#TrueStoryNo4
Na Fredy P. Utd
Katikati ya mwaka 1999, kijiwe hiki kilipata mgeni adhimu kwenye ulimwengu wa watu wenye misimamo mikali, walitembelewa na Khalid al-Masri.
Kama kawaida akaanzisha mjadala kutaka kujua mtazamo wao kuhusu vugu vugu la Jihad lilikuwa linaendeshwa na Waislamu huko Chechnya kupinga eneo hilo kudhibitiwa na Urusi.
Mjadala ulikuwa mkali, ambapo Atta na wenzake walionyesha ni kiasi gani wanaunga mkono vugu vugu hilo.
Mwishoni mwa mjadala wakamuomba Khalid al-Masri awasaidie kuingia Chechnya ili wakajiunge na mapambano hayo ya Jihad.
Khalid akawapa mawasiliano wawasiliane na mtu aliyepo maeneo ya Duisburg anayeitwa Abu Musab.
Atta na vijana wenzake wakafunga safari kumfuata Abu Musab.
Walikuwa hawajui, kumbe huu ulikuwa ni "mchongo" umepangwa kwa umahiri kabisa.
Wakupofika Duisburg na kwenda kuonana na Abu Musab, wakashikwa na butwaa kukuta kumbe Abu Musab lilikuwa ni jina la bandia, ila uhalisia ni kwamba mtu alikuwa ni Mohammedou Ould Slahi moja ya 'makachero' muhimu zaidi wa Al Qaida kwenye nchi za Ulaya.
Slahi akawaeleza vijana hawa, kwamba kwanza ni vigumu mno kuingia Chechnya kutokana na udhibiti mkali wa Urusi.
Lakini pia wanahitaji mafunzo zaidi kama wanataka kujiunga rasmi na Jihad.
Hivyo basi akawashauri waende Karachi, nchini Pakistan na maelekezo zaidi watayakuta huko.
Baada ya Atta na wenzake kukubali, Slahi akawaeleza kuwa wakifika Pakistan waende mpaka kwenye ofisi za Taliban na wamuulizid mtu anaitwa "Umar al Masri".
Atta na wenzake wakayapokea hayo maelezo na kurejea Hamburg.
November 29, mwaka 1999 Atta na Jarrah wakapanda ndege ya shirika la Turkish Airlines, Flight TK1662 kutoka Hamburg kwenda Istanbul. (Shehi aliondoka na ndege nyingine peke yake na bin al-Shibh aliondoka wiki mbili baadae).
Walipofika Istanbul wakapanda ndege nyingine ya Turkish Airlines, Flight TK1056 kutoka Istanbul kwenda Karachi.
Kama walivyoelekezwa na Slahi, wakaelekea mpaka kwenye ofisi za Taliban na baada ya kukaribishwa wakaomba kuonana na "Umar all Masri"!!
Wao hawakujua, wakidhani ni mtu, lakini hili lilikuwa ji neno la fumbo (code word) ambalo kwenye ulomwengu wa siri wa Taliban lilikuwa na maana kuwa hao walikuwa ni wageni wa "Bwana Mkubwa".
Kwahiyo wakachukukiwa kutoka hapa Karachi, Pakistan na kupelekwa Kandahar, nchini Afghanistan.
Wakiwa huku Kandahar, wakapelekwa katika nyumba ya siri, na pasipo kutegemea na kwa mshangao mkubwa... Wakakutanishwa na "Bwana Mkubwa", Usama bin Laden.
Osama akawaeleza kuwa amekuwa anawafuatilia kwa muda mrefu ya vijana hao kupendekezwa kwake na KSM.
Akawaeleza kuwa anataka wawe wahusika kwenye shambulio la kihistoria ambalo litawashikisha adabu wamarekani na hawatasahau maishani mwao mwote, lakini shambulio hilo linahitaji vijana hao wajitoe uhai wao.!! Akawauliza kama wako tayari??
Vijana hao bila kusita sita, wakamueleza kuwa hiyo itakiwa ni heshima kubwa kwao kutekeleza tukio hilo, na wako tayari kuyatoa maisha yao muhanga.
Inaelezwa kuwa Osama "akawaapisha"!
Vijana wakala kiapo cha utii na uaminifu wao kwa Osama na Al Qaida.
Baada ya hapo vijana hawa wakapelekwa kwa kamanda mkuu wa wapiganaji wa Al Qaida, Bw. Mohammed Atef ambaye aliwapa muhtasari kuhusu tukio linahusu nini. Baada ya hapo kwa karibia miezi miwili wakapewa mafunzo ya ukakamavu wa kijeshi na mbinu za mawasiliano ya kijasusi na mbinu za kishushushu.
Kisha, wakapelekwa tena Pakistan ambako huko walikutana na KSM aliyewapa 'specifics' kuhusu mission yote.
