LOWASSA ACHANGIWA SHILINGI LAKI 7 NA MASHEIKH KUGOMBEA URAIS

Author

Masheikh zaidi ya 50 kutoka Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani, leo wamemkabidhi kiasi cha shilingi 700,000/- za kuongezea kuchukua fomu ya kuwania urais 2015.
Mashekhe hao wakiongozwa na Yusuf Surulu na Alli Mtumwa wamemkabidhi fedha hizo nyumbani kwake mjini Dodoma na kushuhudiwa na Mbunge wa Urambo Magharibi, Prof Juma Kapuya.
wamesema kuwa wameona mtu pekee anayefaa kushika wadhifa huo ni yeye hivyo wanamsihi atangaze nia na achukue fomu ya kugombea na wapo nyuma yake katika dua.
Lowassa amewaambia viongozi hao wa dini kuwa makundi mbalimbali ya jamii yamekuwa yakimuomba kugombea Urais lakini wao wamemfanya ashawishike sasa kufanya hivyo wakati ukifika.

0 comments:

Post a Comment