PRISCA-15

Author
PRISCA
SEHEMU YA KUMI NA TANO

ILIPOISHIA

Nilimchukua Yule jamaa na mimi tukatoka nje na kuichukua ile gari niliyokuja nayo, lengo langu kubwa ilikuwa ni kuwaokoa wakina Prisca kwani walinisaidia sana kwenye matatizo yangu

“lazima niwaokoe” nilijisemea

SONGA NAYO

Niliwasha gari kwa speed sana kama nakimbiza majambazi ili niwahi walipopelekwa wakina Prisca nikawaokoe, nilifika maeneo ya Mbezi mwisho nikapandisha njia ya kuelekea Mabwepande, nilipita kwa speed sana huku nikikwepa baadhi ya mashimo yaliyokuwepo barabarani kwa ufundi mkubwa sana

Msitu wa Mabwepande ni msitu ambao majambazi wengi huwa wanafanyia maovu yao kama vile kutesa watu, kuua na hata baadhi ya majambazi wanautumia msitu huu kwaajili ya kujificha pindi wanapofanya matukio sehemu mbalimbali ili wasikamatwe kirahisi sababu msitu wa Mabwepande ni mkubwa sana. Msitu wa Mabwepande pia unasifika kuwa na wanyama wakali sana ambao ni adui kwa binadamu

Tulifika mpaka pale msituni kisha nikamfunga Yule jamaa kwenye mti ili asije kuleta fujo yoyote katika ile mission yangu, niliamua kumuuliza baadhi ya maswali ili yanipe muongozo wa kufanya

“niambie hawa madada wamewekwa sehemu gani halafu nakuacha uondoke zako?” nilimuuliza

“wapo katikati ya msitu watakuwa wamefungwa kwenye mti mkubwa uliokuwepo katikati ya ule msitu,na sidhani kama wataweza kupona mpaka muda huu kwani pale walipofungwa kuna wanyama wakali sana ambao hawawezi kuwaacha wakiwa hai” alisema

“na hao majambazi wenzako wapo wapi?” nilimuuliza

“hao bado watakuwa kule nyumbani kwenu kwani bado wanashida sana na wewe na ndiyo maana wamewakamata wale wanawake ili ukose msaada kwa mtu mwingine” alisema

“OK nashukuru kwa msaada wako ngoja sasa nikuache huru uondoke zako” nilisema huku nikivaa gloves zangu

Nilimfungulia Yule jamaa mpaka yeye mwenyewe alijishangaa kwanini nilimfungulia kirahisi vile na kumruhusu aondoke, mpaka mimi nageuza mgongo kuelekea msituni Yule jamaa alikuwa ameganda kama sanamu akikodoa macho kwangu, ghafla alidondoka chini na kupoteza maisha, usishangae kwanini alidondoka na kufa pale pale,Wakati namfungua nilimpaka ule unga ambao Prisca alikuwa anautumia katika kuua baadhi ya majambazi, mimi niliupata baada ya Prisca kuusahau ndani wakati anakamatwa na wale majambazi

Nisingeweza kumuacha Yule jambazi kwani angenisababishia matatizo makubwa hapo mbeleni, nilianza kuingia kwenye ule msitu kwa tahadhali kubwa sana huku nikiika sawa ile bunduki yangu niliyokabidhiwa na Prisca, nilianza kusikia baadhi ya milio ya wanyama wakali sana pamoja na ndege kama vile bundi, japo nilikuwa na hali ya uoga lakini niliamua kujikaza kisabuni ili nikapambane kuwakomboa wale wanawake

Niliingia ndani zaidi ya ule msitu huku milio ya wanyama wakali nayo ikiongezeka kwa kasi, wakati natemmbea nilijikuta nimekanyaga kamba na kudondoka chini kama mzigo, ile ndiyo ilikuwa pona pona yangu kwani ulichomoka mkuki kwenye kamba na kuchoma kwenye mti, hali ya woga ilianza kuniingia kwani sikujua kwamba kutakuwa na mitego katika ule msitu

“ee Mungu naomba unisaidie ili nitimize adhma yangu ya kuwaokoa hawa wadada” nilijisemea

