Leticia atimkia CCM, Abwao aibukia ACT

Author
WABUNGE Leticia Nyerere na Chiku Abwao – Viti Maalum Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wamekihama chama hicho.
Wakati wa Bunge Maalum la Katiba, wabunge wa Chadema, kikiwa ni mwanachama wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), wakisusia vikao vya bunge hilo, Leticia alishutumiwa kuonekana katika ofisi za bunge akijiandikisha na kuchukua posho. Hali hiyo ilipelekea kutoaminika tena ndani ya chama chake.
Kwa upande wake, Abwao ameshindwa katika mchakato wa kura ya maoni katika kumtafuta mwakilishi wa nafasi ya ubunge kupitia Chadema jimbo la Ismani,Iringa
Nyerere akitangaza kuondoka katika chama hicho huku akionyesha wasiwasi usoni akizungumza kwenye mkutano huo huku wanae wawili wa kike wakimshuhudia.
“Kilichonifanya kuhama chadema ni kwamba nimepakumbuka nyumbani (CCM), ambacho kilikua chama changu cha kwanza kukitumikia katika maisha yangu nimeolewa
na kupata watoto nikiwa huko. ”amesema Leticia.
‘Amejishtukia’ na kuongeza kuwa kuhama kwake katika chama hicho si kwa sababu ya maslahi yake binafsi bali ni shauku yake ya kutaka kupigania haki za wanawake na maendeleo ya chama chake kilichomkuza kisiasa.
Licha ya kuhamia CCM wakati wa kipindi hiki cha vuguvugu la uchaguzi, hatoweza kuwa mmoja wa wagombea wa chama hicho kwa kipindi hichi kwani muda wa kufanya uteuzi wa wabunge wa viti maalum ulishakwisha.

0 comments:

Post a Comment