbioni kuangamizwa
Yalikuwa maeneo mengi sana ambayo nisingeweza kuyataja yote ila eneo la *Kariakoo* lilikuwa kwenye mpango huo, vile vile walipanga maeneo mengine ya nchini Kenya na Uganda, kila mtu alizidisha umakini katika kuangalia vitu vilivyomo katika ile Flash.
Mkuu alifungua file jingine lililoandikwa *OUR MEMBERS* hilo lilikuwa ni file la watu wote wanaousika na kundi hilo akiwemo mzee wangu, kulikuwa na majina mengi sana hata ya watu ambao ulikuwa huwazanii, yalikuwa majina ya viongozi mbali mbali kutoka katika nchi tofauti tofauti nao wakiwa wanausika na lile kundi la magaidi, wote waliokuwa mule ndani walianza kukuna vichwa kwani ule mtandao ulikuwa mrefu sana kiasi kwamba kuumaliza ilikuwa shughuli pevu, jambo lililotufurahisha ni file moja lililoandikwa *MEETING*
Hilo file lilikuwa na ratiba ya vikao vyote vilivyofanyika na vitakavyofanyika siku za usoni, kulikuwa na kikao kimoja kilichondikwa *GENERAL MEETING* kikimaanisha ni kikao cha wanachama wote wa lile kundi pia kilionyesha wapi kitafanyikia, wote tuliangaliana kisha tukarudisha macho kwenye projector kuangalia vitu vingine
Kiukweli ile flash ilikuwa imebeba vitu vingi sana ambavyo siwezi kuvisema vyote, pia niliwakabidhi na CD ili waangalie kuna nini, walipoiweka yalianza kuonekana matukio ya ajabu sana watu wakichinjwa huku wengine wakifanyishwa ngono kwa nguvu, wapo waliokuwa wanaingiliwa kinyume na maumbile wanawake kwa wanaume, picha nyingi zilikuwa ni za unyama sana kiasi kwamba mtu mwenye roho nyepesi hawezi kuangalia hata kidogo
Tulimaliza kuiangalia ile CD kisha kila kitu kilizimwa na kubaki kila mmoja wetu akiwaza yake, mimi ilikuwa nawaza ni jinsi gani watakavyoweza kukabiliana na wale jamaa sababu wale jamaa walikuwa ni hatari sana,
“kijana tutahitaji msaada wako katika kufanikisha swala hili kwani ninyi ndiyo mnajua wapi pa kuanzia na wapi pa kuishia, bila ya nyie hatujui kama hii mission tutakayoipanga kama itaenda sawa” alisema yule mkuu
“sawa mimi nitakuwa pamoja nanyi ila mission hii hawezi kwenda bila kuwa na yule msichana aliyekuwa hospitali” nilisema huku nikimaanisha kwamba ni Prisca
“kwani kikao chao kitafanyika lini sababu inatakiwa tuvamie katika tarehe hiyo ndiyo tutawakuta wote?” aliuliza mkuu
“kikao chao kitafanyika baada ya miezi miwili mbele” alisema yule mkuu wa police
“nadhani mpaka kipindi hicho huyo mwanamke aliyekuwepo hospitali atakuwa ameshapona na mission itaanza sawa” alisema na kusimama
Watu wote tulitoka kwenye kile chumba cha mkutano ili kwenda kuangaika na majukumu mengine, mimi nilichukuliwa pale na kupelekwa hospitali aliyohamishiwa mpenzi wangu Prisca, pale hospitali nilikuta ulinzi mkubwa sana japo lilikuwa eneo la jeshi, nilipitiliza moja kwa moja mpaka kitandani kwa mgonjwa ili nimuangalie Mpenzi wangu Prisca
Nilipofika chumbani nilimkuta Prisca akiwa amefumbua macho japo alikuwa hawezi kuongea vizuri, moyoni nilifurahi sana kwani nilijiona shujaa sana kusababisha mpenzi wangu akapona, nilimshukuru sana Mungu kwani bila yeye nisingeweza kumuona Prisca akifumbua macho yake tena
“nakupenda sana mpenzi wangu na sijui bila wewe nitaishije” nilisema huku machozi yakinilenga
“na na kupenda pia” alisema kwa kigugumizi
“naomba umuache mgonjwa apumzike kwani amechoka sana” Daktari alisema
Prisca alichomwa sindano ya usingizi na kulala, mimi nilitoka na kwenda kuonana na Rose ili tupange mipango, niliongea sana na Recho mpaka usiku ulipokuwa mkubwa sana na kuamua kwenda kulala, tulipewa hifadhi pale pale jeshini sababu ya usalama wetu
Siku ziliendelea kukatika huku hali ya Prisca ikitengemaa, ilipofika mwezi mmoja na nusu Prisca alikuwa amepona kama zamani japo alikuwa na kovu kwenye mkono wake, baada ya Prisca kupona mipango ya kwenda kuvamia ile kambi ya magaidi ilianza kupangwa, kila mtu alikuwa ameshajipanga vya utosha kwaajili ya kuvamia ile kambi ya magaidi
Jeshi la Tanzania lilikuwa limejipanga vya kutosha huku taarifa zikiwa zimesambaa mpaka kwenye jeshi la Kenya na Uganda nao wakiwa wanajiandaa kwenda kuvamia kwa pamoja, kila mtu alikuwa na kimue mue cha kwenda kuliangamiza jeshi lote la wale magaidi
