JUMUIYA ya Wanawake wa Chama Cha
Mapinduzi (UWT) Mkoa wa Arusha,
imetangaza wazi kuwakataa walimu
kusimamia uchaguzi wa madiwani,
wabunge na rais, kutokana na tabia ya
kufanya hujuma kwa chama hicho wakati
wanasaidiwa mambo mengi ya msingi na
serikali ya CCM.
Mbali ya walimu, pia UWT
imewanyooshea kidole baadhi ya polisi
mkoani Arusha kwa kuwa na mapenzi
yaliyopitiliza dhidi ya Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema),
hali inayowafanya kushindwa kutenda
haki katika maamuzi mbalimbali.
Msimamo huo umetangazwa kwa nyakati
tofauti na Mwenyekiti wa jumuiya hiyo
mkoa wa Arusha, Flora Zelote alipokuwa
akizungumza katika kata mbalimbali za
wilaya ya Arusha katika ziara yake ya
kikazi ya kukagua uhai wa jumuiya hiyo
na chama kwa ujumla.
Alisema kutokana na hali hiyo, jumuiya
yake ina mpango wa kufikisha
mapendekezo yao kwa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC) na makao makuu ya
CCM ya namna ya kuwapata wasimamizi
wengine wa uchaguzi mbadala wa walimu
hao.
Alisema CCM imeonekana kama mpangaji
katika nyumba yake, kutokana na mabaya
yanayofanywa dhidi yake na watumishi
wanaowalipa mishahara huku chama
hicho kikiendelea kukaa kimya.
“Polisi na walimu wanaolipwa mishahara
na serikali ya CCM wanakihujumu chama
chetu, hii ni sawa na mwenye nyumba
kugeuka kuwa mpangaji au mke
anayebaki kung’ang’ania cheti cha ndoa
wakati nje ‘nyumba ndogo’ amemdhibiti
mumewe.
Hii haiwezekani,” alisema Zelote. Alitumia
nafasi hiyo kuwatahadharisha viongozi
wa Taifa wa CCM, kurejesha majina yale
yale ya wagombea watakayoyapendekeza
mikoani, vinginevyo wakirejesha majina
mengine tofauti, watakuja kuwanadi wao
katika kampeni.
Zelote alisema hali ilivyo sasa, chama
kinapaswa kuheshimu matakwa ya
wananchi ya nani wanamtaka, badala ya
kuendelea na tabia ya kuwapendekeza
watu kwa utashi wa kikundi cha watu,
jambo ambalo linasababisha ugumu
katika kuwanadi wagombea hao.
“Mimi naomba nitoe msimamo wa
jumuiya yangu mkoa wa Arusha, sisi
tutapendekeza wagombea kwa matakwa
ya wananchi watakaowachagua na
tutawafikisha kwao ili wafanye maamuzi
sahihi, wakifanya vinginevyo, wakawaleta
wa kwao, tutawapa taarifa waje
kuwafanyia kampeni,” alisema Zelote.
Alisema maamuzi hayo, pia yatafutwa
katika ngazi ya wilaya, ambapo vilevile
kama wataacha mapendekezo ya kata
zao na wakafanya vinginevyo, nao
watapewa taarifa kwenda kuwanadi
wagombea waliowarejesha kwa utashi
wao.
Mapinduzi (UWT) Mkoa wa Arusha,
imetangaza wazi kuwakataa walimu
kusimamia uchaguzi wa madiwani,
wabunge na rais, kutokana na tabia ya
kufanya hujuma kwa chama hicho wakati
wanasaidiwa mambo mengi ya msingi na
serikali ya CCM.
Mbali ya walimu, pia UWT
imewanyooshea kidole baadhi ya polisi
mkoani Arusha kwa kuwa na mapenzi
yaliyopitiliza dhidi ya Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema),
hali inayowafanya kushindwa kutenda
haki katika maamuzi mbalimbali.
Msimamo huo umetangazwa kwa nyakati
tofauti na Mwenyekiti wa jumuiya hiyo
mkoa wa Arusha, Flora Zelote alipokuwa
akizungumza katika kata mbalimbali za
wilaya ya Arusha katika ziara yake ya
kikazi ya kukagua uhai wa jumuiya hiyo
na chama kwa ujumla.
Alisema kutokana na hali hiyo, jumuiya
yake ina mpango wa kufikisha
mapendekezo yao kwa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC) na makao makuu ya
CCM ya namna ya kuwapata wasimamizi
wengine wa uchaguzi mbadala wa walimu
hao.
Alisema CCM imeonekana kama mpangaji
katika nyumba yake, kutokana na mabaya
yanayofanywa dhidi yake na watumishi
wanaowalipa mishahara huku chama
hicho kikiendelea kukaa kimya.
“Polisi na walimu wanaolipwa mishahara
na serikali ya CCM wanakihujumu chama
chetu, hii ni sawa na mwenye nyumba
kugeuka kuwa mpangaji au mke
anayebaki kung’ang’ania cheti cha ndoa
wakati nje ‘nyumba ndogo’ amemdhibiti
mumewe.
Hii haiwezekani,” alisema Zelote. Alitumia
nafasi hiyo kuwatahadharisha viongozi
wa Taifa wa CCM, kurejesha majina yale
yale ya wagombea watakayoyapendekeza
mikoani, vinginevyo wakirejesha majina
mengine tofauti, watakuja kuwanadi wao
katika kampeni.
Zelote alisema hali ilivyo sasa, chama
kinapaswa kuheshimu matakwa ya
wananchi ya nani wanamtaka, badala ya
kuendelea na tabia ya kuwapendekeza
watu kwa utashi wa kikundi cha watu,
jambo ambalo linasababisha ugumu
katika kuwanadi wagombea hao.
“Mimi naomba nitoe msimamo wa
jumuiya yangu mkoa wa Arusha, sisi
tutapendekeza wagombea kwa matakwa
ya wananchi watakaowachagua na
tutawafikisha kwao ili wafanye maamuzi
sahihi, wakifanya vinginevyo, wakawaleta
wa kwao, tutawapa taarifa waje
kuwafanyia kampeni,” alisema Zelote.
Alisema maamuzi hayo, pia yatafutwa
katika ngazi ya wilaya, ambapo vilevile
kama wataacha mapendekezo ya kata
zao na wakafanya vinginevyo, nao
watapewa taarifa kwenda kuwanadi
wagombea waliowarejesha kwa utashi
wao.
0 comments:
Post a Comment