Wakiwa tayari wamewiva kwenye kile wanachotakiwa kukifanya, February 24 mwaka 2000 wakapanda ndege ya Shirika la Turkish Airlines, Flight TK1057 kutoka Karachi mpaka Istanbul na walipofika Istanbul wakapanda ndege nyingine ya shirika la Turkish Airlines, Flight TK1661 kutoka Istanbul kurejea Hamburg.
Walipofika Hamburg wakaripoti kuwa wamepoteza Passports ili kuficha walikokuwa wametoka.
Hawakutaka kupoteza muda, siku chache baadae wakajiunga na kozi za Urubani hapo hapo Ujerumani.
Baada ya Atta, al-shehhi, al-shibh na Jarrah kurudi Ujerumani walikuwa na mabadiiko makubwa.
Wengi wanaweza kudhani kwamba labda wangekuwa sasa na misimamo mikali lakini ilikuwa tofauti.
Walikuwa na mabadiliko makubwa ya haiba zao na mtindo wa maisha.
Mfano; waliacha kwenda msikito wa Al-Quds, wakanyoa ndevu walizokuwa wamefuga, wakaacha kuvaa 'kiarabu', na badala yake wakaanza kuvaa kimagharibi.
Pia mtu kama Atta ambaye alikuwa ni mkimya kupindukia akabadilika na kuwa mtu mcheshi.
Hii haikiwa bahati mbaya, walifanya hivi ili wasiweze kutilowa mashaka yoyote na watu pamoja na vyombo vya usalama.
Pia kama kawaida wakaripoti kuwa pasipoti wamezipoteza hivyo wakatengeneza nyingine.
Al-Shehhi yeye kwa kuwa alikuwa ni raia wa UAE, hivyo akaenda huko na kuomba kabisa Visa ya kwenda amarekani.
Baada ya wote kujifunza kozi za mwanzo kuhusu urushaji ndege (Basics) kila mmoja akawa anashawishi 'supervisor' wake amuandikie 'recommendation' ya kwenda kusoma zaidi kozi hizo za urubani nchini Marekani. Na wote wakifanikiwa kupata recommendations!
Baada ya hapo wakaanza kutuma maombi kwenge vyuo mbali mbali nchini Marekani.
Kwa mfano, Atta inakadiriwa alituma karibia maombi 60 kwenye vituo mbali mbali vya kufundisha urubani nchini Marekani.
Baada ya hapo wakaanza michakato ya kupata viza.
Mohamed Atta aliomba viza yake siku ya tarehe 17, mwezi May mwaka 2000 katika ubalozi wa Marekani, nchini Ujerumani.
Kutokana na kusoma kwake Ujerumani kwa kipindi kirefu, hivyo basi akaaminiwa na hakufanyiwa upembuzi wowote wa kina, na akapewa viza siku iliyofuata ya tarehe 18 May, 2000.
Akipewa Viza ya miaka mitano ya kundi la B-1/B-2 (viza ya utalii/biashara).
Kama nilivyoeleza, al-Shehhi yeye viza yake alienda kuichukulia UAE.
Lakini kwa bahati mbaya (au nzuri) rafiki zao al-Shibh na Essabar walinyimwa Viza.
Sababu kubwa ya Al-Shibh kunyimwa Viza ilikuwa ni kutokana na uraia wake wa Yemen.
Kwa miaka mingi, mpaka sasa hivi, ni ngumu mno kwa raia wa Yemen kupata Viza ya Marekani. Sababu kubwa ni vile ambavyo kwa miaka mingi, asilimia kubwa ya raia wa Yemen wakienda nchini Marekani hubakia humo Marekani kimagendo hata baada ya Viza zao kuisha muda. Hii imepelekea mamlaka za Marekani kuwakataa Wayemen wengi wanaoomba Viza kwenda nchini Marekani.
Al-Shibh hakukata tamaa haraka baada ya kukataliwa kupewa viza. Kuna kipindi alituma mpaka ada ya dola elfu mbili kwenye kituo cha urubani cha Florida kilichomkubalia kwenda kusomea urubani na akatumia kigezo hicho kwenda kuombea viza (kwamba akubaliwa na Chuo cha Marekani na elipa ada tayari), lakini bado akakataliwa Viza.
Muda mwingine alideposit hela nyingi kwenye akaunti yake ili kuonyesha hana "njaa" hivyo hawezi kibaki kimagendo nchini Marekani akikubaliwa kuingia, lakini bado ubalozi ukakataa kumpa viza.
Baadae akakubali matokeo na akaamua kubaki Ujerumani wenzakw wakielekea Marekani na akaamua kujipa jukumu la kuwatumia hela wenzake wakiwa huko na pia kuwa kuinganishi kwa wao walioko Marekani na viongozi wao waliopo Ulaya ma Uarabuni.
HUSIKOSE #TrueStoryNo5 hapo badae kidogo
0 comments:
Post a Comment