Siku mbili kabla ya kile kikao cha wale magaidi hakijaanza jeshi la Tanzania lilikuwa tayari limeshawasili katika nchi ya Kenya huku mimi, Prisca na Rose tukiwa miongoni mwao, usiku wa kuamkia kikao vyombo vyote vya baharini vilianza kusogea katika nchi ya Somalia kweye ile meli kubwa iliyokuwemo baharini, siku ya siku ndege za kijeshi pamoja na boti za kijeshi za Tanzania,Kenya na Uganda zilikuwa zimeshawasili ndani ya ile bahari iliyokuwa tishio sana katika Bara la Africa
Tulianza kuingia taratibu katika ile meli ambayo kikao kilikuwa kinafanyikia, japo kulikuwa na walinzi wengi sana lakini tuliweza kuwadhibiti na kuwauwa wote, tulizidi kupenya mpaka ndani ya meli huku tukiwaua walinzi waliokuwa kwenye ile meli bila ya kelele yoyote, tulifika mpaka kwenye kile chumba kilichokuwa kinatumika kwaajili ya kikao
Watu wote tulijipanga kwaajili ya kuvamia mule ndani kwa kushtukiza
“one ,twoo, threeeee”
Tulivunja mlango kwa bomu dogo kisha tukaingia ndani kwa nguvu sana, tulipofika ndani wala hatukuanza kuuliza kwani tulianza mashambulizi kwa wale wote waliokuwa wamebeba silaha, sisi tulikuwa wengi sana kuliko wale magaidi kwani tulikuwa ni muunganiko wa majeshi ya nchi tatu, kazi haikuwa rahisi kwani wale magaidi walipambana kwa nguvu zao zote ili kujiokoa kutoka kwenye mikono yetu
Baadhi ya magaidi walipoona tumewazidi nguvu walianza kujipiga risasi na kujiuwa ili wasikamatwe. Wengine waliamua kusalimu amri baada ya silaha zao kuisha risasi kwahiyo hawakuwa na ujanja wowote ule
Watu wote walifungwa pingu akiwemo baba yangu mzazi, nilikuwa napatwa na uchungu sana kila nilipokuwa nikimuangalia,kwani bila yeye sidhani kama ningempoteza mama yangu mzazi
“baba kila kitu kina mwanzo na mwisho leo ni zamu yako na uovu wako wote utaisha leo” nilisema kwa hasira sana
“naomba hii meli ikaguliwe haraka sana tuone kama kuna mateka wowote waliokuwemo humu ndani” alisema mkuu
Meli ilianza kukaguliwa na baada ya muda kidogo walitolewa watu wa nchi mbalimbali wakiwa kama mateka katika ile meli, nilishangaa kuona mpaka wazungu wakiwa wamewekwa mateka katika ile meli, watu wote tulipanda kwenye ndege na wale magaidi waliowekwa chini ya ulinzi walipakizwa kwenye ndege moja wakiwa chini ya ulinzi mkali sana, moyoni nilikuwa najisikia amani sana kwani kila kitu kimeenda sawa
Tulifanikiwa kufika Tanzania salama na magaidi wote waliingizwa gerezani kabla hata ya kesi yao kusomwa, kesi yao ilifanyika katika mahakama ya kimataifa Arusha ambapo ilikuwa inatumika kuendeshea kesi ya mauaji ya kimbali, kwakuwa ushahidi wote ulikuwa wazi kutokana na ile flash pamoja na CD, watuhumiwa walikosa hata namna ya kujitetea kwani kila kitu kilikuwa wazi
Vyombo vya habari vilijaa sana siku ya hukumu kwani kila mtu alikuwa anataka kujua hukumu ya wale magaidi, hukumu ilipita na wale magaidi walihukumiwa kifungo cha maisha katika Gereza la watu walioshindikana *GUANTANAMO*
Mimi, Prisca pamoja na Rose tulionekana kama mashujaa wa ile vita kwani bila sisi sidhani kama kuna kitu kingewezekana, kila chombo cha habari kilitamani kutuhoji ili japo wapate picha au video zetu wakarushe kwenye vipindi vyao au kwenye magazeti
Nilibahatika kuona gazeti moja likiwa limeandika *SHUJAA ALIYENUSURIKA KIFO*,nilitabasamu kuona lile gazeti kwani lilikuwa linanipa sifa mie wakati Prisca na Rose ndiyo walikuwa kila kitu, ndani ya muda mfupi jina langu lilitambaa kwa kasi sana masikioni mwa watu hasa kwenye vijiwe vya kahawa
Nilifanikiwa kufunga ndoa na Prisca kwani yeye ndiye alikuwa msichana pekee aliyenipenda kwa moyo wake wote, niliwasahau wanawake wangu wote waliopita kama Vick, Grace, Maria pamoja na Queen, niliamua kuwa na Prisca kama kitulizo cha roho yangu.
Harusi yetu iliudhuriwa na watu wengi sana sababu ya umaarufu tulioupata kutokana na ule ushujaa tuliouonyesha
“Nakupenda sana Prisca” nilisema
“nakupenda David” alijibu huku akinikumbatia
Hapo ndipo ilikuwa mwanzo wa safari mpya kati yangu na kipenzi changu Prsca. Hakika Prisca amebadilika sana na kunifanya nimpende kupita nilivyokuwa nampenda mwanzo. Nampenda sana Prisca na yeye ndiyo chaguo langu kwa sasa ninapoandika simulizi hii na mpaka milele.
*NAKUPENDA PRISCA*
MWISHOOOOO

posted from Bloggeroid

0 comments:
Post a Comment