HATUKUPENDA TUWE HIVI-25

Author

Ilikua asubuhi yenye hali ya hewa iliyotulia vizuri, nyumbaji kwa marehemu Josephat siku hiyo kulitawaliwa na vilio na machungu yasiyopungua,vijana wenye nguvu walianza zoezi la kuchimba kaburi kwani ilikua siku ya kumzika Josephat,wazazi wake walilia kwa uchungu mama yake alipoteza fahamu mara kadhaa huku bado akiwa haamini kama mwanae kipenzi ndio kashakufa na atakiwa afukiwe ardhini mda mfupi ujao,
"jamani mwanangu siuamke kwenye  huo usingizi unaolala tangia jamani" mama marehemu aliongea kumuomba mwanae aamke kitu ambacho hakingewezekana kutokea milele. Wanafunzi waliokua wakisoma na marehemu walikua wakijiandaa kwa kuchangisha rambirambi, "jamani ndio hivo kashakufa,usilie sana mwaya Happy"ni maneno Angel aliyotamka kumpa moyo rafiki yake aitwae Happy,ambae alikua girlfriend (rafiki wa kike) wa marehemu, lakini Happy alizidi kulia kwa uchungu huku akiamini hakuna siku atakayomsahau rafiki  yake kipenzi, "juzi tu jamani tumeonana alafu leo unakufa mungu wangu nionee huruma nisaidie kumuamsha hata aniage basi nimpige busu la mwisho" Happy alizidi kulia kwa machungu, nguvu ya  mapenzi kwa upande wa Happy ilikua kubwa hadi akajikuta akiishiwa nguvu na kugaragara chini, "huyo analia nini au marehemu kafa na deni lake" Chris alitamka kwa madharau, "hata sielewi ila nimchumba wake bhana" Angel alijibu, "hata kama ni mchumba basi avunge maana atafanya wengine walie bure,kama vipi hata mimi mbona handsome tu" Chris aliongea kama utani lakini aliwakera sana wanafunzi wenzake kwa kauli zake chafu alizokua anatamka. *** "Huyu mtoto uchunguzi wake umefikia wapi?" baba wa marehemu alimuuliza askari mmoja aliyefika nyumbani kwake, "hii kesi kweli ni ngumu maana hata ushahidi mwenyewe tunashindwa kuupata maana binafsi tunaona kama yale mauaji hayamhusishi huyu tunayesema mhalifu" askari alijibu akiwa katazama chini, "basi hii kesi mimi namwachia mungu ndio muweza wa yote,ila nyie chunguzeni mjue hili tatizo linatoka wapi, mimi naamini mungu ndiye msemaji wa mwisho" baba wa marehemu alitamka kisha kuinama chini na kumwaga chozi kwa uchungu. *** Ilifika saa nne kamili ya asubuhi Anitha aliomba ruhusa ya kuenda kuangalia nyumba ya rafiki yake kwani alikabidhiwa kuangalia kila kitu, "dada samahani" ilikua sauti ya kijana mmoja aliyekua amesimama kama mita mia hivi kutoka kilipo chumba cha Miriam, "Bila samahani kaka" Anitha alijibu huku akihisi labda kijana yule alikua anaulizia njia au kuna kitu anataka kuulizia,hivyo alisimama na kuanza kumsikiliza, "kwanza pole na kazi dada" kijana yule alivaa suruli ya kitambaa na shati alilochomekea vizuri kitu kilichomfanya Anitha aone mwanaume wa heshima ambae hatamwambia mambo ya kihuni, "asante kaka nawe pia pole na kazi" Anitha alijibu huku akipokea salamu ya mkono aliyopewa, "nimeagizwa kwako dada" yule kijana aliongea huku akitoa karatasi mfukoni na kumkabidhi,Anitha alianza kuisoma,haikua na maandishi mengi sana, "MIMI MIRIAM,NIMEMTUMA HUYU KAKA AJE KUCHUKUA KILA KITU CHANGU HAPO NDANI,NIMEHAMA SITAKAA TENA HAPO KUNA MKOSI HIVYO MPE KILA KITU NA HAKIKISHA HAKIHARIBIKI KITU HAPO,BAADAE NITAKUJA KUKUJULISHA NILIKOHAMIA AU KAMA UNA MDA BASI ANDAMANA NAO HADI WANAKOPELEKA HIVYO VITU ILI UPAJUE."baada ya Anitha kusoma aliinua macho na kumtizama yule kijana kwa huzuni, "yaani huyu mtoto amenisumbua acha tu nimemwambia asubirie baadae aje ila  kalazimisha kua nije nitakukuta,sasa cha kufanya inabidi kwanza nikaone mizigo yenyewe ili nikalete gari
inayotoshea" kijana yule alinza kuongea tu mara baada ya Anitha kumwangalia. Ndani ya dakika tano Anitha na huyo kijana ambae hata jina hakujitambulisha basi walikua ndani ya chumba cha Miriam, na baadae waliingia katika banda la kuku, "ngoja nikalete gari", alisema kijana huyo na kuondoka

0 comments:

Post a Comment