Mateka wakatwa vichwa na IS

Author
Katika video iliyorushwa hewani na kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislam Novemba 16, ambalo limekiri kumkata kichwa mateka wa Marekani, Peter Kassig, kundi hilo limekiri pia kuwakata vichwa wanajeshi wa Syria.



Wakati huu kundi hilo la wapiganaji wa Dola la Kiislam limekua likiwaua mateka kutoka nchi tofauti, hususan Uingereza, Marekani, Ufaransa...
Wanajeshi 18 wa Syria wameonekana katika video hiyo wakiwa wanasubiri kukatwa vichwa na wapiganaji wa kundi la Islamic State.
Hayo yakijiri rais wa Marekani Barrack Obama, ameelezea kuawa kwa Kassing kwa kukatwa kichwa na wapiganaji hao kama kitendo cha kinyama na kuthibitisha kuuliwa kwa mfanyakazi huyo wa kujitolea aliyekwenda Syria kutoa misaada ya kibinadamu kabla ya kukamatwa na wapiganaji hao.
Obama ameongeza kuwa Marekani imempoteza mtu aliyejitolea kubadilisha maisha ya watu nchini Syria, kifo ambacho kimepokelewa kwa huzuni kubwa na familia ya Kassing mwenye umri wa miaka 26.
Abdul-Rahman Kassing ambaye awali alifahamika kama Peter Kassing na kubadilisha dini, kwa lengo la kunusuru maisha yake kutoka kwa wapiganaji hao anakuwa mtu wa tano kutoka mataifa ya magharibi kuuliwa kwa kukatwa kichwa na wapiganaji hao wa Islamic State.
Kinyume na hapo awali, wapiganaji wa Islamic State hakutoa nafasi kwa Kasing kuzungumza kabla ya kutekeleza mauji hayo.

0 comments:

Post a Comment