Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana amezitaka ofisi zote zilizopo
mipakani zinazohusika na ufuatiliaji wa ushuru wa forodha hususani kwa
upande wa malori kuangalia utaratibu wa kueleweka ili kupunguza
msongamano na usumbufu kwa madereva wa magari hayo.
Magari hayo yanadaiwa kukaa katika maeneo ya mipakani kwa muda mrefu kabla ya kuvuka kwenda nchi jirani.
Akiongea na wananchi wa Longido katika Mkutano uliofanyika kijiji cha Olendeki alisema tatizo hilo ni la muda mrefu sana na sio namanga pekee hali hiyo ipo hata katika mpaka wa Tunduma.
Kwa upande wao madereva ambao wamekuwa wakisafirisha bidhaa mbalimbali yakiwemo mafuta kwa kupitia Mpaka wan a manga walisema hali hiyo imekuwa ikiwaathiri kiuchumi kwa kiasi kikubwa
Ni siku ya Sita Tangu Katibu Mkuu huyo wa CCM ambaye ameambatana na Katibu wa Nec itikadi na uenezi Nape Tangu alipoanza ziara Mkoani arusha kwa lengo la Kuimarisha chama pamoja na kushiriki ujenzi wa miradi mbalimbali
0 comments:
Post a Comment