Wenger:Arsenal itaibandua Monaco

Author
Image result for arsenal   Kocha wa Arsenal Arsene Wenger anaamini kuwa kilabu hiyo bado ina fursa ya kuibandua Monaco katika michuano ya kilabu bingwa barani Ulaya licha ya kucharazwa 3-1 katika awamu ya kwanza ya mechi hizo.
Arsenal itakabiliana na timu hiyo ya Ligi ya daraja la kwanza siku ya jumapili huku ikiwa hakuna timu ilioweza kufanikiwa kubadilisha matokeo kama hayo katika michuano hiyo.
Wenger:Tuna changamoto kubwa mbele yetu lakini tutafanya kila kitu kuhakikisha kwamba tunafuzu kwa robo fainali.
''Wao ndio wanaopigiwa upato kufuzu lakini tunaweza kubadilisha mambo''.
''Tutahakikisha kuwa tuna hamu na imani ya kushinda''
Arsenal italazimika kufunga bao tatu kwa bila ili kuweza kufuzu kwa robo fainali.
Tayari kilabu hiyo imepata motisha kufuatia ushindi wao wa mabao 3-0 dhidi ya kilabu ya West Ham siku ya jumamosi.

0 comments:

Post a Comment