Nan kuibuka mchezaji bora EPL

Author
CHAMA cha wanasoka wa kulipwa England
kimatangaza orodha ya mastaa
watakaochuana kuwania Tuzo ya
Mwanasoka Bora wa Mwaka katika nchi
hiyo.
Straika kinara wa mabao kwenye kikosi
cha Tottenham Hotspur, Harry Kane
ametajwa sambamba na mastaa wa Chelsea,
Eden Hazard na Diego Costa wanaopewa
nafasi kubwa ya kutamba huku kukiwa na
mshangao mkubwa kwamba hakuna
mchezaji yeyote wa Manchester City.
Kipa David De Gea ndiye mchezaji pekee
kutoka kwenye kikosi cha Manchester
United aliyepewa nafasi kwenye orodha
hiyo baada ya kuonyesha kiwango kizuri
msimu huu.
Mastaa wa kutoka Amerika Kusini, Alexis
Sanchez wa Arsenal na Philippe Coutinho
wa Liverpool wameingia kwenye orodha ya
wakali wanaopewa nafasi kubwa ya
kuibuka kidedea katika tuzo hiyo.
Winga wa Chelsea, Hazard ndiye
anayepewa nafasi kubwa ya kutamba
akifuatiwa na Kane. Sanchez, anashika
namba nne kwenye orodha ya wenye nafasi
kubwa na kufuatiwa na De Gea, Coutinho
na Mhispaniola mwenye asili ya Brazil,
Costa.
Orodha ya wachezaji makinda wanaowania
tuzo hiyo imetajwa pia, huku nyota sita
wakiwamo kwenye upande wa
wanaoshindania tuzo ya wakubwa.
Wachezaji wengine wanaotajwa kwenye
kuwania tuzo iyo ni kipa Thibaut Courtois
wa Chelsea na winga Mwingereza wa
Liverpool, Raheem Sterling.

0 comments:

Post a Comment