Wataalamu wa afya wanasema kuwa, idadi ya kesi mpya ni muhimu sana kuliko wanaokufa kutoka na ugonjwa huo, kwani inaakisi jinsi virusi vya Ebola vinavyosambaa.
Watu wasiopungua 75 wamewekewa karantini katika mji mkuu wa Mali, Bamako baada ya kufariki dunia muuguzi mmoja aliyekuwa na ugonjwa huo.
WHO imeongeza kuwa, vifo vingine 13 na watu 30 wameambukiwa katika nchi 5 za Nigeria, Senegal, Mali, Uhispania na Marekani.
Shirika hilo limeongeza kuwa, maambukizo ya ugomjwa huo yamepungua katika nchi za Guinea na Liberia lakini yameendelea kuongezeka huko Sierra Leone ambako kumeripotiwa kesi mpya 421 za maambukizi
Shirika la madaktari wasiokuwa na mipaka Medecins Sans Frontieres limetangaza kuwa litafanyia majaribio tiba mpya za maradhai ya Ebola Afrika Magharibi.






0 comments:
Post a Comment