Polisi mkoani Singida inawashikilia waganga wanane wa kienyeji kwa
tuhuma za kuendesha shughuli zao bila kuwa na kibali halali na kupiga
ramli chonganishi zilizozuiwa na Serikali kutokana na kutajwa kuwa
chanzo cha mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi Albino.
Watuhumiwa hao wakiwemo wanawake wanne wamekamatwa na Askari Polisi wa doria Jumatatu hii majira ya saa sita mchana wakati wakifanya shughuli zao katika maeneo mbalimbali ya Mji wa Singida.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida Mrakibu mwandamizi Simion Haule amesema mbali ya kuendesha shughuli za uganga wa kienyeji bila kibali na kupiga ramli chonganishi, watuhumiwa hao pia wamekutwa na nyara za Serikali.
Kaimu Kamanda Haule amesema pamoja na kudhibiti rasmli chonganishi, Polisi mkoani Singida imeweka mikakati mbalimbali ya ulinzi wa Albino ili kuzuia mauaji yanayoendelea dhidi yao.
Watuhumiwa hao waliokamatwa na Polisi wanatarajiwa kupandishwa kizimbani wakati wowote kwa ajili ya kujibu shtaka la kufanya shughuli za uganga wa kienyeji bila kuwa na kibali, kupiga rasmli chonganishi zilizozuiwa na Serikali pamoja na kumiliki nyara za Serikali kinyume cha sheria.

0 comments:
Post a Comment