SIMBA jana ilijichuja katika mbio za
kuwania nafasi ya pili katika Ligi Kuu ya
Tanzania Bara baada ya kufungwa mabao
2-0 na Mbeya City huku wapinzani wao
katika nafasi hiyo, Azam FC wakiibuka na
ushindi.
Kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya,
wenyeji Mbeya City walizima matumaini
ya Simba kushika nafasi ya pili baada ya
ushindi huo ulioifanya sasa iwe nyuma ya
Azam FC kwa pointi saba baada ya
mabingwa hao watetezi kuishinda Kagera
Sugar kwa mabao 2-1 kwenye Uwanja wa
Azam Complex, Chamazi nje ya Jiji la Dar
es Salaam.
Simba sasa imebaki na pointi zake 35 na
imebakiwa na mechi nne sawa na Azam
FC, ikiwa na maana kuwa Wekundu wa
Msimbazi wana uwezo wa kufikisha pointi
47.
Azam FC ikiwa na uwezo wa kunyakua
pointi 54, hivyo inahitaji pointi tano tu
kuifuta Simba katika michuano ya
kimataifa kwa msimu mwingine wa tatu.
Jijini Mbeya, Joachim Nyambo anaripoti
kuwa mabao yaliyopeleka kilio kwa Simba
jana yalifungwa na Paul Nonga na Peter
Mwalyanzi katika kila kipindi na
kuiwezesha timu hiyo mali ya
Halmashauri ya Jiji la Mbeya kuweka hai
matumaini ya kubaki Ligi Kuu baada ya
msimu ambao ulikabiliwa na changamoto
kubwa kwake.
Nonga alifunga bao la kwanza katika
dakika ya 45 akiunganisha krosi ya Deus
Kaseke, kabla ya Mwalyanzi kutokea
benchi akichukua nafasi ya Cosmas Fred
kufunga bao la pili kwa kuwachambua
mabeki wa Simba na kipa wao, Manyika
Peter, na kufunga bao ambalo limefifisha
matumaini ya Simba kupanda ndege
mwakani.
Huo ni ushindi wa pili wa Mbeya City kwa
Simba msimu huu baada ya kushinda
mechi ya kwanza kwa idadi kama hiyo ya
mabao kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
Kwenye Uwanja wa Azam Complex,
wenyeji Azam FC walizinduka baada ya
kuandamwa na sare tatu mfululizo na
kuishinda Kagera Sugar inayokamata
nafasi ya nne, kwa mabao 2-1.
Mabao ya Azam yalifungwa na Frank
Domayo katika dakika ya 40 na
Gaudennce Mwaikimba katika dakika ya
81. Bao la Kagera lilifungwa na Babu Ali
dakika ya 52.
Matokeo hayo yameifanya Azam FC
kufikisha pointi 42, ikiwa ni pointi nne
nyuma ya vinaraYanga huku mabingwa
hao watetezi wakiwa wamecheza mechi
moja zaidi ya Yanga yenye mechi 21.
Mjini Morogoro, John Nditi anaripoti
kuwa Polisi Morogoro ilipata ushindi wa
mabao 2-0 dhidi ya Ndanda FC kwenye
Uwanja wa Jamhuri na kufufua
matumaini ya kubaki Ligi Kuu na kuiweka
pabaya timu hiyo ya Mtwara.
Bao la kwanza la Polisi lilifungwa katika
dakika ya 49 na Christopher Edward kwa
shuti baada ya kupokea krosi ya Salum
Kihimba. Mfungaji aliingia kipindi cha pili
kuchukua nafasi ya Edgar Mfumakule.
Bao la pili lilifungwa katika dakika ya 63
kwa penalti na Said Bahanuzi baada ya
kipa wa Ndanda, Wilbert Mweta
kumkwatua mfungaji alipompiga chenga
na kwenda kufunga.
Mwamuzi Erick Anoka wa Arusha
aliamuru penalti na kadi nyekundu kwa
Mweta na kuingizwa kipa Saleh Malande
baada ya kutolewa mchezaji mwingine.
Zikiwa zimebaki dakika 10 pambano
kumalizika, mwamuzi huyo alimtoa nje
kwa kadi nyekundu Ally Telu wa Polisi
kwa kumdanganya kwa kujiangusha
katika eneo la hatari, akiwa tayari
amepewa kadi ya njano.
Polisi Moro imefikisha pointi 24 na
kuishusha mkiani Prisons yenye pointi 21,
yenyewe ikifungana pointi na JKT Ruvu
katika nafasi ya 12. Ndanda FC imebaki
na pointi 25 katika nafasi ya 11.
Ligi hiyo itaendelea leo kwa mechi mbili
kwa Prisons kuwa mwenyeji wa Mtibwa
Sugar kwenye Uwanja wa Sokoine wakati
Mlandizi mkoani Pwani, Ruvu Shooting
itakuwa mwenyeji wa Mgambo JKT.
kuwania nafasi ya pili katika Ligi Kuu ya
Tanzania Bara baada ya kufungwa mabao
2-0 na Mbeya City huku wapinzani wao
katika nafasi hiyo, Azam FC wakiibuka na
ushindi.
Kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya,
wenyeji Mbeya City walizima matumaini
ya Simba kushika nafasi ya pili baada ya
ushindi huo ulioifanya sasa iwe nyuma ya
Azam FC kwa pointi saba baada ya
mabingwa hao watetezi kuishinda Kagera
Sugar kwa mabao 2-1 kwenye Uwanja wa
Azam Complex, Chamazi nje ya Jiji la Dar
es Salaam.
Simba sasa imebaki na pointi zake 35 na
imebakiwa na mechi nne sawa na Azam
FC, ikiwa na maana kuwa Wekundu wa
Msimbazi wana uwezo wa kufikisha pointi
47.
Azam FC ikiwa na uwezo wa kunyakua
pointi 54, hivyo inahitaji pointi tano tu
kuifuta Simba katika michuano ya
kimataifa kwa msimu mwingine wa tatu.
Jijini Mbeya, Joachim Nyambo anaripoti
kuwa mabao yaliyopeleka kilio kwa Simba
jana yalifungwa na Paul Nonga na Peter
Mwalyanzi katika kila kipindi na
kuiwezesha timu hiyo mali ya
Halmashauri ya Jiji la Mbeya kuweka hai
matumaini ya kubaki Ligi Kuu baada ya
msimu ambao ulikabiliwa na changamoto
kubwa kwake.
Nonga alifunga bao la kwanza katika
dakika ya 45 akiunganisha krosi ya Deus
Kaseke, kabla ya Mwalyanzi kutokea
benchi akichukua nafasi ya Cosmas Fred
kufunga bao la pili kwa kuwachambua
mabeki wa Simba na kipa wao, Manyika
Peter, na kufunga bao ambalo limefifisha
matumaini ya Simba kupanda ndege
mwakani.
Huo ni ushindi wa pili wa Mbeya City kwa
Simba msimu huu baada ya kushinda
mechi ya kwanza kwa idadi kama hiyo ya
mabao kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
Kwenye Uwanja wa Azam Complex,
wenyeji Azam FC walizinduka baada ya
kuandamwa na sare tatu mfululizo na
kuishinda Kagera Sugar inayokamata
nafasi ya nne, kwa mabao 2-1.
Mabao ya Azam yalifungwa na Frank
Domayo katika dakika ya 40 na
Gaudennce Mwaikimba katika dakika ya
81. Bao la Kagera lilifungwa na Babu Ali
dakika ya 52.
Matokeo hayo yameifanya Azam FC
kufikisha pointi 42, ikiwa ni pointi nne
nyuma ya vinaraYanga huku mabingwa
hao watetezi wakiwa wamecheza mechi
moja zaidi ya Yanga yenye mechi 21.
Mjini Morogoro, John Nditi anaripoti
kuwa Polisi Morogoro ilipata ushindi wa
mabao 2-0 dhidi ya Ndanda FC kwenye
Uwanja wa Jamhuri na kufufua
matumaini ya kubaki Ligi Kuu na kuiweka
pabaya timu hiyo ya Mtwara.
Bao la kwanza la Polisi lilifungwa katika
dakika ya 49 na Christopher Edward kwa
shuti baada ya kupokea krosi ya Salum
Kihimba. Mfungaji aliingia kipindi cha pili
kuchukua nafasi ya Edgar Mfumakule.
Bao la pili lilifungwa katika dakika ya 63
kwa penalti na Said Bahanuzi baada ya
kipa wa Ndanda, Wilbert Mweta
kumkwatua mfungaji alipompiga chenga
na kwenda kufunga.
Mwamuzi Erick Anoka wa Arusha
aliamuru penalti na kadi nyekundu kwa
Mweta na kuingizwa kipa Saleh Malande
baada ya kutolewa mchezaji mwingine.
Zikiwa zimebaki dakika 10 pambano
kumalizika, mwamuzi huyo alimtoa nje
kwa kadi nyekundu Ally Telu wa Polisi
kwa kumdanganya kwa kujiangusha
katika eneo la hatari, akiwa tayari
amepewa kadi ya njano.
Polisi Moro imefikisha pointi 24 na
kuishusha mkiani Prisons yenye pointi 21,
yenyewe ikifungana pointi na JKT Ruvu
katika nafasi ya 12. Ndanda FC imebaki
na pointi 25 katika nafasi ya 11.
Ligi hiyo itaendelea leo kwa mechi mbili
kwa Prisons kuwa mwenyeji wa Mtibwa
Sugar kwenye Uwanja wa Sokoine wakati
Mlandizi mkoani Pwani, Ruvu Shooting
itakuwa mwenyeji wa Mgambo JKT.
0 comments:
Post a Comment