Kauli ya hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere kuwa Watanzania
wanataka mabadiliko na wasipoyapata ndani ya CCM, watayatafuta nje ya
CCM inaweza kutimia mwaka huu.
Mwalimu alikuwa
akihutubia Mkutano Mkuu wa Halmashauri Kuu ya CCM mkoani Dodoma wakati
wa mchakato wa kumpata rais wa awamu ya tatu mwaka 1995. Alisema mambo
mengi lakini aliwasisitizia wajumbe kuwa Watanzania wanataka mabadiliko
na kwamba wasipoyapata ndani ya CCM, watayatafuta nje ya CCM.
Huku
akisikilizwa kwa umakini, Mwalimu alisema kuna mambo Watanzania
wanataka uongozi wa awamu ya tatu uyafanye mojawapo ni kupambana na
rushwa kwa kuwa Watanzania wengi wamechoka na rushwa.
“Wajumbe wa zamani wa NEC watakumbuka nimepigia sana kelele rushwa wakati nikiwa mwenyekiti. Sasa hivi hali ya rushwa ni mbaya.”
Aliongeza;
“Pili, Tanzania ni masikini, nchi ni ya wakulima na wafanyakazi ambao
si matajiri, nchi haijawa ya matajiri, chama hakijawa chama cha
matajiri, tushughulikie kwa dhati matatizo ya wananchi, hali zao za
uchumi, viwandani, mashambani, shuleni, hospitalini na ateuliwe mtu
ambaye anajua nchi bado ya masikini, wakulima na wafanyakazi na awe
anatambua hivyo.”
Suala la tatu alilozungumzia ni
kuhusu udini akisema umeanza kuzungumzwa kama vile ni sifa. Alisema
zamani hawakuwa wanazungumzia udini wala kujali dini ya mtu kwa vile ni
ya mtu mwenyewe anaijua na hawakuwa wanauliza dini ya mtu, kwa kuwa
haiwahusu.
“Tunataka nchi yetu ipate kiongozi safi, na
kiongozi safi hawezi kutoka nje ya CCM, ninyi wapiga kura, mnaweza
kutupatia kiongozi safi kwa kura zenu, sasa tupatieni kiongozi safi.”
0 comments:
Post a Comment