Niliinuka na kuendelea na safari yangu ya kuingia ndani ya msitu wa pande, safari hii nilikuwa natembea kwa uangalifu mkubwa sana kwani nilikuwa naogopa sana mitego ya wale majambazi, wakati naendelea kutembea kwa nilisikia sauti ya mnyama akilia kwa nguvu kama amebanwa na kitu, nilipopepesa macho yangu kuangalia kuna nini niliona mnyama mfano wa digidigi akiwa amezungukwa na bonge la chatu likitaka kummeza

Hapo ndiyo nusunusu nighairi ile safari yangu kwani katika viumbe nilivyokuwa naviogopa katika maisha yangu wa kwanza ni nyoka, kwakuwa nilikuwa mimi ni mwanaume nilijikaza na kuendelea na safari yangu huku nikiwa makini sana, niliingia mpaka kati kati ya msitu huku nikipepesa macho yangu kuangalia wapi walipofungwa wakina Prisca na Rose

Nilianza kusikia sauti za fisi zikilia huku zikiambatana na sauti za wanawake, nilianza kukimbia kuelekea pale sauti zinaposikika ili nikajue kuna nini, nilipofika pale niliwakuta wakina Prisca wakiwa wamefungwa kwenye mti huku fisi wakiwa wanawazunguka, nilianza kunyata huku nikiangalia pembeni nione kama kuna watu wananiangalia, nilipofika pembeni ya Prisca nilikuta kuna kisu kidogo kilichodondoka chini

Nilikiokota kile kisu na kuanza kukata kamba alizofungwa nazo Prisca, nilimfungua Prisca kisha naye akaenda kumfungua Roseili tuweze kukimbia kwa pamoja. Tuliwatisha wale fisi mpaka wakakimbia na kutuacha wenyewe

“Prisca hawa jamaa wameenda wapi?” niliwauliza

“wameenondoka kwani walihisi hapa hatuwezi kupona David tunakushukuru sana kwa msaada wako” alisema Prisca

“wala usijali mimi ni wako na siwezi kukuacha kwenye mateso wakati mimi nipo” nilisema huku nikimkumbatia Prisca

Tulianza kuondoka kwa tahadhali kubwa sana ili tutoke ndani ya ule msitu wa Mabwepande, tulitembea kwa uelekeo wa sehemu nilipoegesha gari wakati na kuja msituni, tulianza kusikia minong’ono ya watu huku mbwa wakibweka kwa nguvu kuelekea kule tulipotokaa ,mara tulisikia ukimya kidogo kutoka kwa wale mbwa, zilipita kama dakika kumi tukasikia risasi zikipigwa hewani mfululizo

Walikuwa wanafanya vile baada ya kukuta wakina Prisca hawapo eneo lile, tulikaa tayari kwa vita itakayokuja mbele yetu kwani muda wowote wale jamaa wanaweza kutufikia pale tulipo, tulizidisha mwendo wa kukimbia ili tuingie kwenye gari na kuondoka, tulipofika pale kwenye gari tulikuta watu wakiwa wamelizunguka lile gari na watu hao walikuwa ni maaskari

Nilishangaa kuona askari wapo pale na sikujua wamefuata nini eneo lile, niliwaangalia wakina Prisca kisha nikarudisha macho yangu kwa wale maaskari, niliweza kumtambua askari mmoja ambaye nilimkabidhi ile flash niliyopewa na Prisca, alitoka kwa wale wenzake na kuja kusimama mbele yetu

“Mbona mmetuletea flash siyo yenyewe?” aliuliza huku akinipiga ngumi ya tumbo

“mkuu mbona hiyo flash ndiyo ina kila kitu kuhusu wale majambazi” nilisema huku nikiugulia tumbo

“usitake kututania nimenusurika kupoteza maisha yangu sababu ya uzembe wako” alisema

Nilianza kujiuliza kwanini Yule askari angekufa kwa uzembe wangu, au kuna sheria kama askari akifanya kitu cha uongo mbele ya jeshi la Police lazima auwawe? ,lile neno lilikuwa aliniingii akilini kabisa

“kwanini ufe?” niliuliza

“haikuhusu na usiendelee kuniuliza maswali zaidi na safari hii lazima ufe mimi siyo askari kama ulivyotegemea mimi ni askari ninaoshirikiana na hili kundi ili kukutafuta wewe, leo hautotoka katika mikono yetu” alisema Yule askari huku akiwageukia wenzake

