WEMA,PENNY WADAIWA KUMALIZA BIFU LAO, DIAMOND ANGO'A CHUMA KIPYA

Author
Mastaa wa Bongo Wema Sepetu na Penniel Mungilwa 'Penny'ambao walikuwa na bifu kwa muda mrefu kisa kikiwa ni kugombea penzi la staa wa Bongo Fleva,Diamond Platinumz wamedaiwa kumaliza tofauti zao baada ya picha kusambaa mtandao wawili hao wakionekana kukumbatiana kwa furaha.
Wakati wawili hao wakipatana picha nyingine zimezagaa mtandaoni zikimuonyesha Diamond akiwa na mrembo mwimbaji wa nchini Uganda,Zari the boss lady wakiwa kimahaba huku mashabiki wakijiuliza ni kweli Diamond aachana na Wema na sasa yupo na mrembo huyo?
Habari zingine zinasema mrembo huyo ametua nchini kufanya ngoma na Diamond.

0 comments:

Post a Comment