RAIS KIKWETE ZIARANI NAMIBIA

Author

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewasili nchini Namibia Ijumaa, Machi 20, 2015 kwa ziara ya siku tatu nchini humo ambako atahudhuria sherehe mbili kubwa na muhimu kwa taifa la Namibia.
Rais Kikwete na ujumbe wake amewasili kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Hosea Kutako mjini Windhoek kiasi cha saa 12 jioni kwa saa za Namibia tayari kwa ziara hiyo.
Wakati wa ziara hiyo, Rais Kikwete atahudhuria Sherehe za Miaka 25 ya Uhuru wa Namibia na pia kuhudhuria Sherehe za Kuapishwa Rais wa Tatu wa Jamhuri ya Namibia, Mheshimiwa Hage Gotrified Geinagob.
 

0 comments:

Post a Comment