Akili ilinicheza haraka haraka na kutema mate pembeni kwa nguvu,Yule askari alipoangalia tu wakati natema mate alishangaa nikimkata mtama na kudondoka chini kama mzigo, Prisca na Rose walichomoka pale kama mshale na kwenda kuwavamia wale jamaa wengine bila kuhofia kama wana bunduki mikononi mwao, wale jamaa walipigwa mateke ya mfululizo na kudondosha bunduki zao chini

Hapo vita ya ngumi ndipo ilipoanza,kwa upande wangu nilikuwa namshikisha adabu Yule askari kwani kidogo nilikuwa najua kupigana ngumi sababu wakati nipo darasa la sita katika shuke ya Msingi Mgulani nilijifunza mchezo wa karate kwa miezi miwili japo nilificha makucha yangu. Yule askari alikuwa mlaini sana kwani nilimfanya nilivyotaka

Baada ya dakika kadhaa tulikuwa tumeshamaliza kazi ya kupiga wale jamaa, tuliingia kwenye gari na kumuingiza Yule askari ili tukamuumbue mbele ya askari wakubwa

“Prisca sasa tunafanyaje hapa?” niliuliza

“kuhusu nini?” na yeye aliuliza

“wewe unadhani askari wote hawapo hivi?” niliuliza

“mimi bado sijajua tutafanyaje David” Prisca alisema

“kama kweli mmeamua kuwaumbua waovu wote fanyeni mpango tuende kwenye vyombo vya habari ili kila raia aweze kuona na kusikia mwenyewe kuhusu hawa viumbe hatari sana” Rose alitoa ushauri huo

Hapo kila mmoja wetu alilidhika na lile wazo la Rose alilolitoa kuhusu nini cha kufanya, lile swala tungelipeleka kwenye kituo cha Police sidhani kama tungekosa askari wengine ambao si waaminifu katika jeshi la Police, lile wazo la Rose lilikuwa bora sababu hata kama mabaya yangetukuta raia wangetambua nini kinaendelea

“ kwanini Yule askari alikuwa anasema flash niliyompa siyo ya ukweli?” niliuliza

“ndiyo siyo ya ukweli mimi nilinunua nyingine ili tupime kama kuna usalama wowote katika kile kituo na kama ulivyoona kumbe askari mwenyewe alikuwa siyo mwaminifu” Prisca alisema

Kweli Prisca alitumia akili sana kubadilisha ile flash na kunipatia nyingine kwani bila ya kufanya hivyo sidhani kama tungesalimika, kwa muda huu wasingeweza kutuua mpaka watakapopata vitu vyao ndiyo wangeweza kutuangamiza

Nilikimbiza gari kwa speed ili tuwahi katika chombo chochote cha habari tukaanike maovu ya wale jamaa, tuliingia kwenye babarabara ya Morogoro na kuanza kuelekeka mjini. Tulifanikiwa kupata kituo kimoja cha televishion kilichopo maeneo ya Mikocheni (sio TBC, ITV wala Clouds), tulingia na kueleza shida zetu tulizoenda nazo.

Mpaka tunaingia katika chumba cha mahojiano Prisca alikuwa hana raha kabisa muda mwingi alikuwa anatoa kifaa chake na kukiangalia huku akitikisa kichwa chake, tulianza mahojiano huku nikielezea kila kitu kilichotokea mpaka tunafika hapo, camera zilikuwa mbele yangu zikiniangalia nami nikiziangalia kwa umakini mkubwa

Baada ya muda kidogo nilishtuka na kuziangalia zile camera vizuri nikagundua kwamba ziklikuwa hazirecord chochote zaidi ya kuwashwa tu, nilipowageukia wale jamaa nikaona wameshtuka na kunikazia macho

“vipi mbona camera hazirecord chochote?” niliuliza

Wale jamaa walinitumbulia macho na kutoa bastola katika mifuko yao kisha wakaninyooshea

“tunaomba mtupatie kila kitu kinachotuhusu sisi” wale jamaa walisema

ITAENDELEA…………

Je, nini kitaendelea hapo?
Je, hao jamaa ni wakina nani?

posted from Bloggeroid

0 comments:

Post a Comment