HATUKUPENDA TUWE HIVI-24

Author

HADITHI,
HATUJAPENDA TUWE HIVI,
SEHEMU YA ISHIRINI NA NNE 24,
MTUNZI Deo Young Massawe,
MAWASILIANO, 0769297430.
                       sehemu ya 24.
   Taarifa ilizidi kusambaa kuhusu hilo tukio la kusikitisha na kila mtu  alilipokea kwa majonzi,katika familia ya Jesophat wanandugu walikua na hasira juu ya Miriam aliyegundulika kua muuaji,ila kwa upande wa watu wanaomjua vizuri Miriam basi walizidi kupata machungu wakiamini Miriam amesingiziwa kwani wanamjua alivyo na ukarimu kutoka moyoni.
"Hapa hadi tuandamane ndo wamuweke huru,sio mtu  wa kuua yule ni mtu  wakusaidia wasiokua na kitu" ni  maneno waliosema wafanyakazi wa hotel Aquiline huku nao wakiwa na majonzi makubwa.
                               *******
  "Katika kituoa cha police cha central basi madaktari walikua katika uchunguzi,wakiongozwa na doctor August,
"we dada ni kweli uliuwa au unasingiziwa?"
"ningeanzaje kumuua  huyo rafiki yangu?je kanikosea nini hadi nimuue?"
"na mbona ulisema  unataka kuua na wazazi wake katika yake maandishi?"
"maandishi yapi  tena mimi  sijaua mtu  wala sijui kitu yule ni rafiki angu mwenyewe nasikitika kwa kifo chake kwani nimepoteza mtu muhimu sana katika maisha yangu?"
"kwani ni mpenzi wako?"
"sio mpenzi ila ni zaidi ya mpenzi kwani mimi  nikishakua rafiki na mtu  basi tunakua  zaidi ya wapenz kabisa?".
  Hayo ni baadhi ya mahojiano ya madaktari waliofanya na Miriam akiwa chini ya ulinzi wa polisi kwani madaktari waliomba wafanye uchunguzi kidaktari
"sidhani kama ni huyu kaua,hapa kuna kitu" daktari August aliwaza kichwani mwake huku akitikisa kichwa kutoka kushoto kwenda kulia.
  Mzee Massawe nae alimwita askari mmoja pembeni na akawa anazungumza nae,
"hivi afande hapa mbona sielewi hili tatizo?"
"hilo mzee ndo hivo lishatokea huyu mtoto wa kike kaua yani bila huruma yani sidhani kama atakua uraiani tena" huyo askari alijibu kwa heshima kwani alijua anaongea na mtu  mwenye pesa,
"ila si kuna dhamana?" mzee  Massawe aliuliza kwa kumchokoza askari,
"hapatawezekana kua na dhamana kwanza kwa usalama wake.
"sasa hii kesi itakuaje,maana siamini kama huyu mtoto anaweza fanya hichi kitendo nimekaa nae mda mrefu sana hajawahi kunionesha jambo baya,nimekua nikimuamini sana ofisini kwangu" mzee Massawe aliongea mengi na huyo askari ila mwisho huyo askari alimpa moyo kwa kumwambia  uchunguzi utafanyika kwa makini na kisha itagundulika.
  Jioni ilifika Miriam aliwekwa rumande,
"naomba nimtumie  rafiki yangu ujumbe  aniangalizie nyumba  yangu" Miriam aliongea huku akitokwa na machozi,
"ujumbe gani?" Askari mmoja aliuliza kwa hasira,
"si aniangalizie nyumba yangu na kuku wangu naofuga" Miriam alijibu kwa hasira kwani alikua na machungu sana.
"haya karatasi hiyo hapo andika tumpe huyo boss wenu" aliongea askari mmoja huku akimkabidhi Miriam karatasi na kalamu, ila walishangazwa na Miriam kuomba msaada wa kuandikiwa,
"hujui hata kuandika wewe mwanamke utaolewa na nani" aliuliza kwa madharau askari mmoja mwanamke,
"nitaolewa na Genes" Miriam alijibu kwa tabasamu kwani aliona kama kaulizwa swali zuri sana,
"sema tuandike nini" huyo askari mwanamke aliuliza huku akishika kalamu tayari kuanza kuandika,
"MAMBO ANITHA,MIMI NI MIRIAM NAOMBA UNIANGALIZIE NYUMBA YANGU NA MIFUGO WANGU WOTE UHAKIKISHE WAPO SALAMA,ALAFU NASKIA KESHO NDO MAZISHI YA JESOPATH  HIVYO NAOMBA UNIWAKILISHE HUKO,USIACHE KUHUDHURIA MAZISHI NA UTOE PIA  RAMBIRAMBI YANGU,ZINGATIA UMAKINI HAPO NYUMBANI KILA KITU NIMEKUKABIDHI WEWE UFUNGUO CHUKUA PALE OFISINI KWANGU" Miriam alitaka hayo na kisha alimaliza kwa kilio kikubwa.
