KAMA ni majivuno, kama ni kweli, kama
ni mzembe, vyovyote utakavyoona, lakini
staa wa Barcelona na Argentina, Lionel
Messi amesahau idadi ya ‘hat trick’
alizofunga katika maisha yake ya soka.
Messi amevunja rekodi ya mchezaji
aliyepiga hat trick nyingi zaidi akiwa
anachezea timu moja. Machi mwaka huu
katika ushindi wa mabao 6-1 dhidi ya Rayo
Vallecano Nou Camp alitupia hat trick yake
ya 32 katika maisha ya soka ikiwa ni moja
zaidi ya mkongwe wa zamani wa Athletic
Bilbao, Telmo Zarra.
Hat trick hiyo ilikuwa ya 24 kwa La Liga
peke yake na kumfanya kuwa mchezaji
aliyetupia hat trick nyingi zaidi La Liga.
Lakini Messi pia amekuwa mchezaji wa
kwanza kufunga mabao 40 katika misimu
sita tofauti ya Ligi ya La Liga.
Hata hivyo, licha ya ufungaji wa hat trick
nyingi, Messi amehojiwa na mtandao wa
klabu yake ya Barcelona na kukiri kwamba
hana kumbukumbu na hat trick alizofunga
na hakumbuki jinsi alivyofunga mabao
hayo.
“Kwa sasa tunavyoongea siwezi
kukumbuka. Inabidi niyaone tena mabao,
au mtu aniambie kitu kuhusu hayo mabao
ndiyo nitayakumbuka,” alisema Messi
ambaye anachukuliwa kama mmoja kati ya
wachezaji bora kuwahi kutokea katika uso
wa dunia. Hata hivyo, licha ya usahaulifu huo, Messi
anakumbuka hat trick moja aliyopiga dhidi
ya Real Madrid katika dimba la nyumbani
Nou Camp kuwa ni moja kati ya hat trick
ambayo hawezi kuisahau.
“Moja niliyofunga dhidi ya Real Madrid
wakati tulipotoka sare ya 3-3 pale Nou
Camp ilikuwa maalumu sana kwangu,
kwanza ilikuwa na maana kwa sababu ya
umuhimu wa mechi yenyewe, pia ilitupa
uongozi wa ligi,” anakumbuka Messi.
“Ingawa hatukutwaa ubingwa lakini
ilikuwa muhimu sana kwa sababu ilikuwa
dhidi ya Real Madrid,” aliongeza Messi
ambaye ameifungia Barcelona mabao 277
katika kipindi cha miaka 10 na zaidi
alichotumia klabuni hapo akitokea kwao
Argentina akiwa na umri mdogo.
Hata hivyo, Messi aliwasifu sana wachezaji
wenzake ambao wote huwa wanasaini
mipira anayopewa huku akidai kwamba
bila ya wao asingeweza kupiga hat trick
hizo nyingi.
“Siku zote wanasaini kwa sababu najua ni
kazi ya timu nzima. Bila ya wachezaji
wenzangu nisingeweza kufikia tuzo hizi
binafsi na kwa sababu nawategemea wao ili
nifunge mabao, ni heshima kwangu kuwa
na saini zao,” aliongeza Messi
ni mzembe, vyovyote utakavyoona, lakini
staa wa Barcelona na Argentina, Lionel
Messi amesahau idadi ya ‘hat trick’
alizofunga katika maisha yake ya soka.
Messi amevunja rekodi ya mchezaji
aliyepiga hat trick nyingi zaidi akiwa
anachezea timu moja. Machi mwaka huu
katika ushindi wa mabao 6-1 dhidi ya Rayo
Vallecano Nou Camp alitupia hat trick yake
ya 32 katika maisha ya soka ikiwa ni moja
zaidi ya mkongwe wa zamani wa Athletic
Bilbao, Telmo Zarra.
Hat trick hiyo ilikuwa ya 24 kwa La Liga
peke yake na kumfanya kuwa mchezaji
aliyetupia hat trick nyingi zaidi La Liga.
Lakini Messi pia amekuwa mchezaji wa
kwanza kufunga mabao 40 katika misimu
sita tofauti ya Ligi ya La Liga.
Hata hivyo, licha ya ufungaji wa hat trick
nyingi, Messi amehojiwa na mtandao wa
klabu yake ya Barcelona na kukiri kwamba
hana kumbukumbu na hat trick alizofunga
na hakumbuki jinsi alivyofunga mabao
hayo.
“Kwa sasa tunavyoongea siwezi
kukumbuka. Inabidi niyaone tena mabao,
au mtu aniambie kitu kuhusu hayo mabao
ndiyo nitayakumbuka,” alisema Messi
ambaye anachukuliwa kama mmoja kati ya
wachezaji bora kuwahi kutokea katika uso
wa dunia. Hata hivyo, licha ya usahaulifu huo, Messi
anakumbuka hat trick moja aliyopiga dhidi
ya Real Madrid katika dimba la nyumbani
Nou Camp kuwa ni moja kati ya hat trick
ambayo hawezi kuisahau.
“Moja niliyofunga dhidi ya Real Madrid
wakati tulipotoka sare ya 3-3 pale Nou
Camp ilikuwa maalumu sana kwangu,
kwanza ilikuwa na maana kwa sababu ya
umuhimu wa mechi yenyewe, pia ilitupa
uongozi wa ligi,” anakumbuka Messi.
“Ingawa hatukutwaa ubingwa lakini
ilikuwa muhimu sana kwa sababu ilikuwa
dhidi ya Real Madrid,” aliongeza Messi
ambaye ameifungia Barcelona mabao 277
katika kipindi cha miaka 10 na zaidi
alichotumia klabuni hapo akitokea kwao
Argentina akiwa na umri mdogo.
Hata hivyo, Messi aliwasifu sana wachezaji
wenzake ambao wote huwa wanasaini
mipira anayopewa huku akidai kwamba
bila ya wao asingeweza kupiga hat trick
hizo nyingi.
“Siku zote wanasaini kwa sababu najua ni
kazi ya timu nzima. Bila ya wachezaji
wenzangu nisingeweza kufikia tuzo hizi
binafsi na kwa sababu nawategemea wao ili
nifunge mabao, ni heshima kwangu kuwa
na saini zao,” aliongeza Messi
0 comments:
Post a Comment