DK SHEIN MGENI RASMI NANE NANE

Author
RAIS wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa maonyesho ya wakulima Nanenane ambamo kitaifa itafanyika mkoani Lindi kuanzia agosti mosi .
Aidha, maadhimisho hayo yamedhaminiwa na Kampuni ya mtandao wa simu za mkono Tigo.
Lengo lingine ni kuweza kuwauzia wananchi simu za Tigo zenye mtandao kwa bei nafuu, na zilizounganishwa na habari zinazohusu hali ya hewa na kilimo kwa njia za mtandao.
“TIGO tumeshawahi kudhamini maonyesho hayo kwa muda mrefu na tumeshawasaidia wananchi wengi sana kupitia simu zetu ambapo tunawasaidia kupata taarifa za masoko na kuwanganisha wakulima nchi nzima”amesema Wanyancha.
Mbali na kutoa punguzo za bei kwa bidhaa zao pia watatoa mafunzo ya kilimo kwa wananchi wote watakaohudhulia katika maonyesho hayo pamoja na kutoa uduma mbalimbali.
Naye Mwenyekiti Taifa wa Chama cha Wakulima Tanzania (TASO) Engelbert Moyo amesema, maadhimisho hayo ya Nane nane yalianzishwa rasmi mnamo mwaka 1993 na kuzinduliwa rasmi mwaka 1994 kwa lengo la kuwakumbuka wakulima.
Moyo amesema, siku hiyo kutakuwa na washiriki wengi kutoka sehemu tofauti yakiwemo, makampuni mbalimbali pamoja na Mawizara mbalimbali.

0 comments:

Post a Comment