Karatasi alipewa mzee Massawe aipeleke kwa Anitha,
Pia madaktari waliokua pale walishangaa kumuona Miriam hajui kuandika,
"hii karatasi aliandikiwa na nani?" Dr August aliuliza wenzake,
"kweli hapa kuna utata" Dr mwingine alijibu,
"huyu kijana itakua alijiua mwenyewe,au alikua anatembea na hizi sumu,aidha ikamwingia bahati mbaya" Dr August alikua anasisitiza sana kwani kilichompa uhakika wa kumtetea Miriam ni ile  jumapili Josephat alivyoenda na sumu iliyomuua ofisini kwangu.
"Hii hapa karatasi mwenzako kanipa" mzee Massawe aliongea huku akimkabidhi Anitha karatasi, Anitha aliipokea na kuisoma  kisha alizidi kumwaga machozi,wafanyakazi wote walimwaga machozi kuskia mwenzao tena kipenzi cha watu kinalazwa rumande,
"kama hadi boss kashindwa kuhonga atoke basi ni kesi kubwa sana" alisema mfannyakazi mmoja kwani waliamini boss wao ataenda kuhonga pesa na Miriam atolewe.
Mda huo huo Anitha aliondoka na kuenda kwa Miriam kuanza shughuli ya kulisha kuku na badae kuenda kwake kufanya usafi kisha arudi kulala kwa Miriam kwani ndiko kulikua na miradi mingi.
                               *******
"Jaman poleni sana jirani zangu,ni kazi ya mungu" ni maneno ya Dr August alipofika kwa  marehemu Jesophat usiku wa mwisho kabla ya mazishi,
"kazi ya mungu yaani mtu  amuue alafu iwe kazi ya mungu?" baadhi ya waombolezaji walijibu kwa hasira.
Dr August alimuita baba wa marehenu na kukaa nae pembeni ambapo alimueleweshe kila kitu kuhusu sumu aliyokua nayo marehemu Josephat kabla ya ajali kumkuta,hadi mama wa marehemu alitwa na kusimuliwa,
"hivyo itakua kajidunga mwenyewe au vipi?" mama marehemu aliuliza kwa machungu,
"kweli hapo sijui ila kwa kweli yule mwanamke kule mahakamani hana hatia  yoyote" Dr August aliongea kwa uhakika,wazazi wote wa marehemu walishangaa sana na kuulizana wenyewe  kwa mwenyewe kwamba kwa nini yote hayo yatokee,
"sasa yale maandishi yanamaanisha nini,na kwa nn ayaandike?"mama Jesophat aliuliza,
"ndo nashangaa alafu yule mwanamke hajui kuandika hata kidogo" Dr August alijibu.
Wazazi wa marehemu walikua watu wenye huruma nahapo wakajikuta wakimhurumia Miriam zaidi hata ya mwanao aliyekufa,
"ngoja kesho asubuhi kabla mazishi tutamtoa na ikiwezekana kesi itafutwa,mungu ndo ataona hili na ndo atatoa hukumu kwa muuaji, sisi binadamu wote tunapita" baba wa marehenu alijikuta akitoa machozi kwa ajili ya Miriam anaeteseka rumande.
Waliendelea  kuomboleza, huku vijana wakicheza karata,wazee walicheza bao  na wengine wakicheza drafti ilimradi tu mtu  asilale,wote walisubiria kesho ifike kwa ajili ya mazishi,na wanafunzi waliokua wanasoma na marehenu Josephat walisubiria kwa hamu siku ya mazishi kila mmoja akiwa na sababu yake,
wengine wakitaka kuandamana na marafiki zao wa jinsia tofauti, pia waliokua  hawapendi masomo basi walifurahia sana siku kama hizo kwani.
Kwa Miriam ilikua ni kilio kisichoisha,
"itakua Genes au yule mwanamke wake ananisingizia mimi  nifungww ile nisije kuolewa nae" Miriam alijisemea ila bado aliamini mapenzi yake kwa Genes hayatapungua kamwe,
"natamani hata nihudhirie mazishi" Miriam alijisemea kisha alizidi kuangua kilio.

Itaendelea

Kama unahitaji script (story) za  filamu  za aina zote, unaweza nichek inbox tufanye biashara kwani nitakutolea kitu cha kipekee, ambacho kila mtu  atapendezwa kuangalia movie yako,,,,,,, hata kwa mnaojua kuimba jaman naweza kukuandikia mashairi yenye viwango ,,,,,

0 comments:

Post a Comment