HATUKUPENDA TUWE HIVI-32

Author

Genes alirudi katika chumba alichomwacha Angel,alipata furaha ya ajabu kumwona Angel ameamka kitandani akijifuta,"ulifanyaje?" Genes aliuliza huku akimshika mkono,"mbona sijafanya kitu?" Angelalijibu,"mbona mlango umefungwa na ufunguo haupo hapo?" Genes aliuliza huku akiwa na haraka ya kuondoka maeneo yale.Angel alitoa ufunguo na kumkabidhi,Genes alimuaga kwa kumbusu shavuni kwa kumshukuru kwa penzi tamualilopata.***Baada ya wiki mbili Angel alianza kujihisi hali ya tofauti tumboni,tabia ya kutema mate,kutapika na tumbo kuvuruga ilianza,"usikute ninamimba" Angel alijiuliza,lakini kwakua alikua kidato cha nnealijikazana kusema hata kama ni mimba basi yupo karibu kuhitimu hivyo isingemwachisha shule,"ngoja ikifika siku ya kawaida ya kuingia mwezini nitapata jibu kamili" alijisemea Angel.Genes alijihisi mshindi kwa kukuta msichana mrembo kama Angel kua bikra,maranyingi alisikia mwanaume wenzake wakisema ni vigumu sana kumkuta msichana mrembo kua na bikra.Licha na hayo mapenzi yake na Miriam yalizidi kukua kadri siku zilivyozidi kusonga,Miriam alijiona mwenye bahati kila siku alisali sana na kumshukuru mungu kwa zawadi hiyo, alifanya kazi kwa bidii na umakini ili kuhakikisha anapata mafanikio makubwa ili aweze kuanza maisha na Genes.Jina la Miriam lilizidi kukuaalifingua duka la vifaa vyaujenzi (hardware) katikati ya mji wa Arusha, alitoa ajira kwa vijana wengi na wafanyakazi wake walimpenda kwani alihakikisha kila mfanyakazi wake anafanikiwa.***Baada ya miaka mitatu tayari Miriam alishakua katika orodha ya matajiri wakike tena kwa umri mdogo katika jiji la Arusha, alijenga nyumbaza kifahari,alifungua hotel za kitaliina kuanzisha miradi katika mikoa mbalimbali,alifungua super market kubwa mtaa wa Kariakoo jijini Dar es salam,hivyo alifanya safari nyingi mikoani,alimiliki mashamba ya mpunga hukokahama.Genes alizidi kufurahia maisha kwani alipomaliza kidato cha nne alishindwa mtihani hivyo hakuendelea tena na masomo na kwa bahati nzuri Miriam alikua ashakua tajiri mkubwa,"sasa tuoane tuanze kuishi pamoja" Miriam aliongea kwa utani kutaka waanzemaisha na Genes,na bila ubishi kwa kua naye Genes alishaanza maisha yake mwenyewe basi walianza maisha rasmi wakiishi pamoja katika nyumba yao waliyoijenga maeneo ya Sakina.Waliishi maisha ya furaha wakifanya kazi kwa bidii,"natakasiku moja tuwe matajiri wa kwanza Tanzania" Miriam alimwambia Genes huku
akicheka,"yote yanawezekanatukifanya kazi kwa bidii" Genes alijibu.

0 comments:

Post a Comment