SEPTEMBER 11

Author

#TrueStoryNo6
---------------
SEPTEMBER 11

Na Fredy P. Utd

MAELEKEZO YA MWISHO KUTOKA KWA BIN LADEN

(KONGAMANO LA SPAIN)

Mara kadhaa tangu Mohammed Atta afike nchini Marekani alisafiari mara kwenda Ujerumani na hata Indonesia, yote hii katika kuratibu tukio lilikuwa mbele yao.

Lakini katika safari zote hizi safari ya muhimu zaidi ni ile aliyoifanya July 7, 2001.

Siku hii Atta alipanda ndege ya shirika la SwissAir, Flight 117 kutoka Miami kwenda Zurich, Uswisi.

Alipofika Zuric akapanda ndege nyingine ya SwissAir, Flight 656 kwenda Madrid nchini Hispania.
Aliwasili hispania saa 10:45 jioni na kukaa katika Hoteli inayoitwa Diana Cazadora iliyopo maeneo ya Bajaras karibu kabisa na Uwanja wa ndege.

Usiku wa siku hiyo alimpigia simu mtu anayeitwa Bashar Ahmad Ali Mesleh, mwanafunzi wa Jordan mjini Hamburg.
Huyu ndiye alikuwa mtu wa kati kiunganishi kati yake na Ramzi bin al-Shibh.

Siku mbili mbele, Atta alikodi gari aina ya Hyundai Ascent na kuendesha mpaka mitaa ya beach ya Tarragona kwenye eneo linaloitwa Reus.
Hapo alikuwa anasubiriwa na bin al-Shibh aliyewasili kutoka uwanja wa ndege.

Baada ya hapo wakaelekea kwenye hoteli inayoitwa Monica na wakalala hapo mpaka kesho yake.

Siku iliyofuata hawakujulikana walienda wapi, na ina aminika kuwa walienda kwenye 'safe house' ya Al-Qaida hapo nchini Spain.

Wakiwa huko wakafanya kikao kizito sana.
Ina aminika kwenye kikao hicho alikuwepo Atta, bin al-Shibh, KSM na Said Bahaji.
Kikao hiki ndicho kilichobatizwa jina la "2001 summit" katika ulimwengu wa jamii ya Ujasusi.

Kikaoni hapa ndipo al-Shibh na KSM wakawasilisha kwa Atta maagizo kutoka kwa bin Laden.

Kwamba;

Anataka shambulio lifanyike haraka kwani, anahofia kuwa na "makachero" wengi wa Al-Qaida kwa pamoja ndani ya marekani hii inaweza kuharibu mpango wote na kushitkiwa na vyombo vya ulinzi na usalama.

Pia akataja na target anazozitaka zilipuliwe, na akataja Whitehouse, World Trade Center na Pentagon.
Akazitaja hizi kama "Symbol of America". Ndizo sehemu ambazo zitawafedhehesha, kuwadhalilisha na kuwauma Wamarekani zikishambuliwa.

Akamuagiza kuwa kama ikitokea dharura yoyote kukawa na dalili kuwa ndege haitofikia target yake, basi idondoshwe mahali popote.. Kamwe wasikubali kukamatwa wakiwa hai.

Pia akampa angalizo kuwa asiwaambie wenzake details zote hizo mpaka siku za mwisho kabisa kabla ya tukio.

Atta akapokea maagizo yote haya kwa utii. Pia akatoa dukuduku lake. Mwenzao, Jarrah.

Atta alikuwa na wasiwasi kuwa Jarrah anaweza akabadili mawazo kuhusu ushiriki wake katika tukio hilo.
Akadai kuwa Jarrah amebadilika mno baada ya kufika Marekani. Amekuwa anatumka pombe, na pia amepata girlfriend wa kituruki anayeishi Hamburg ambaye kila siku lazima ampigie simu na mara kwa mara anasafiri nje ya Marekani.
Akatilia mkazo zaidi kwamba hata muda huo anapotoa taarifa hiyo, Jarrah yuko kwao Yemen ameenda "kusalimia" na akiwa anarudi huko lazima atapitia Hamburg kwa girlfriend wake.

Bin al-Shibh akajitolea kuongea na Jarrah akifika Hamburg ili asije kujitoa mwishoni na kuvuruga mpango wote.

Lakini pia KSM akamsisitiza bin al-Shibh kwamba akiongea naye na akihisi Jarrah hana nia tena ya kuendelea na mpango huo, basi amjulishe mapema na nafasi yake ichukuliwe na kijana mwingine aliyeitwa Zacharias Moussaoui.

Wote wakakubaliana na kikao kikaisha.

Bin al-Shib akaondoka Spain kurudi Ujerumani tarehe 16, July 2001.

Atta akakaa Spain siku tatu zaidi.
Akakaa siku mbili katika Hoteli ya Casablanca Playa Hotel.
Kisha akakaa siku mbili nyingine Hotel Residencia Montstant.

Atta akaondoka Spain Tarehe 19, July 2001 kwa ndege ya shirika la Delta Airlines na kurejea Marekani.

Sasa ilibakia hatua moja tu! Yeye na wenzake kutekeleza tukio..

HUSIKOSE #TrueStoryNo7 hapo kesho.
😂😂😂

0 comments:

Post a Comment