#TrueStoryNo5
----------------
SEPTEMBER 11
Na Fredy P. Utd
June 2, 2000 Atta alipanda basi kutoka Ujerumani mpaka Nchini Czech Republic katika jiji la Prague. Kutokea hapo akapanda ndege mpaka nchini Marekani.
Al-Shehhi yeye aliondokea kutokea Dubai ambapo alipitia Brussels na baadae akatua Marekani.
Kumbu kumbu zinaonyesha kuwa al-Shehhi alianza kuwasili na siku chache, mbele Atta naye akawasili, yaani June 3, 2000.
Wote waliwasili kupitia uwanja wa ndege wa Newark Inatenational Airport.
Kwa mwezi mzima walikuwa wanakaa kwenye mahoteli kwenye miji mbali mbali huku wakiendelea kuomba nafasi kwenye vituo mbali mbali vya kufundisha urubani.
Kumbukumbu zinaonyesha kuwa waliwahi kufika hata kituo cha chuo cha Airman Flight School kilichopo Norman, Oklahoma lakini hawakupapenda na wakaendelea "kutalii" kwenye vyuo vingine.
Hatimaye wakapata sehemu waliyoipenda, Venice, Florida ambapo walipata nafasi katika kituo cha Huffman Aviation.
Kwahiyo wakaweka kabisa makazi na kupanga apartment hapa hapa Venice, Florida.
Wote wawili wakafungua akaunti katika benki ya SubTrust na wakawa wanalokea fedha za kujikimu kutoka kwa mtu anayeitwa Ali Abdul Aziz Ali aliyeko UAE. Mtu huyu alikuja kugundulika baadae kuwa alikuwa ni mpwa wa KSM.
Rafiki yao Ziad Jarrah naye alipata kituo cha kujifunza urubani hapa hapa Venice lakini kilikuwa ni kituo tofauti na kile wanachojifunzia Atta na al-Shehhi.
Atta na al-Shehhi walianza rasmi mafunzo tarehe 6 July, 2000.
Inaelezwa kuwa walikuwa na bidii haswa ya kujifunza. Walitrain kila siku asubuhi mpaka jioni kana kwamba hawana kingine chochote cha kufanya au wameletwa duniani kujifunza kurusha ndege pekee.
Mpaka kufikia mwanzoni mwa mwezi August, walikuwa wanaweza kurusha ndege wenyewe bila msimamizi au abiria (solo flight).
Wakaendelea kujifinza kwa bidii kubwa na hatimaye mwishoni mwa mwezi September, 2000 wakapata leseni za Urubani wa ndege binafsi.
Baada ya hapo mwezi October wakahama kituo cha kujifunzia na kwenda katila kituo cha Jones Aviation kilichopo Sarasota.
Lengo lao la kwenda huku ni ili wapatiwe mafunzo ya kurusha ndege kubwa zenye nguvu zaidi (multi-engines planes).
Lakini wakaanza kupewa 'longolongo' kuwa inabidi waanze na videge vidogo kisha baadae wahamoe kwenye midege mikubwa.
Hawakutaka kupoteza muda, mwezi huo huo kati kato wakarudi kwenye kituo chao cha zamani cha kujifunzia cha Huffman Aviation.
Wakaendelea kunifunza kwa bidii zaidi na zaidi na hatimaye mwezi November wakapewa daraja la 'instrument' (instrument rating).
Hawakutaka kubweteka wala kuridhika mapeka, 'wakakaza" zaidi na kuongea juhudi kubwa, na hatimaye mwezi December, 2000 wote wawili wakakabidhiwa Leseni za Urubani wa Ndege za Abiria.
Kwahiyo sasa walikuwa na rihusu kuendesha au kujifunza dege la aina yoyote haijalishi ukibwa wake.
Ndipo hapa kuanzia Desemba 22 hadi 29, wakaenda chuo Eagle International kwa ajili ya mafunzo mafupi ya Kuendesha Madege makubwa.
Kwa kuwa walikuwa wanakimbizana na muda, iliwabidi waanze kujifunza kwa njoo ya 'Mafunzo hisi' (Simulation trainings) ili kuepuka mlolongo wa urasimu wa kupata madege makubwa ya kujifunzia.
Mafunzo haya ya 'simulation' mfano mzuri kuyaelezea unakuwa kwenye chumba maalumu na chenye vifaa maakumu na ukakuwa kama vile "unacheza game" lakini tofauti na "game" za kawaida, hii yenyewe inakuwa ina uhalisia kabisa. Unakuwa kana kwa 100% kama upo kwenye ndege halisi.
Kwahiyo, kwanza wakaenda Opa-locka Airport ambapo hapa walifanya 'simulation training' ya ndege ya Boeing 727 kwa tarehe 29 na 30 ya mwezi desemba, 2000.
Baada ya hapo wakaenda Pam Am International Airport kwa ajili ya 'simulation training' ya ndege ya Boeing 767, hii walifanya tarehe 31 desemba.
Mpaka kufikia hapa walikuwa na ujuzi wote waliokuwa wanahotaji ili kurusha aina yoyote ya ndege.
WASHIRIKA WENGINE WANAWASILI
Jumla ya washiriki wote walihusika kuteka ndege na kuzilipua kwenye majengo siku ya 9/11 jumla yao walikuwa watu 19.
