Serikali ya Tanzania kupitia kikosi maalumu kilichopewa kazi ya
kuchunguza mtandao wa Ujangili kwa miaka miwili kimefanikiwa
kuwakamata watuhumiwa takribani 40 wanaodaiwa kujihusisha na baiashara
haramu ya pembe za ndovu.
Kwa mujibu wa mkuu wa kitengo cha kupambana na ujangili wa mamlaka
ya hifadhi ya ngorongoro (NCAA) Robert Mande alisema kwamba mafanikio
ya kuufumua mtandao huo yanatokana na ushirikiano wa vikosi vya kuzuia
ujangili, katika mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro hifadhi ya Serengeti,
Manyara na Tarangire.
Aliongeza kuwa changamoto katika kupambana na majangili hao ni ukubwa na uzito walio nao watuhumiwa wa mtandao huo.
Inadiawa kuwa wanaojihuisha na ujangili ni watu wa ngazi mbali mbali
wakiwemo wataalamu wa kuua tembo na kutoa meno kwa muda mfupi,
madalali, ambao wamekuwa wakipewa mikopo ya magari, silaha na mahitaji
mengine ya kufanya ujangili ili kufanikisha kazi hizo pamoja na kutoa
rushwa kwa baadhi ya watendaji wanaojaribu kukwamisha kazi yao.
Katika hatua nyingine, Mapambano zaidi yanahitajika dhidi ya vitendo
vya ujangili kwa kuwa inaonekana wazi kwamba baadhi ya majangili ni watu
maarufu na pengine wana ushawishi mkubwa katika jamii. Suala la Msingi
ni kutowafumbia macho majangili hao, kwa kufanya hivyo kamwe adhma ya
kukomesha vitendo vya ujangili nchini Tanzania havitakoma
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment