PRISCA
SEHEMU YA KUMI NA SITA
ILIPOISHIA
“vipi mbona camera hazirecord chochote?” niliuliza
Wale jamaa walinitumbulia macho na kutoa bastola katika mifuko yao kisha wakaninyooshea
“tunaomaba mtupatie kila kitu kinachotuhusu sisi” wale jamaa walisema
SONGA NAYO
Akili ilianza kunicheza huku nikipepesa macho yangu pembeni mfano wa mtu aliyekuwa anaangalia kitu kilichodondoka chini, wale jamaa nao wakaanza kuniangalia huku wakiwa hawaelewi nini nafanya
“wewe ina maana hautusikiii au?” waliuliza tena
Bado niligandisha macho yangu pembeni huku nikiibia chini chini kuwaangalia wakina Prisca, nilianza kujiweusha akili kama chizi na kuanza kutembea tembea mule ndani huku nikiruka ruka kama kichaa, wale jamaa walikuja na kunishika bila kujua lile ndiyo kosa walilolifanya, Prisca na Rose waliwavamia wale jamaa na kuanza kuwashambulia kwa mateke mfululizo mpaka wakadondoka chini
Baada ya kuona wamedondoka chini na kuanza kugalagala, tulitoka nje na kuanza kuangalaia usalama mwingine nje palikuwa shwari sana hakukuwa na kitu chochote cha kuogopesha kwa mbali tulianza kusikia miguno ya watu katika chumba kimoja ile miguno ilikuwa ni ya kulalamika kwa maumivu makali sana
Tulifungua kile chumba kwa taadhali kubwa na kuwakuta watu wakiwa wamefungwa kamba huku damu zikiwatoka kwa wingi tulipowaangalia vizuri tukakuta wale ni wafanyakazi wa kile kituo cha habari tulianza kuwapa huduma ya kwanza kisha tukatafuta simu ya mezani ilipo na kutaka kupiga hospitali yoyote ili watume gari ya wagonjwa kuja kuwachukua
Tulipokuwa tukijaribu kupiga namba za hospitali tukagundua kwamba zile simu zilikuwa zimekatwa mawasiliano niliamua kuwasha gari moja lililokuwepo pale na tukaanza kushilikiana na wakina Prisca kuwapakiza wale wagonjwa kwenda hospitali
Baada ya wagonjwa wote kupata nafasi kwenye gari tuliwasha gari na kuondoka kwa speed, tulifanikiwa kufika hospitali ya Muhimbili na kupeleka gari mpaka kwenye sehemu husika huku tukiwasha taa za dharula ili tupate huduma mapema, manesi walianza kufika pale tulipokuwa huku wengine wakiwa wamebeba machela ili kuwabeba wale wagonjwa kuwapeleka wodini
Wakati wanawabeba wale wagonjwa kuna kitu kilinishangaza sana, kitu kilinishangaza ni kuona mtu mmoja kati ya wale wagonjwa akiwa na alama ile waliyokuwa nayo wakina Prisca yaani ile alama ya magaidi, macho yalianza kunitoka kwani sikujua nini kinachoendelea pale
“Prisca unaiona ile alama?” nilimuuliza huku nikimuonyesha
“Mungu wangu nimeiona” Prisca alisema
“nini kinaendelea pale?” niliuliza
“mama yako yupo hatarini” Prisca alisema
“mama yangu yupo hatarini kivipi?” niliuliza
“Yule mgonjwa ni msichana na ataenda kulazwa wodi moja na mama yako na kama unavyojua hawa jamaa ni hatari sana na pale siyo kama ameumia hapana ile ni mipango waliyoipanga ili kumuangamiza mama yako” Prisca alisema
“sasa tunafanyaje ili nimuokoe mama yangu?” niliuliza
“nisubiri” Prisca alisema
Prisca alitoka pale na kuanza kukifuata kitanda cha Yule mama aliyekuwa na alama za magaidi, alijifanya kama anawasaidia manesi kumuweka vizuri, hakuna aliyekuwa anamtilia mashaka kitu gani anataka kukifanya pale, nilimuona Prisca akinifuata huku akitabasamu kwa furaha
“vipi mbona unacheka?” nilimuuliza
“mchezo umekwisha” alisema
“umekwishaje?”niliuliza tena
“wewe subiri sekunde kadhaa utaona” alisema
Na kweli baada ya dakika kadhaa nilianza kuwaona manesi wakianza kuangaika kuhusu Yule mgonjwa. Yule mgonjwa alianza kukakamaa huku damu zikimtoka kwa wingi katika sehemu zote zilizokuwa na matundu, manesi walimkimbiza wodini ili kumpatia huduma ya kwanza kabla hajapoteza maisha
Baada ya dakika tano tuliona manesi wawili wakitoka huku wakitufuata tulipo, nilikaa kwa umakini kuwasikiliza nini wanataka kuongea na sisi
“jamani moja ya wale wagonjwa mliowaleta amefariki dunia sasa hivi” nesi mmoja alisema
Nilijifanya kuhuzunika lakini moyoni nilikuwa nafurahia sana kwani Yule mgonjwa angekuwa kikwazo kwa mama yangu, tulitoka pale na kuelekea ofisini kwa daktari ili tupate japo ripoti ya mama yangu anavyoendelea, tulipofika ofisini na kumkuta daktari akiendelea na kazi zake, nilipoingia alinitolea macho sana mpaka nikawa naogopa kumuangalia
“karibu sana kijana” alisema
“asante” nilijibu
“okey niambie shida yako?” aliuliza
“nimekuja kuangalia maendelea ya mama yangu” nilisema
Yule daktari aliinuka pale kwenye kiti na kwenda kwenye kabati la mafile ili achukue file la mama yangu, macho yalinitoka baada ya kuona kitu kilichonishangaza sana kutoka kwa Yule daktari. Yule daktari alikuwa na ile nembo waliyokuwa nayo magaidi katika shingo yake
“nimekwishaaa” nilijisemea
ITAENDELEA……………

posted from Bloggeroid

0 comments:
Post a Comment