Huko Manyara nyumbani kwa Miriam walipata taarifa kuhusu mwanamke tajiri anayeitwa Miriam,mwenye asili ya kimasai,"usikute ni yule mtoto wetu aliyetoroka nyumbani?" Mzee Lizery alimwambia mke wake,"haiwezekani akawa huyo kwani yule itakua alifia msituni akitoroka mila zilizoletwa na mababu zetu" mama yake Miriam alijibu.Wote waliamini huyo mtoto wao alishaaga dunia kwani ni zaidi ya miaka kumi na tisatokea aondoke nyumbani.Maisha yalizidi kuwa mazuri na Genes alishaanza kuzunguka mikoni kuangalia biashara zake na mkewe.Asubuhi moja siku ya Jumamosi,Genesaliagana na mkewe Miriam kwa safari ya kuenda Dar es salam,"uwemakininjiani mme wangu" Miriam alimuaga mumewe kwa kumrukia na kupata denda kisha Genes akapanda ndani ya Toyota Prado nyekundu."byee mwaaaah!" Miriam alimuaga tena kwa kumpungia kupitia (side mirror) kioo cha pembeni.Ili kukwepa foleni Genes alikatiza Chalinze na kupitia barabara ya Bagamoyo na ndani ya masaananetayari alikua ameshaingia jijini Dar es salam."Ngoja nielekee Kawe nikatafute hotel ya kulala ili nipunge upepo wa baharitaratibu" Genes alijisemea,kwani alihitajika kupumzika ili kesho aamkiekukagua biashara zake.Jumapili mwendo wa saatatu asubuhi Genes alikua katikati ya foleni maeneo ya Morocco akisubiri taa zimruhusu,"mbona kama hii sura naijua?" Genes alijiuliza huku akishusha kioo cha gari na kumtazama mwanadada aliyekua akiomba msaada eneo lile,"eti dada samahani" Genes alijikuta akimuita dada huyo, na kwa haraka dada huyo alitii wito kwa furaha kwani ilikua nadra sana ombaomba kuitwa,"samahani nikuulize swali" Genes alianza maongezi huku akiwa bado kwenye gari akizidi kuvuta kumbukumbu juu ya msichana huyo,"ndio niulize" msichana huyo alijibu huku akitetemeka,"wewe unaitwa nani?" Genes aliuliza ila kabla hajajibiwa alishtushwa na mlio mkali wa honi,gari iliyokua nyuma ilimtaarifu kwani taa ya kijani ilishawaka kuashiria kupita.Genes aliondoa gari kuendelea na safari,yule dada alishuhudia tena gari ikienda na kuegesha pembeni ya barabara marabaada ya kuvuka mataa,hapo akaamini mazungumzo yataendelea. Hakuona sababu ya kukaa pale,alitoka haraka kulifuata gari liliposimama,"huyu kaka ana heshima sana kumbe angekuja hapa aliponiacha" huyo dadaalisema,na akiendelea kupiga hatua kubwa kumfuata."mbona kama nimekufananisha" Genes alianzisha tenamazungumzo,"na nani" dadaalijibu,"kwanza nambie unaitwa nani" Genes alirudia swali,"mimi naitwa Lissa" huyo dada alijibu baada ya kufikiria kwa sekunde tano, Genes alizidi kupata wasiwasi juu ya sura ile,"sasa samahani basi sio wewe" Genes alitamka hayo hukuakitokanoti yaelfu kumi na kumkabidhi,"asante sana,lakini mbona umeniuliza swali hilo la jina?" huyo dada alipokea pesa kisha
kuuliza,"apana dada nilikufananisha namsichana mmoja anayeitwa Angel, niliyesoma naye shule moja lakini yeye akitangulia kwa kidato kimoja" Genes aliongea maneno hayo na ghafla alishuhudia dadahuyo akitoa machozi na kilio kikubwa,"ndio mimihata wewe nimekufananisha na Genes,sijui kama ndio wewe" huyo dadaalijibu huku akijifuta machozi,"ndio mimi" Genes alijibu,"unaona navyoteseka kwa ajili yako"huyo dadaambaye kwa wakati huo ashaweka wazi jina lake kua ni Angel.Hakika Genes hakuamini macho yake kukutanana Angel mazingira yale wala haikumuingia akilini msichana aliyekua akitikisa shule nzima kwa uzuri alafu awe jinsi alivyokua,Genes aliona kama ndoto kwani kwa miaka mitatu Angel amebadilika sura,amekonda,na kuwa ombaomba barabarani.Genes hakutaka kuendelea kukaa naye