WAZIRI mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, amepanga wakati wowote kutoka sasa, kumkatia rufaa Rais Jakaya Kikwete.
Mkutano kati ya Lowassa na vyombo vya habari, unalenga kumshitaki
Kikwete kwa wananchi kwa kile kinachoitwa, “kukaidi matakwa ya wengi.”
Lowassa alikuwa miongoni mwa wanachama 38 wa chama hicho
waliojitosa katika mbizo za urais, lakini jina lake liliondolewa katika
hatua za awali. Kikwete ndiye anayetajwa kumuengua Lowassa kwa maslahi
yake binafsi.
“Ni kweli kwamba Edo (Edward Lowassa), amepanga kueleza
kilichotokea Dodoma kwenye mikutano ya chama chake. Atafanya hivyo
kupitia mkutano kati yake na waandishi wa habari,” ameeleza mmoja wa
watu waliokaribu na kiongozi huyo.
Hakuweza kufahamika mara moja, ikiwa Lowassa atautumia mkutano huo kueleza mustakabali wake wa baadaye wa kisiasa.
Hata hivyo, mwishoni mwa wiki, madiwani 20 kutoka jimboni kwake
Monduli, walitangaza kukihama CCM na kujiunga na Chadema; jambo ambalo
linadaiwa na wachambuzi wa kisiasa kuwa ni maandalizi ya mwanasiasa huyo
kukimbilia Chadema.
0 comments:
Post a Comment