Tukiacha washiriki wakuu watatu kutoka "Hamburg Cell" ambao nimewaelezea kwa kina (Atta, al-Shehhi na Jarrah).. Washiriki wengi wachache waliwasili mwaka 2000 lakingi waliwasili mwanzano na kati kati ya mwaka 2001.
Washiriki hawa wote ni hawa wafuatao;
Nawaf al-Hamzi (miaka 25)& Khalid Mihdhar (miaka 26)
Hawa wawili walikuwa wanahusudiwa sana na bin Laden. Na aliwachagua yeye binafsi wawemo kwenye mpango huu.
Marafiki hawa wawili walipigana kwenye vita ya Bosnia upande wa Waislamu, na walishiri mapigano mengi huko Afghanistan.
Uraia: Saudi Arabia
Wail al-Shehri (miaka 28) & Waleed al-Shehri (miaka 22)
Hawa walikuwa ndugu. Kaka mtu alikiwa ni mwalimu wa shule ya awali na mdogo mtu alikiwa ni mwanafunzi wa chuo.
Walijiunga na kambi za Al-Qaida nchini Afghanistan mwaka 2000 na kuchagulowa kushiriki makakati huu.
Uraia: Saudi Arabia
Abdulaziz al-Omar (miaka 25)
Hakuna kumbu kumbu nyingi kumuhusi huyu, ila inafahamika tu kwamba alikuwa ni Imam na pia alikuwa mlinzi kwenye uwanja wa ndege.
Uraia: Saudi Arabia.
Satam al-Saquami (miaka 25) & Majed Moqed (miaka 24)
Hawa marafiki wote wawili walikuwa ni wanafunzi wa chuo kikuu cha Saudi Arabia wakisome sheria.
Waliacha chuo mwaka 2000 na kujiunga na kambi za Al-Qaida nchini Afghanistan.
Uraia: Saudi Arabia
Fayez Banihammad (miaka 24)
Huyu alikuwa ni kibarua ambaye alipata viza kwa programu maalumu ya 'Visa Express'.
Uraia: UAE
Hamza al-Ghamdi (miaka 20), Ahmed al-Ghamdi (miaka 22) & Mohammed al-Shehri (miaka 22)
Hawa ndugu wawili na rafiki yao wote walikuwa ni wanafunzi wa chuo kikuu.
Wote waliacha chuo mwaka 2000 na kwenda kujiunga na mapigano ya waislamu huko Chechnya. Baadae wakajiunga na kambi za Al-Qaida nchini Afghanistan.
Uraia: Saudi Arabia
Hani Hanjour (miaka 29)
Huyu Mara ya kwanza alifika Marekani mwaka 1991 na kujiunga na chuo kikuu cha Arizona akisomea Kingereza.
Mwaka mmoja baadae akaondoka na kurejea kwao.
Akarudi tens Marekani mwaka 1996 akiishi maeneo ya California akosomea tena Kiingereza lakino pia Safari hii akaongeza na masomo ya Urubani.
Mwaka 1999 akapata leseni ya Urubani wa ndege za abiria na kurejea Saudi ili kutafuta kazi.
Mwaka 2000 akajiunga na Al-Qaida na ndiko huko Osama akagundua ujuzi wake wa Urubani na kuamua kumtumia.
Uraia: Saudi Arabia
(Huyu ndiye aliyemreplace al-shibh yule mwanachama wa "Hamburg Cell" aliyenyimwa viza!! Mpango wa awali wa Osama ulikuwa ndege zote ziendeshwe na wanachama wa Kijiwe cha Hamburg, kwahiyo baada ya al-shibh kunyimwa viza ndipo ukaja ulazima wa kumtumia huyu)
Salem al-Hamzi (miaka 20)
Huyu naye alienda Marekani kama kibarua kwa program maalumu ya 'Visa Express'.
Uraia: Saudi Arabia
Ahmed al-Haznawi (miaka 20)
Kuna taarifa chache kumuhusu huyu.
Inajulikana tu mwaka 2000 aliingia Chechnya na kujiunga ma mapigano ya waislamu na baadae akaelekea Afghanistan ambako alijiunga na Al-Qaida.
Uraia: Saudi Arabia
*Ahmed al-Nami (miaka 24)*
Huyu alikuwa ni muazini huko Saudia.
Taarifa zinaonyesha kwamba mwaka 2000 alienda Hijja na aliporejea moja kwa moja akaenda Afghanistan na kujiunga na Al-Qaida.
Uraia: Saudi Arabia
Saeed al-Ghamdi (miaka 21)
Huyu haana undugu wa kifamilia na wale "Ghamdi" nilio waorodhesha mwanzoni japo wote wanatoka kabila moja.
Huyu naye alikuwa ni mwanafunzi wa chuo nchini Saudi Arabia na aliacha chuo mwaka 2000 na kuelekea Chechnya kujiunga na mapigano ya waislamu.
Akiwa huko akashawishowa kwenda Afghanistan ambako alijiunga na kikundi cha Al-Qaida.
Uraia: Saudi Arabia
HUSIKOSE #TrueStoryNo6 hapo baadae tena. 😂😂😂
#TheBold
0 comments:
Post a Comment