maeneo yale,"twende tuondoke hapa" Genes alitamka kichwa kikiwa kimeinamishwa chini,"ngoja nipo na watoto wangu" Angel alisema na mara moja aliwaitwa watoto wake waliokua wamekaa pembeni ya barabara.Walikua watoto wawili mapacha,walivaa matambara yaliyoacha sehemu kubwa ya mwili wazi.Genes aliwaachukua na kurudi kwanza kufanya mazungumzo na Angel."ehe nambie Angel imekuaje hadi upo katika mazingira haya ambayo sijatarajia kama nitakukuta,Genes alianzisha maongezi wakiwa katika chumba kimoja pamoja na watoto wa Angel,"yani ni hadithi ndefu,ilakwa kifupi maishahaya yalianza siku ile tuliyofanya mapenzi pale chumbani kwangu,kwani baada ya siku ile wazazi wangu walikuja kugundua kwa kutumia camera za CCTV zilizofungwa ndani namimi nilikua sijui,na pia nilipata ujauzito wa hawa watoto hapa,lakini siunakumbuka tulifanya mapenzi nikiwa karibu nahitimu pale shuleni,hivyo basi maana na wewe ulinikataa baada ya kulala na mimi,nilikuja kufukuzwa nyumbani nikiwa na ujauzito wa miezi sitanikaja huku Dar es salaam nikajifungua nikiwa ombaomba hadi leo,hivyo hawa watoto hapa ni wako" Angel hakuweza kuendelea zaidi ya hapo kwani machozi yalishamjaa.Genes aliinua kichwa na kuwatazama watoto wake, kisha kuinama na kuanza kutoamachozi upya,"yaani miminakula na kusaza alafu kuna watoto wangu wanateseka njaa ?" Genes alijiuliza kimoyo moyo.Angel na watoto wake waliondoka na kuingia katika duka la nguo kila mmoja akavalishwa aliyoipenda,wakapatachakula Genes hakuamini macho yake kilekitendo kilichokua kikiendelea pale,bado aliamini ni ndoto.Baada ya kupata chakula na nguo Genes aliwachukua na kuwapeleka katika nyumba moja iloyopo Sinza."kaeni hapa nitakuja kuwatembelea mara kwa mara" Genes aliwapa makazi mapya na pesa za matumizi.Hapo alirudisha kumbukumbu nyuma na kukumbuka siku ya kwanza alivyokutana na Angel jinsi alivyozimia katikati ya tendo,yote hayo yalimfanya kumuona Angel hana makosa wala hastahili kuteseka hata kidogo.Baada ya siku tatu Genes alirejea Arusha,"mbona una mawazo sana mpenzi kuna nini huko" Miriam alimuuliza mumewe,
"acha tu mama watoto huko yaniwale mafundi wanaojenga nyumba yetu wanapeleka kazi taratibu sana itabidi niwe naenda mara kwa maraili wamalize mapema" Genes alimdanganya mkewe kwani uhalisia wa mawazo yake yalitokana na Angel.Genes aliwaza ni kwa jinsi gani angemweleza mkewe juu ya mambo yanayoendelea, hakutaka kupoteza uaminifu kwa mkewena hakutaka kuona Angel akiteseka na watoto wake. Hivyo safari za kuenda Dar es Salam ziliongezeka kadri siku zilivyoenda,Angel alianza kurudia uzuri wake, maziwa yalianza kusimama na weupe wake ulianza kuonekana,mapaja yalianza kutengeneza hips.Siku moja Genes alimuuliza Angel,"vipi una mpango gani?""miminikipata mume naolewa ila hawa watoto wako sasa""weweusiolewe kaa hapa hapa nitakua nakutunza na tutaendelea kufanya yetu".Baada ya hayo penzi lilianza upya kati ya Genes ana Angel kikubwa kilichozingatiwa ni mahusiano ya Miriam na Genes kwani Genes ashamueleza Angel kila kitu.Penzi lilizidi kukua,wale watoto mapacha waliitwa Eledy na Eledius,wote walifurahi sana kumjua baba yao.Miaka miwili badae Genes alikua akisafiri hukaa hata wiki moja bila kurudi nyumbani,"sasa Angel yule mke wangu sijui hazai au vipi""kwani vipi""tokea nimeoana naye hajapata mtoto kabisa",Yalikua mazungumzo kati ya Angel na Genes kumhusu Miriam ambaye kila alipobeba mimba ilitoka.***
HATUKUPENDA TUWE HIVI-33
18:39:00
No comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment